Rais awasamehe Makamishina walioshirikiana na Kangi Lugola uliokuwa na viashiria vya ufisadi

Rais awasamehe Makamishina walioshirikiana na Kangi Lugola uliokuwa na viashiria vya ufisadi

Atake asitake tutamshinikiza aendelee kuwa Rais ili kuhakikisha wenye akili na maarifa na mafanikio kama Nyinyi muishi kwa huzuni na sie Mafala wajinga wajinga tuendelee ku enjoy
Acha kushabikia ujinga . Zuzu wewe
 
Magufuli hataki maadui wa kudumu na uchaguzi huo unakaribia napia siumeona anavyo wakataa vibaraka wake wasimuingize Choo cha kike kwa Masirahi ya matumbo yao na familia zao Magufuli anajielewa mkuu hataki maadui na hataki kuongeza muda anaheshimu katiba ya nchi yetu na chama chake. Pongezi kwake viva magufuli Safi kwa point ulizoongea leo
 
Sisi tutamuongezea kwa lazima
 
Rais anahuruma na Upendo Sana hata akikasika vipi watu wakiiba ,huwa anawasamehe!
Kumbuka wale wezi wa msbonge ya dhahabu Mwanza na Hawa wa Trilioni za Zima Moto ....hapa kazi tu!
 
Atake asitake tutamshinikiza
Pale mnapodanganya watu hakuna zaidi ya magufuli
FB_IMG_15918986877281735.jpeg
 
Leo Akifungua ofisi za kikosi Cha Zimamoto Dodoma,ametamka kuwasamehe maofisa waliohusika na utiaji saini wa tender ya kununuliwa vifaa vya Zimamoto toka kwa Wakoloni.Maana yake Kange Lugola saa hizi ni kicheko,hakuna Cha takukuru wala harufu ya Ukonga.Ila najiuliza huruma hii ya Magu imeanza lini?
Hizo fedha za kununulia vifaa vya zimamoto zilikuwa mali ya Magufuli au za Serikali ya watanzania?
 
Magufuli hataki maadui wa kudumu na uchaguzi huo unakaribia napia siumeona anavyo wakataa vibaraka wake wasimuingize Choo cha kike kwa Masirahi ya matumbo yao na familia zao Magufuli anajielewa mkuu hataki maadui na hataki kuongeza muda anaheshimu katiba ya nchi yetu na chama chake. Pongezi kwake viva magufuli Safi kwa point ulizoongea leo
Mbona ana saving ya maadaui wa kutosha na wengine wanatoa interest!
 
Nitapambana Na Rushwa Bila Kigugumizi Chochote Na Dawa Ya Jipu Ni Kulitumbua
Nimejipa Kazi Ya Mtumbua Jipu
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Atake asitake tutamshinikiza aendelee kuwa Rais ili kuhakikisha wenye akili na maarifa na mafanikio kama Nyinyi muishi kwa huzuni na sie Mafala wajinga wajinga tuendelee ku enjoy
Yaani sisi wa kanda pendwa.... hii ni zamu yetu
 
Yan hata akikataa tutafanya Kama kwa Mbowe tulivyo fanya
Tutachanga hela ya fom tumchulie alafu tumpelekee mpaka chato [emoji1787][emoji1787]
 
Magufuli hataki maadui wa kudumu na uchaguzi huo unakaribia napia siumeona anavyo wakataa vibaraka wake wasimuingize Choo cha kike kwa Masirahi ya matumbo yao na familia zao Magufuli anajielewa mkuu hataki maadui na hataki kuongeza muda anaheshimu katiba ya nchi yetu na chama chake. Pongezi kwake viva magufuli Safi kwa point ulizoongea leo
Hujaongelea ile sumu aliyopewa mangula
 
Tumemsikia wenyewe Rais Magufuli siku ya Jana kuwa amemsamehe aliyekuwa Kamishna Mkuu wa kikosi cha Zimamoto, Thobias Andengenye kwa madai kuwa amemuomba msamaha.

Tukumbuke kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Magufuli alimtumbua Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na Kamishna huyo, Thobias Andengenye kwa madai kuwa wameingia mkataba unaokadiriwa kuwa wa Eoro mikioni 408, sawasawa na shilingi za kitanzania trillion moja., kinyume cha taratibu kwa kuwa mkataba huo haujapitia Bungeni kama zinavyoagizwa na sheria za nchi yetu.

Baada ya kutumbuliwa huko kwa Waziri Kangi Lugola na Kamishna huyo Thobias Andengenye, tukaambiwa kuwa TAKUKURU wanawachunguza watu hao na ikithibitika kuwa waliingia mkataba huo kinyume cha taratibu, basi wataburuzwa mahakamani ili wakajibu mashitaka yao.

Hata hivyo imepita takribani miezi 5 hatujasikia taarifa yoyote ya uchunguzi huo wa TAKUKURU unavyoendelea na ndiyo hiyo Jana tememsikia Rais Magufuli akidai kuwa amemsamehe huyo Kamishna Thobias Andengenye!

Swali tunalojiuliza hivi Rais Magufuli ana uwezo wa kuwasamehe hao kina Kangi Lugola ambao yeye mwenyewe alidai waliingia mkataba ulioliingizia Taifa letu hasara ya shilingi trillion moja?

Je uchunguzi wa TAKUKURU hivi sasa unaendeshwa na Rais Magufuli, kwa kuwaelekeza hao TAKUKURU wa-STOP kuendelea na uchunguzi, pale anapojisikia kufanya hivyo?

Tunajua kuwa kwa tuhuma nzito hiyo ya kuingia mkataba uliolitia hasara Taifa hili la takribani shilingi trillion moja, ni wajibu wetu sisi wananchi kushinikiza kuwa kama kweli watu hao wamelitia hasara Taifa hili kiasi hicho kikubwa sana cha pesa, basi wawajibishwe wakajibu tuhuma hizo mahakamani na siyo kwa Rais wetu kutoa msamaha wa kienyeji.

Kwa kuwa pesa hiyo tuliyoambiwa na Rais wetu kuwa watu hao wamelitia hasara Taifa hili ni pesa za walipa kodi wa nchi hii na.wala siyo pesa za Rais Magufuli.

Tutambue kuwa wapo watanzania wengi ambao wapo magerezani kwa kesi ndogo ndogo za kuiba kuku, iweje kwa hao tulioambiwa na Rais wetu kuwa wamelitia hasara Taifa hili kiasi kikubwa hicho cha pesa zinazokadiriwa kuwa shilingi trillion moja wapewe msamaha kirahisi rahisi hivyo?

Naomba wasomaji wa JF, tudadavue kama ni sahihi kwa Rais wetu kutoa misamaha ya aina hiyo wakati vyombo vya uchunguzi vya TAKUKURU vinavyoshughulikia tuhuma hizo kabla havijatoa taarifa yao ya namna uchunguzi wao ulipofikia tamati.
 
ESCROW wallipiga TSHS 340 billions, lakini wakina kangi tunaambiwa waliingiza taifa hasara ya Bills 1000, mpaka leo akina Rugemalira wako ndani lakini hawa wamesamehewa.

Hapo ndipo utajua kuwa dunia ina mambo mpaka jogoo anaweza taga.
 
Back
Top Bottom