Rais awasamehe Makamishina walioshirikiana na Kangi Lugola uliokuwa na viashiria vya ufisadi

Yajayo.... kauli mbiu ya bunge la 11
 
Eti huyu ndio mtu anaechukia ufisadi na ndio aliahidi kuanzisha mahakama ya mafisadi!!!
Yaani nawashangaa hata wale jamaa zake wa Lumumba, kila siku wanamsifu huyu jamaa kuwa eti yeye ndiye mpambanaji wa ufisadi??

Hivi ingekuwa hivyo ndiyo tungeona ununuaji wa wabunge wa upinzani nchini ambao umeweka rekodi, ya wakati wote??
 
Kesi ya mbunge shapu nayo pia itapitia njia ya kutubu
 
zingatia unapoombwa msamaha na mtu akatubu makosa yake inakupasa kumsamehe, sijaona alipokosea kama aliombwa msamaha na akasamehe kweli
Tambua kuwa yeye Rais ni Mtumishi wa Umma, kama huyo Kamishna Andengenye angekuwa amemkosea yeye binafsi, nisengekuwa na mashaka na msamaha wake, lakini ni yeye mwenyewe alitutangazia kuwa Andengenye ameingia mkataba wa kifisadi wa shilingi trillion moja, kwa maana hiyo hilo suala limegeika na kuwa ni la Umma, kwa hiyo tunaopaswa kusamehe ni sisi wananchi wote wa Taifa hili na wala siyo kwa yeye binafsi peke yake Rais Magufuli
 
ESCROW wallipiga TSHS 340 billions, lakini wakina kangi tunaambiwa waliingiza taifa hasara ya Bills 1000, mpaka leo akina Rugemalira wako ndani lakini hawa wamesamehewa.

Hapo ndipo utajua kuwa dunia ina mambo mpaka jogoo anaweza taga.
Nafaka
Hiyo ndiyo inayoitwa kwenye idara ya sheria kuwa ni "double standards"

Ambayo ni kitu kibaya sana kwenye taaluma ya sheria
 
Ooh sijui napambana na ufisadi , hakuna lolote unafiki mtupu
 
Mambo mengine tujizuwie kuongea sana ila tuamini kile kimeshasemwa amemsamehe kwa dhati. Sasa wewe endelea kumchunguza uwone yatakayo kukuta. Amesha samehewa. End
 
Binafsi sishangai Rais kumsamehe mtu aliesemekana kuingia mkataba wa Tril1. Sababu hata alivomtuma Kinana kwenda kutibiwa India sikushangaa pia.
 
Mungu-mtu siyo?
 
ESCROW wallipiga TSHS 340 billions, lakini wakina kangi tunaambiwa waliingiza taifa hasara ya Bills 1000, mpaka leo akina Rugemalira wako ndani lakini hawa wamesamehewa.

Hapo ndipo utajua kuwa dunia ina mambo mpaka jogoo anaweza taga.
Hao wazee wadhikiri kabisa huyu bwana aishie October tu anavopenda bifu na ligi akirudi watasubiria ushahidi kukamilika Hadi atakapoondoka madarakani haijalishi ni lini.Au la wapige goti wakae mezani wanagain wanunue Uhuru wao.
 
MOJA WAPO YA sifa moja kubwa ya utawala huu ambayo inabidi iandikwe kwenye vitabu ni PERSECUTION.
Retired
Halafu bado wapo wanamuomwamini akisimama juu ya majukwaa na kudai kuwa MAENDELEO HAYANA CHAMA!

Wakati yeye mwenyewe ndiye kinara wa kuvichukia vyama vya upinzani, especially Chadema!
 
Kusema kweli sijui awamu hii inapeleka wapi nchi hii, matumizi ya fedha za umma ni namna watawala wanavyotaka zitumike, nani asamehe, nani ahukumiwe, nani atoswe, wapi fedha zipelekwe, wapi wanyimwe!
 
Niliwahi kusema kuwa msishangae ikija kugundulika kuwa awamu hii ndio ilisheheni kwa ufisadi kuliko awamu zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…