Ukishakuwa mvaa Kobaaz basi tayari wewe ni mpinga kristo
Mizani ya Imani ya mkristo
Bwana Yesu Kristo alieleza mizani na alama za imani kama ifuatavyo:
1. Mkiwa na imani ya punje ya haridali, mtauambia mlima huu, ondoka hapa nenda kule, nao utaondoka; wala halitakuwapo neno lisilowezekana kwenu. (Mathayo17:20; 21:21; Marko 11:22-23, 9:23, Luka 17:6, 12, 13).
2. Bwana akasema: “Kama mngekua na imani kiasi cha chembe ya haridali mngeuambia mkuyu huu, ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.” (Luka 17:7).
3. Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia mkiwa na imani , msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, ngo'ka ukatupwe baharini, litatendeka. na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. (Mathayo 21:21-22)
4. Amin, Amin, nawaambieni, yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwani mimi naenda kwa Baba. (Yohana 14:12-13).
5. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lolote nanyi mtatendewa. (Yohana 15:7).
6. Tena nawaambia, wawili wenu mtakapopatana duniani katika jambo lolote watakalo liomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. (Mathayo 7:3-12)
7. Ombeni nanyi mtapewa.... (Mathayo 7:3-12).
Katika mizani hii ya imani ya Wakristo, tumejua kwamba Mkristo atatambulika kwa alama zilizotajwa hapo juu.
Tena hizi ni alama za imani ndogo sana ya chembe ya haridali.
Lakini kama Mkristo atakuwa na imani kubwa ataweza kuonesha miujiza mikubwa zaidi.
Vilevile Mkristo mwenye imani ni yule ambaye ataweza kuonesha miujiza na hasa sawa na ya Bwana Yesu bali mikubwa zaidi kuliko yake.
Sasa kwanza tutafute miujiza ya Bwana Yesu katika Biblia, tumeona baadhi yao kama ifuatavyo:
1. Kuponya wagonjwa (Mathayo 8:16, 9:22, na 15:21).
2. Kuponya walemavu (Mathayo 8:1-3).
3. Kuponya mabubu. (Mathayo 9:3-7; 12-22).
4. Kuponya mwenye kupooza upande mmoja (kiarusi) (Mathayo 8:5-13. 9:1-7, 12:22).
5. Kumponya mwenye kifafa. (Mathayo 17:14-19).
6. Kuponya mkono wenye ukoma. (Mathayo 12:15).
7. Kuponya mgongo uliopinda (Kibyongo) (Luka 13:10).
8. Kuwafufua wafu. (Mathayo 9:24).
9. Kugeuza maji kuwa pombe. (Yohana 2:1-9).
10. Chakula kidogo kitoshe watu elfu tano. (Mathayo 14:13-21).
11. Kutembea juu ya maji. (Mathayo 14:22-23).
12. Kuzuia tufani . ( Mathayo 8:23-33).
Hapa nimetoa baadhi ya mifano tu ya miujiza ya Bwana Yesu.
Kama Wakristo hamuwezi kuonesha miujiza ya aina hii au alama ya imani yenu sawa na Biblia, basi mambo mawili yanathibitika.
A. Bwana Yesu pia hakuonesha mujiza wowote bali ni hadithi za kutungwa tu zisizo na ukweli ndani yake.
B. Siku hizi Mkristo yeyote hana imani sawa na chembe ya haridali, bali wote mumeshapotea tayari na hamuna alama au dalili yoyote ya imani.
Hali hizi zote mbili ni mbaya sana na za kutisha.
Na dawa yake ni moja tu kwamba muingie katika dini ya Mwenyezi Mungu, ISLAM, baada ya kutambua umoja wa Mungu na Mtume Muhammad s.a.w.bila hivyo mutaendelea kufedheheka siku hadi siku.
TAMBIO:
Ninawapa Wakristo tambio (challenge) kwamba kama munayo imani sawa na chembe ya haridali, mtuoneshe miujiza iliyotajwa hapo juu.
Mkristo mmoja au wawili au mujumuike wote, tunataka kuona miujiza tu ya imani yenu, hata Pope wenu ajitokeze