Tetesi: Rais Dkt Magufuli kufanya ziara nchini China

Inapumbaza na kukufanya usiwakatalie lolote watakalokwambia.
Kumbuka walimpa Kikwete U professa wa Heshima, matokeo yake leo hii Kariakoo kuna wachina wanarusha Mpesa Tigopesa na Kuchoma mahindi.
Tafakari
Si ndiyo vizuri na Kariakoo yetu sasa ina sura ya kimataifa badala ya zamani ya kizaramo. Na wazungu wanakaribishwa Kariakoo kuchoma mahindi na kuuza mitumba.
 
Awaombee mapunda waachiwe huru.... huku bongo bidhaa zimeadimika
 
Akitoka China apitie na Japan. Tunataka viwanda nchi zilishatuahidi kuleta viwanda vyao hapa katika awamu ya nne. JK awe ni kati ya watu atakaoenda nao, ni hazina ya taifa.
 
Kwanza tu review ile mikataba ya riz1 maana ilisainiwa haraka haraka hata bila kujadiliwa na kujua haswa ni ya nini! Mingine hata haieleweki hadi sasa! Wanasema tu utamandu na utalii! Mbon hatuelewi?
 


Hoja kwamba eti "mikataba yote alisaini JK" ni ya uongo mkubwa. JK hakusaini mikataba yote yote ile. Isipokuwa ni kweli mikataba mingi ilisainiwa chini ya uongozi wake. Kuweni makini na taarifa zenu. Humu ndani ya JF siyo wote mambumbumbu...
 
Mbona mapema mno kuanza kutembeza bakuli?
 
Hoja kwamba eti "mikataba yote alisaini JK" ni ya uongo mkubwa. JK hakusaini mikataba yote yote ile. Isipokuwa ni kweli mikataba mingi ilisainiwa chini ya uongozi wake. Kuweni makini na taarifa zenu. Humu ndani ya JF siyo wote mambumbumbu...

Sasa unakubali nini na unakataa nini?? Ok ila inafahamika na ilitangazwa kua jamaa alisaini mikataba 17 at per na rais wa China alivyokuja hapa Tz , tunajua kwa nini ilimbidi asaini hiyo mikataba yote bila kubisha wala kushauriana na wanasheria wa wizara husika.
 
Sema tena!
 
Mkuu wa Kaya hasije kua kama mzee wa msoga, kupewa tu degree ya heshima kauza maliasili zote kwa mchina
 
Hivi mbona Marekani na Ulaya haikufungua vikwazo vya Zimbabwe baada ya Mugabe kufungamana na China? Mbona China hakumwaga hayo mapesa kuokoa uchumi wa Zimbabwe? Sio kosa lenu.... Lishe duni imewatafuna akili zenu kiasi cha kushindwa kufikiri.

Itabidi ujitahidi kusoma International Relations na Geo-politics kama njia mojawapo ya kupanua uelewa wa issues mbalimbali
 
Kama ni kweli. Basi JPM ana akili sana
Nakuunga mkono. Nadhani ana washauri wazuri. Hizi nchi za Ulaya zinakwenda kufilisika na kufa wakati mashariki inaibuka juu. ni karne ya mashariki hii ijayo na vizuri kuweka misingi imara. Ingawaje JK pia aliendeleza uhusiano na China ila alikuwa na mioyo miwili. Anapenda kujiona zaidi kuwa ni mzungu. Hata utaona namna alivyomlaki Obama na rais wa China. Obama alimpa heshima kubwa wakati Wamarekani hawana msaada wowote wa maendeleo. Kazi yao kubwa ni majungu tu na mambo ya kuuwana, sijui terrorism na kupambana na mbu!
Akitoka huko aende Vietnam, nchi inayokuja juu sana na yenye mengi ya kuiga. Kisha aende Uturuki. Huko iatuwa ndege wawili kwa jiwe moja. Ziara yake Uturuki utawapoza moyo wazungu kuwa hailekei Mashariki tuu, lakini pia Uturuki inapenda sana kujipanua ufukwe wa Mashariki ya Afrika. Labda Iran pia itakuwa vizuri kuzatiti uhusiano. Wanaweza kutusaidia kujenga mabwawa ya kuzalisha umeme dams, na pia kujenga mtambo wa kusafishia mafuta huko Tanga. Wapange ziara hii wakiwa na akili za mwaka 2050 wakati idadi ya watu wa Tanzania itafikia milioni 100.
 
Marekani na Yuropa wakisikia hivi, lazima warejeshe hela walizosusa kuzitoa.

Hawatakubali kuona mchina anapata influence kubwa namna hii ukanda huu.
Na ukitaka kupata influence kwa masikini, we mwaga mihela, utapendwajeee
Asijione kwamba anamkomoa mzungu kwa yeye kwenda china, hawa wachina si watu kabisa. Namkubali mzungu mara 200% kuliko mchina kwa .002%.
Asilete sifa za kisukuma ktk kuendesha nchi
 

Hujui unachosema
 
CCM wamebadilishia gia angani awamu hii bakuli haliendi tena kwa wazungu linaenda kwa wachina, sijui watatuambia ni msaada au zawadi?! maajabu hayaishi nchi hii.
 

Naunga mkono hoja yako ingawa sikubaliani sana na Uturuki. Kwa maoni yangu akitoka China aende Russia halafu Vietnam na pia Singapore kuhusu masuala ya maritime. Kumbuka Singapore ndkio wenyewe kwa masuala ya maritime. Halafu historia ya Singapore na Tanzania inafanana. Walipata uhuru mwaka 1961 kama sisi. Tangu wakati huo wanatawaliwa na chama kimoja kama sisi (TANU/CCM). Hivi sasa Singapore uchumi wao ni wa first world.
 
Magu atafanya ziara ya nje hivi karibuni, waziri wa mambo ya nje kathibitisha hivyo ila hajasema ni lini na wapi. Ziara ya Rais haiwekwi wazi sijaelewa ni kwa nini au ndo mambo ya usalama! Hao walio ktk riski ya usalama ziara zao zinatangazwa miezi 3 hadi 6 kabla. Yaani sisi kila kitu ni tukio la kushitukiza hatuna ratiba ya mipango yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…