Rais anayekuja kazi yake kubwa iwe kurudisha nchi kwenye uchumi wa kati

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
8,105
Reaction score
20,307
Benki ya dunia na IMF mwaka 2019 viliitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati baada ya maboresho makubwa ya kiuchumi yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano iliyokuwa ikiongozwa na hayati Magufuli na Makamu wake Samia.

Serikali ya awamu ya tano ilifikia hayo mafanikio ya kuingiza nchi uchumi wa kati baada ya kubana matumizi, kudhibiti ufisadi, kujenga viwanda na kuhimiza wananchi kuchapa kazi kwa nguvu zao zote.

Hali ilibadilika ghafla baada ya Rais Samia kuapishwa serikali yake ya awamu ya sita ikaacha kuhubiri viwanda wala wananchi wake kuchapa kazi na akatangaza sera mpya ya kula kulingana na urefu wa kamba yako! Matokeo yake ni kuuzwa kwa sekta muhimu za kuingizia nchi kipato kama bandari zote na makaa ya mawe.
Kutokana na kuzorota huku kwa usimamizi wa rasilimali za taifa Tanzania imeshushwa kutoka uchumi wa kati na sasa haieleweki iko uchumi gani!

Hivyo Rais ajaye baada ya Samia atakuwa na kazi kubwa ya kubana matumizi, kudhibiti ufisadi serikali, kulinda rasilimali za taifa na kuirudisha nchi uchumi wa kati tena.

Kuna kila aina ya ushahidi kuwa Rais Samia amekata tamaa na haumizi kichwa tena kuhusiana na shida za watanzania ila inaonekana awamu yake hii ya pili alijipanga kula raha na kusafiri sana duniani ila mauwaji ya oktoba 29 yamempunguza speed baada ya kupigwa marufuku kusafiri ndani ya nchi za Ulaya.
 
Ukifanya kazi eneo moja kwa muda mrefu huwa inapunguza morale wakati mwingine

Sasa mtu yupo hapo tangu 2015, hakuna anayemkumbusha majukumu yake ya msingi

Unategemea atakuja na jipya gani

Washauri wake wenyewe akina Profesa, badala ya kumshauri sawasawa, wao wanamwambia tu Kila kitu kipo sawa

Hali ya huduma ya Maji imefikia asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mjini

Lakini ukiwauliza wakazi wenyewe wa DSM, watu hawajapata huduma tangu mwaka Jana

Kwenye miundominu napo hivyo, wanamwambia hakuna Rais amejenga mtandao Mkubwa wa lami kama yeye

Lakini ukitembea barabara KUU zote, unakutana na mashimo kama bwawa la mtera

Kwenye pembejeo hivyo, ni kuimba kwamba yeye ndiyo amefanya vizuri kuliko wengine wote tangu Nchi ipate Uhuru

Lakini ukija kwa wakulima wenyewe, unakuta wanauziwa pembejeo ghali kuliko kawaida

Masoko kwa mazao yao napo ni shida

Ila washauri wake wanamwambia Kila kitu Kiko bomba 🙌
 
Benki ya dunia na IMF mwaka 2019 viliitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati baada ya maboresho makubwa ya kiuchumi yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano iliyokuwa ikiongozwa na hayati Magufuli na Makamu wake Samia.
Serikali ya awamu ya tano ilifikia hayo mafanikio ya kuingiza nchi uchumi wa kati baada ya kubana matumizi, kudhibiti ufisadi, kujenga viwanda na kuhimiza wananchi kuchapa kazi kwa nguvu zao zote.
Hali ilibadilika ghafla baada ya Rais Samia kuapishwa serikali yake ya awamu ya sita ikaacha kuhubiri viwanda wala wananchi wake kuchapa kazi na akatangaza sera mpya ya kula kulingana na urefu wa kamba yako! Matokeo yake ni kuuzwa kwa sekta muhimu za kuingizia nchi kipato kama bandari zote na makaa ya mawe.
Kutokana na kuzorota huku kwa usimamizi wa rasilimali za taifa Tanzania imeshushwa kutoka uchumi wa kati na sasa haieleweki iko uchumi gani! Hivyo Rais ajaye baada ya Samia atakuwa na kazi kubwa ya kubana matumizi, kudhibiti ufisadi serikali, kulinda rasilimali za taifa na kuirudisha nchi uchumi wa kati tena.
Kuna kila aina ya ushahidi kuwa Rais Samia amekata tamaa na haumizi kichwa tena kuhusiana na shida za watanzania ila inaonekana awamu yake hii ya pili alijipanga kula raha na kusafiri sana duniani ila mauwaji ya oktoba 29 yamempunguza speed baada ya kupigwa marufuku kusafiri ndani ya nchi za Ulaya.
Kweli kabisa yupo yupo tu kila kona anapigwa spana
 
