Rais atoe taarifa za kweli juu ya tozo na fedha za IMF

Rais atoe taarifa za kweli juu ya tozo na fedha za IMF

Nawatania

Senior Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
148
Reaction score
549
Rais Samia awe makini kukwepa kusema uongo mbele ya umma

Rais Magufuli alipenda propaganda ndio maana watu werevu walimchoka mapema kwa propaganda

Alichukua pesa za michango ya rambirambi Bukoba na kwenda kufanyia mambo mengine kabisa. Mara tunajenga kwa pesa zetu

Sasa na Samia ameanza kuingia kwenye mtego wa uongo kama mtangulizi wake. Wiki iliyopita akienda Bagamoyo alisimama Tegeta na kuwaaminisha watanzania kwamba tozo zinahitajika ili kujenga madarasa.

Na akasisitiza misaada na mikopo sio mizuri kutoka kwa wazungu.

Ila Leo kashachukua pesa za IMF za kupambana na athari za covid 19 kwenda zaidi ya trilioni moja baada ziende kwenye athari za covid kama kuimarisha sector ya utalii na kukopesha wafanyabiashara waliopoteza mitaji yeye anapeleka pesa kwenye madarasa?

Kipaumbele Cha tozo ni madarasa na kipaumbele Cha mkopo wa IMF ni madarasa.

Tozo hazitoshi? Wakati ndani ya wiki nne zinakusanywa zaidi ya billion 50 maana yake kwa mwaka ni billion 600 hizi pesa zote zitaenda wapi?

Allocation of resources hakuna tena wakati Rais Mchumi, Makamo wake Mchumi, Waziri wa fedha yupo ila bado wanachukua pesa kwa ajiri ya athari za Corona wao wanapeleka kwenye madarasa kumbukeni Kila kitu ni muhimu.

Kuna wafanyakazi kwenye hoteli za kitalii wanadai bado mishahara ya mwaka Jana.

Kuna makampuni yalikopa mikopo mikubwa benk na mdororo wa kiuchumi umewafanya kupunguza wafanyakazi.

Kuna sector ya anga kesho mtakuja tena kusema ITCL imepata hasara wakati hamuwezi hata kulinda makampuni ya umma.

Rais unatukwaza Sana acha kudanganya umma kwamba madarasa yanajengwa na tozo wakati unakopa pesa nje kujenga madarasa.
 
we kweli unamatatizo, kwaiyo pesa ya tozo kama inajenga mafarasa, hatakiwi kuongezea nyingine,

vipi ulikua unahitaji mkoponaimag

We kweli una matatizo, kwa hiyo pesa ya tozo kama inajenga madarasa, hatakiwi kuongezea nyingine,

vipi ulikuwa unahitaji mkopo?
Hivi billion 300 kwa mfano zinaweza kujenga madarasa mangapi ? Ambayo ni pesa ya tozo kwa miezi 6 tu?
 
Kazi gani???
Mkuu, huzioni?

Leo tu yenyewe kuna mawaziri wapya wameapishwa, kabla ya hapo kulikuwa na uteuzi na usisahau uteuzi ulifanyika akiwa ziarani kuandaa documentary ya kuiingizia nchi kipato, kabla ya hapo, tozo zililetwa rasmi, nyuma ya hapo alikamatwa kiongozi wa chama cha siasa, nyuma yake chanjo ya uviko-19 ilianza rasmi, nyuma zaidi tulitembelewa na akina Tony Blair na wengineo, ukirudi zaidi kulikuwa na safari za nje kadhaa, kipindi hicho pia tukapewa misaada kede kede ya uviko-19

Na sasa tunashukuru pesa ni nyingi mtaani, watanzania wote wana furaha.
 
Sema anakukwaza mimi namuona muwazi sana sio kama tapeli yule
 
Mliongea sana oooh ANAUPIGA MWINGI leo mnaanza kulialia hapa, vumilieni tu ndo kwaanza tunautafuta mwaka wa kwanza.

Nakukumbusha msemo ule usioisha makali; "Mwanasiasa akikwambia toka nje kuna giza, jiongeze mwenyewe uende ukahakikishe kweli kuna giza"
 
Mara anataka kujenga madarasa, Mara barabara vijijini, Mara zahanati. Ni Kama nao hawaelewi, leo watasema tozo ni kwa ajili ya madarasa, kesho watasema ni kwa ajili ya zahanati, kesho kutwa watasema ni kwa ajili ya barabara za vijijini
Huyu bibi tumepigwa
 
Back
Top Bottom