Rais awasamehe Makamishina walioshirikiana na Kangi Lugola uliokuwa na viashiria vya ufisadi

Rais awasamehe Makamishina walioshirikiana na Kangi Lugola uliokuwa na viashiria vya ufisadi

Absolutely true

Jaribu kufikiria kwa mfano ile kesi ya aliyekuwa DC, Alexander Mnyeti, ambapo aliyekuwa mbunge wa Aru Meru ya Mashariki kutoa ushahidi wa video clip kwa TAKUKURU, namna huyo Mnyeti anavyowahonga hao madiwani wa Chadema, badala ya kufanyika uchunguzi huo, ndiyo kwanza huyo Mnyeti akapata "promotion" na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara!
Yajayo.... kauli mbiu ya bunge la 11
 
Eti huyu ndio mtu anaechukia ufisadi na ndio aliahidi kuanzisha mahakama ya mafisadi!!!
Yaani nawashangaa hata wale jamaa zake wa Lumumba, kila siku wanamsifu huyu jamaa kuwa eti yeye ndiye mpambanaji wa ufisadi??

Hivi ingekuwa hivyo ndiyo tungeona ununuaji wa wabunge wa upinzani nchini ambao umeweka rekodi, ya wakati wote??
 
zingatia unapoombwa msamaha na mtu akatubu makosa yake inakupasa kumsamehe, sijaona alipokosea kama aliombwa msamaha na akasamehe kweli
Tambua kuwa yeye Rais ni Mtumishi wa Umma, kama huyo Kamishna Andengenye angekuwa amemkosea yeye binafsi, nisengekuwa na mashaka na msamaha wake, lakini ni yeye mwenyewe alitutangazia kuwa Andengenye ameingia mkataba wa kifisadi wa shilingi trillion moja, kwa maana hiyo hilo suala limegeika na kuwa ni la Umma, kwa hiyo tunaopaswa kusamehe ni sisi wananchi wote wa Taifa hili na wala siyo kwa yeye binafsi peke yake Rais Magufuli
 
ESCROW wallipiga TSHS 340 billions, lakini wakina kangi tunaambiwa waliingiza taifa hasara ya Bills 1000, mpaka leo akina Rugemalira wako ndani lakini hawa wamesamehewa.

Hapo ndipo utajua kuwa dunia ina mambo mpaka jogoo anaweza taga.
Nafaka
Hiyo ndiyo inayoitwa kwenye idara ya sheria kuwa ni "double standards"

Ambayo ni kitu kibaya sana kwenye taaluma ya sheria
 
Ooh sijui napambana na ufisadi , hakuna lolote unafiki mtupu
 
Tumemsikia wenyewe Rais Magufuli siku ya Jana kuwa amemsamehe aliyekuwa Kamishna Mkuu wa kikosi cha Zimamoto, Thobias Andengenye kwa madai kuwa amemuomba msamaha.

Tukumbuke kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Magufuli alimtumbua Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na Kamishna huyo, Thobias Andengenye kwa madai kuwa wameingia mkataba unaokadiriwa kuwa wa Eoro mikioni 408, sawasawa na shilingi za kitanzania trillion moja., kinyume cha taratibu kwa kuwa mkataba huo haujapitia Bungeni kama zinavyoagizwa na sheria za nchi yetu.

Baada ya kutumbuliwa huko kwa Waziri Kangi Lugola na Kamishna huyo Thobias Andengenye, tukaambiwa kuwa TAKUKURU wanawachunguza watu hao na ikithibitika kuwa waliingia mkataba huo kinyume cha taratibu, basi wataburuzwa mahakamani ili wakajibu mashitaka yao.

Hata hivyo imepita takribani miezi 5 hatujasikia taarifa yoyote ya uchunguzi huo wa TAKUKURU unavyoendelea na ndiyo hiyo Jana tememsikia Rais Magufuli akidai kuwa amemsamehe huyo Kamishna Thobias Andengenye!

Swali tunalojiuliza hivi Rais Magufuli ana uwezo wa kuwasamehe hao kina Kangi Lugola ambao yeye mwenyewe alidai waliingia mkataba ulioliingizia Taifa letu hasara ya shilingi trillion moja?

Je uchunguzi wa TAKUKURU hivi sasa unaendeshwa na Rais Magufuli, kwa kuwaelekeza hao TAKUKURU wa-STOP kuendelea na uchunguzi, pale anapojisikia kufanya hivyo?

Tunajua kuwa kwa tuhuma nzito hiyo ya kuingia mkataba uliolitia hasara Taifa hili la takribani shilingi trillion moja, ni wajibu wetu sisi wananchi kushinikiza kuwa kama kweli watu hao wamelitia hasara Taifa hili kiasi hicho kikubwa sana cha pesa, basi wawajibishwe wakajibu tuhuma hizo mahakamani na siyo kwa Rais wetu kutoa msamaha wa kienyeji.

