Nakuunga mkono. Nadhani ana washauri wazuri. Hizi nchi za Ulaya zinakwenda kufilisika na kufa wakati mashariki inaibuka juu. ni karne ya mashariki hii ijayo na vizuri kuweka misingi imara. Ingawaje JK pia aliendeleza uhusiano na China ila alikuwa na mioyo miwili. Anapenda kujiona zaidi kuwa ni mzungu. Hata utaona namna alivyomlaki Obama na rais wa China. Obama alimpa heshima kubwa wakati Wamarekani hawana msaada wowote wa maendeleo. Kazi yao kubwa ni majungu tu na mambo ya kuuwana, sijui terrorism na kupambana na mbu!
Akitoka huko aende Vietnam, nchi inayokuja juu sana na yenye mengi ya kuiga. Kisha aende Uturuki. Huko iatuwa ndege wawili kwa jiwe moja. Ziara yake Uturuki utawapoza moyo wazungu kuwa hailekei Mashariki tuu, lakini pia Uturuki inapenda sana kujipanua ufukwe wa Mashariki ya Afrika. Labda Iran pia itakuwa vizuri kuzatiti uhusiano. Wanaweza kutusaidia kujenga mabwawa ya kuzalisha umeme dams, na pia kujenga mtambo wa kusafishia mafuta huko Tanga. Wapange ziara hii wakiwa na akili za mwaka 2050 wakati idadi ya watu wa Tanzania itafikia milioni 100.