Ukifanya kazi eneo moja kwa muda mrefu huwa inapunguza morale wakati mwingine

Sasa mtu yupo hapo tangu 2015, hakuna anayemkumbusha majukumu yake ya msingi

Unategemea atakuja na jipya gani

Washauri wake wenyewe akina Profesa, badala ya kumshauri sawasawa, wao wanamwambia tu Kila kitu kipo sawa

Hali ya huduma ya Maji imefikia asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mjini

Lakini ukiwauliza wakazi wenyewe wa DSM, watu hawajapata huduma tangu mwaka Jana

Kwenye miundominu napo hivyo, wanamwambia hakuna Rais amejenga mtandao Mkubwa wa lami kama yeye

Lakini ukitembea barabara KUU zote, unakutana na mashimo kama bwawa la mtera

Kwenye pembejeo hivyo, ni kuimba kwamba yeye ndiyo amefanya vizuri kuliko wengine wote tangu Nchi ipate Uhuru

Lakini ukija kwa wakulima wenyewe, unakuta wanauziwa pembejeo ghali kuliko kawaida

Masoko kwa mazao yao napo ni shida

Ila washauri wake wanamwambia Kila kitu Kiko bomba 🙌
Inasikitisha sana pengo la Urais liko wazi kabisa
 
Mwigulu, Ridhiwani, Ndejembi, Samia na Makamba sioni wa kufanya unachokisema. Actually, CCM kule hakuna anayeweza hata kidogo. Labda Tundu Lissu tumpe ajaribu kupambana na mafisadi. Yasipomuua anaweza!
tapatalk_1439129242584.jpeg
 
Mwigulu, Ridhiwani, Ndejembi, Samia na Makamba sioni wa kufanya unachokisema. Actually, CCM kule hakuna anayeweza hata kidogo. Labda Tundu Lissu tumpe ajaribu kupambana na mafisadi. Yasipomuua anaweza!
View attachment 3675801
Deo Mwanyika au Antony Mtaka ndio watu ninaowaona kama transformative wakipewa nafasi ya kushika hicho kiti kutokana na uwezo wao japo hawazungumzwi sana
 
Apore pesa za wafanya biashara wote kama kawaida ili kuwafurahisha wasio na cha kupoteza!
... ONLY IN BONGOLAND!
 
Tanzania ipo Uchumi wa kati, hivi JF inaruhusu vipi content za kijinga kama hizi? Na tuliingia Uchumi wa kati 2014, Magu alitushusha ila tulivyorudi propaganda nyingi watu wakajua ndio first time.

The so called Uchumi wa kati ni kuwa na GDP per Capita zaidi ya 1100 it's nothing special, sasa hivi sisi tupo around 1300.
 
Lete ushahidi
 
Lete ushahidi
World bank
Screenshot_20260922-173103~2.jpg

Source

Sijui mnatoa wapi taarifa zenu, huu uongo mara kwa mara unarudiwa humu jukwaani, kujua kama nchi ni middle ama lower income unaangalia tu GDP per Capita haiwezekani ufike 1300-1400 GDP per Capita na usiwe middle income.
 
World bank
View attachment 3675838
Source

Sijui mnatoa wapi taarifa zenu, huu uongo mara kwa mara unarudiwa humu jukwaani, kujua kama nchi ni middle ama lower income unaangalia tu GDP per Capita haiwezekani ufike 1300-1400 GDP per Capita na usiwe middle income.
Duh
 
Uchumi wa kati wa juuu hahahaha siku hizi sisikiii hizo kelele tena za uchumi sijui wa kati daah
 
Back
Top Bottom