mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
[emoji125][emoji125][emoji125]
Tumemsikia wenyewe Rais Magufuli siku ya Jana kuwa amemsamehe aliyekuwa Kamishna Mkuu wa kikosi cha Zimamoto, Thobias Andengenye kwa madai kuwa amemuomba msamaha.
Tukumbuke kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Magufuli alimtumbua Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na Kamishna huyo, Thobias Andengenye kwa madai kuwa wameingia mkataba unaokadiriwa kuwa wa Eoro mikioni 408, sawasawa na shilingi za kitanzania trillion moja., kinyume cha taratibu kwa kuwa mkataba huo haujapitia Bungeni kama zinavyoagizwa na sheria za nchi yetu.
Baada ya kutumbuliwa huko kwa Waziri Kangi Lugola na Kamishna huyo Thobias Andengenye, tukaambiwa kuwa TAKUKURU wanawachunguza watu hao na ikithibitika kuwa waliingia mkataba huo kinyume cha taratibu, basi wataburuzwa mahakamani ili wakajibu mashitaka yao.
Hata hivyo imepita takribani miezi 5 hatujasikia taarifa yoyote ya uchunguzi huo wa TAKUKURU unavyoendelea na ndiyo hiyo Jana tememsikia Rais Magufuli akidai kuwa amemsamehe huyo Kamishna Thobias Andengenye!
Swali tunalojiuliza hivi Rais Magufuli ana uwezo wa kuwasamehe hao kina Kangi Lugola ambao yeye mwenyewe alidai waliingia mkataba ulioliingizia Taifa letu hasara ya shilingi trillion moja?
Je uchunguzi wa TAKUKURU hivi sasa unaendeshwa na Rais Magufuli, kwa kuwaelekeza hao TAKUKURU wa-STOP kuendelea na uchunguzi, pale anapojisikia kufanya hivyo?
Tunajua kuwa kwa tuhuma nzito hiyo ya kuingia mkataba uliolitia hasara Taifa hili la takribani shilingi trillion moja, ni wajibu wetu sisi wananchi kushinikiza kuwa kama kweli watu hao wamelitia hasara Taifa hili kiasi hicho kikubwa sana cha pesa, basi wawajibishwe wakajibu tuhuma hizo mahakamani na siyo kwa Rais wetu kutoa msamaha wa kienyeji.
Kwa kuwa pesa hiyo tuliyoambiwa na Rais wetu kuwa watu hao wamelitia hasara Taifa hili ni pesa za walipa kodi wa nchi hii na.wala siyo pesa za Rais Magufuli.
Tutambue kuwa wapo watanzania wengi ambao wapo magerezani kwa kesi ndogo ndogo za kuiba kuku, iweje kwa hao tulioambiwa na Rais wetu kuwa wamelitia hasara Taifa hili kiasi kikubwa hicho cha pesa zinazokadiriwa kuwa shilingi trillion moja wapewe msamaha kirahisi rahisi hivyo?
Naomba wasomaji wa JF, tudadavue kama ni sahihi kwa Rais wetu kutoa misamaha ya aina hiyo wakati vyombo vya uchunguzi vya ulivyoambiwa vya TAKUKURU vinavyoshughulikia tuhuma hizo kabla havijatoa taarifa yao ya namna uchunguzi wao ulipofikia tamati.