Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Rais ndiyo Nembo

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Rais ndiyo Nembo

Pesa nyingi ambazo zingetumika kwenye safari za Rais mara kwa mara huko Ulaya,zinafanya mambo mengine ya maendeleo,wateule wa Rais kama mabalozi,waziri wa mambo ya nje n.k watamuwakilisha Rais.
 
Kuna nchi ngapi nje, akizitembelea zote nilini atawatembelea watanzania walio mchagua na angeeleza nini wananchi wakati huu wa uchaguzi.

Kuna mgombea hafahamu hata majina ya vijiji na shida zao.

Kwani huko nje anaenda kukaa huko Mwezi mzima !?.

Na kipindi hichi cha Uchaguzi kipi cha maana alicho waambia Watanzania zaidi ya mambo yale yale ya Mabarabara na Madaraja !?.Uchaguzi wa 2015 aliahidi Milioni 50 kila Kijiji ,hajazitoa mwisho tumebaki na Manyoya tu.
 
Wakati mwingine hushangazwa na mawazo ya kijima katika karne hii, tena ajabu ni kutoka kwa Mtu anadaiwa kuwa na doctorate, hivi ni kweli upeo wa Rais na wasaidizi wake unaweza kuwa finyu kiasi hicho
 
Nafikiri Magufuri alisikia kilio chetu wapenzi wa Chadema tangu enzi za Mze Kikwete tulivyokuwa tunamusakama rais kwamba anakwenda sana nje ya nchi. Sasa Magufuri kaamua kutulia nafikiri hapo tungefurahi zaidi kwasababu hapendi kwenda nje
 
Anajitekenya mbele ya wapiga kura wake tu ila lugha tatizo lugha anafahamu lugha ya kujibu mtihani ila sio ya kuongea
 
Hela zinabaki hapa hapa! Unafikili msafala, na kulala mahoteli ya kifahari raisi na wasaidizi wake fedha kiasi gani zingebaki huko kwa mabeberu? Acha kuwaza mkojo unapoishia mkuu!

Nijibu kwanza tulinganishe Gharama za ziara za hapa Nchini na Nchi za nje.Halafu unapojadiliana na Watu usiweke Maneno machafu yasio na Sababu.
 
Kwani huu Msafara wake wa hapa hapa Nchini na Helkopter juu unajua anatumia kiasi gani Mkuu !?
Gharama za misafara ya magufuli ni balaa, directly and indirectly. Mbali ya hayo magari na helcopter, huku mikoani barabara hufungwa mjini wakati bado anahutubia wilayani umbali wa 100km!
 
Hebu weka hapa kura sahihi za wagombea wote, unajua kwanini haziruhusiwi kuhojiwa? Na sheria hiyo iliwekwa na CCM ambao ndio wanaotangaza matokeo na kuandaa uchaguzi.
CCM inawanachama hai zaid ya 8.7m+, bado wanao fall in love hawa hawana vyama, wengine ni wa vyama vingine nk.

Sasa jiulize mwaka 2005, 2010, 2015 na sasa 2020 unadhani ni kiasi gani cha watanzania wamejiandikisha kupiga kura na kulingana na takwimu za wanachama wa ccm nk nikiasi gani kwa makadirio tu ya kawaida ccm itashinda na huwa inashinda.

Matokeo hayahojiwi kwasababu ya sheria iliyowekwa, na sio kwamba imewekwa na wanaccm bali na wawakilishi wa wananchi kutoka vyama vyote, kama wanaona sheria hii inawazuia kuhoji basi wao waliotunga na kupitisha wanaweza kubadilisha
 
Kuwa Mwenyekiti wa SADC ilikuwa ni zamu by ROTATION wala hakugombea akashinda MSITUPOTOSHE!!!!!!
 
Mkuu haunijui sikujui hivyo hauwezi kunisemea chochote juu ya Maisha yangu ,Great thinker hajadili Watu hapa unatakiwa kujadili Hoja iliyo Mezani.
Nikweli ila umenielewa vibaya, nilikuwa namaanisha umesema sisi watanzania ni masikini basi nikasemea family yako kama miongoni mwa watanzania labda kama sio watanzania nyie.

Sorry...
 
Tatizo lake tunalijua. Hayo mengine ni mbwembwe za kudanganya watanzania wajinga maskini.
 
Kuhusu SADC hakuchaguliwa ni zamu ya nchi tu ilifika, asituone wajinga sana... huenda hata hajui utaratibu wa SADC mwenyekiti anapatiakanaje!
 
"Mtu anasimama analalamika eti sina mahusiano mazuri na Nchi za Ulaya kwani ni lazima mtu kwenda huko Ulaya, hata sasa kuna mkutano wa umoja wa mataifa nimesema siendi nitatuma Mabalozi wetu wakatuwakilishe huko na ndiomaana tukawaweka huko watuwakilishe"

"Ningekuwa sina mahusiano mazuri je ningechaguliwa kuwa mwenyekiti wa SADC, mimi nitabakia hapa hapa kuwapambania Watanzania wanyonge walionipigia kura sio lazima kwenda huko Ulaya " Dr Magufuli CHATO


Wewe ndiye Rais wetu, uliechaguliwa kwa matokeo ya uchaguzi. Tulitegemea utakua unaiwakilisha nchi katika mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na pia Umoja wa Afrika. Matokeo yake uliwatuma wateule na wasaidizi wako. Tunahitaji Rais atakaetuwakilisha kwenye mikutano. Hatukuchagua mwari wa kukaa ndani.
Wwe unataka Raisi atoke Nje ya Nchi ili upige deal lako,Sasa na hatoki ngoo Mabalozi wanatosha!!
 
Kuna tofauti kubwa sana ya Cheo cha Rais na hao wawakailishi unao wahubiri hapa ,katika kutia uzito (msisitizo) wa jambo flani hasa ukizingatia kuwa sisi ni Nchi Masikini sana.
Balozi anamuwakilisha Raisi tuseme inatosha!!
 
Acha abaki na watu waliomchagua, kwenda Ulaya sio jambo msingi kiasi cha kushupaziwa shingo hivyo...!
 
Back
Top Bottom