Kwa kuwa pesa hiyo tuliyoambiwa na Rais wetu kuwa watu hao wamelitia hasara Taifa hili ni pesa za walipa kodi wa nchi hii na.wala siyo pesa za Rais Magufuli.

Tutambue kuwa wapo watanzania wengi ambao wapo magerezani kwa kesi ndogo ndogo za kuiba kuku, iweje kwa hao tulioambiwa na Rais wetu kuwa wamelitia hasara Taifa hili kiasi kikubwa hicho cha pesa zinazokadiriwa kuwa shilingi trillion moja wapewe msamaha kirahisi rahisi hivyo?

Naomba wasomaji wa JF, tudadavue kama ni sahihi kwa Rais wetu kutoa misamaha ya aina hiyo wakati vyombo vya uchunguzi vya ulivyoambiwa vya TAKUKURU vinavyoshughulikia tuhuma hizo kabla havijatoa taarifa yao ya namna uchunguzi wao ulipofikia tamati.
Mambo mengine tujizuwie kuongea sana ila tuamini kile kimeshasemwa amemsamehe kwa dhati. Sasa wewe endelea kumchunguza uwone yatakayo kukuta. Amesha samehewa. End
 
Tambua kuwa yeye Rais ni Mtumishi wa Umma, kama huyo Kamishna Andengenye angekuwa amemkosea yeye binafsi, nisengekuwa na mashaka na msamaha wake, lakini ni yeye mwenyewe alitutangazia kuwa Andengenye ameingia mkataba wa kifisadi wa shilingi trillion moja, kwa maana hiyo hilo suala limegeika na kuwa ni la Umma, kwa hiyo tunaopaswa kusamehe ni sisi wananchi wote wa Taifa hili na wala siyo kwa yeye binafsi peke yake Rais Magufuli
Binafsi sishangai Rais kumsamehe mtu aliesemekana kuingia mkataba wa Tril1. Sababu hata alivomtuma Kinana kwenda kutibiwa India sikushangaa pia.
 
Mungu-mtu siyo?
Magufuli anapenda sana kunyenyekewa kuliko kawaida.

Ukijinyrnyekeza kwake na 'ukatubu' anakusamehe dhambi zako zote.

Andengenye ni kachero wa tiss, hivyo atakua ameomba radhi sana kupitia kina Diwani, kina Mabeyo, kina Siro na wengine. Maombi yake yamemfikia mzee kwenye kiti chake cha kunesa nesa amesamehewa

Hii kitu ilikua staged from the beginning, unakumbuka mbwembwe za takukuru kila mara updates za uchunguzi, kukamilika uchunguzi na kupeleka jarada kwa dpp kwa makosa ya uhujumu uchumi halafu kimia kizito hadi leo.

Kuna walioshirikiana na Andengenye wote amesema amewasamehe na amewaacha pale pale zimamoto waendelee kula maisha. Anasema akiwaangalia tu anaona wana nyuso za kutubu na yeye kama msamehe na msikia toba hana sababu ya kutowasamehe.

Mzee anachopenda ni uwe tayari kukis his ass. Kina ruge bado wako jela kwa sababu ya ujeuri wao, hawataki kukis his ass.
 
ESCROW wallipiga TSHS 340 billions, lakini wakina kangi tunaambiwa waliingiza taifa hasara ya Bills 1000, mpaka leo akina Rugemalira wako ndani lakini hawa wamesamehewa.

Hapo ndipo utajua kuwa dunia ina mambo mpaka jogoo anaweza taga.
Hao wazee wadhikiri kabisa huyu bwana aishie October tu anavopenda bifu na ligi akirudi watasubiria ushahidi kukamilika Hadi atakapoondoka madarakani haijalishi ni lini.Au la wapige goti wakae mezani wanagain wanunue Uhuru wao.
 
MOJA WAPO YA sifa moja kubwa ya utawala huu ambayo inabidi iandikwe kwenye vitabu ni PERSECUTION.
Retired
Halafu bado wapo wanamuomwamini akisimama juu ya majukwaa na kudai kuwa MAENDELEO HAYANA CHAMA!

Wakati yeye mwenyewe ndiye kinara wa kuvichukia vyama vya upinzani, especially Chadema!
 
Kusema kweli sijui awamu hii inapeleka wapi nchi hii, matumizi ya fedha za umma ni namna watawala wanavyotaka zitumike, nani asamehe, nani ahukumiwe, nani atoswe, wapi fedha zipelekwe, wapi wanyimwe!
 
Niliwahi kusema kuwa msishangae ikija kugundulika kuwa awamu hii ndio ilisheheni kwa ufisadi kuliko awamu zote.
 
Back
Top Bottom