Rais Dkt. Mwinyi amteua Maalim Seif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Rais Dkt. Mwinyi amteua Maalim Seif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Hivi katiba ya Zanzibar kuhusu makamo wa rais nae anatumbuliwa??
 
Wiki kama Tatu hivi nikiwa katika 'Kijiwe' changu Kimoja nakumbuka niliwaambia wana Kijiwe Wenzangu kuwa kama kuna Mwanasiasa hapa nchini Tanzania na tena atokae 'Zanzibar Isles' ambaye wasipoteze muda Wao katika Kumuamini na hata Kumsikiliza kwakuwa ni 'Mnafiki' Mwandamizi ni Maalim Seif Sharif Hamad na kuwaambia kuwa akiteuliwa hiki Cheo hatokikataa ng'o kwani nae pia ana 'Njaa' na hatimaye Usiku huu imekuwa.
Hivi ninyi mlitaka akatae wakati ukweli ndio alishindwa na nafasi aliyostahili ndio hiyo. Maalim Seif sio mnafiki ila ninyi ndio wanafiki.
 
Kazi kwa CHADEMA sasa; ACT inasonga mbele kisiasa wakati CHADEMA bado imejifungia chumbani.

Ingawa najua kuwa huu mwafaka ndiyo huwa lengo kuu la Sharif Hamad ili awena madaraka, akishyakosa ndipo anapoanzan kulalamika. Sasa hivi swala la "haki za binadamu" au "kuuwawa kwa raia wasikuwa na hatia" huo Zanzibar hutalisikia tena.
Kusonga mbele kisiasa kwa kulamba matapishi yako....
 
aloo! ya wana siasa waachieni wanasiasa, watu walikufa kisa wanasiasa na siasa, leo hii ndo haooo wameungana kula bata kwa pamoja, nadhani siku zingine hakuna atakae kubali kufa au kudhurika kisa mwana siasa au siasa, bila shaka hili ni fundisho na litakuwa ni fundisho tosha kwa watu wote.
 
CCM itatawala nchi hii mpaka siku jeshi likisema basi!
aloo! ya wana siasa waachieni wanasiasa, watu walikufa kisa wanasiasa na siasa, leo hii ndo haooo wameungana kula bata kwa pamoja, nadhani siku zingine hakuna atakae kubali kufa au kudhurika kisa mwana siasa au siasa, bila shaka hili ni fundisho na litakuwa ni fundisho tosha kwa watu wote.
 
Hivi ninyi mlitaka akatae wakati ukweli ndio alishindwa na nafasi aliyostahili ndio hiyo. Maalim Seif sio mnafiki ila ninyi ndio wanafiki.

Ni kweli, Maalim Seif anajua kulinda tumbo lake. Muafaka ili Seif apate ulaji kwa umwagikaji wa damu za wananchi!
 
Hivi na wewe umekaa ukawaza na kujiaminisha kweli maalim Seif alishinda. Mambo mengine mnajipa presha bure tu.

Maalim Seif ashinde halafu akubali kuwa makamu kirahisi vile.

Kumbuka 2015 uchaguzi ulipofutwa alikataa hata kushiriki uchaguzi wa marudio kwani ule wa kwanza alishinda.

Hapo sasa hivi mtamuonea tu, ndio nafasi yake anastahili na yupo happy.
 
Tanzania ni kisiwa cha amani na upendo, waliotaka kutufarakanisha wamefarakana wenyewe
Lala unono Jumbe

Ni hivi, ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Seif akapiganie tumbo maana umri umemtupa.
 
Tangu 1995 tunasusia kimebadilika nini?
Tuache siasa za chuki tusonge mbele.

Isitoshe miaka yote hiyo wazanzibar tunasusia nyinyi watanganyika munaenda bungeni hata hamjali kuhusu sisi leo kibao kimewageuka ndio mnajifanya wapinzani kweli.

Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Hivi na wewe umekaa ukawaza na kujiaminisha kweli maalim Seif alishinda. Mambo mengine mnajipa presha bure tu.

Maalim Seif ashinde halafu akubali kuwa makamu kirahisi vile...
Hiyo 2015 alipewa huo ushindi wake?
 
Hata kundamana tulikataa. Maalim na miaka yake 77 nilimwona akindamana kabla ya kukamatwa. Katika watu wachache waliondamana kupinga matokeo ni Maalim na akina Jussa.
Tangu 1995 tunasusia kimebadilika nini?
Tuache siasa za chuki tusonge mbele.

Isitoshe miaka yote hiyo wazanzibar tunasusia nyinyi watanganyika munaenda bungeni hata hamjali kuhusu sisi leo kibao kimewageuka ndio mnajifanya wapinzani kweli.

Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Kusonga mbele kisiasa kwa kulamba matapishi yako....
Kamati kuu ya ACT imeshakaa na kuamua! Kwenye siasa kuna ushauri kuwa mwenzi akikushinda, shirikiana naye ili upate sehemu ya madaraka yake! Ukizila, yeye ataendelea na madaraka yote na hutapata hata chembe yake.
 
Wazanzibari msirudie tena kupiga polisi mawe
😄😄😄
Ushauri murua kabisa. Akina Jusa naamini wamepona.

Tunasubiri hawa wakimbizi wa kujitakia warudi kwani nchi ni shwari na wabunge wao 20, mmoja toka jimboni na 19 viti maalumu wapo bungeni. Kwa hiyo warudi tu tujenge nchi wala hakuna tishio lolote kwani wabunge wamama hawa wanatesa tu Dodoma bila hofu.
 
Ama kweli unafiki ni KIPAJI. ACT Wazalendo mmekusanya ushahidi na kupeleka katika taasisi za Kimataifa ICC, UNHRC na kwingineko kuwashtaki madhalimu wa maccm. Hata kabla hamjajibiwa MMEKURUPUKA kudandia madaraka! Chama cha wasaliti na waroho wa madaraka. Haya sasa jipongezeni kwa usaliti wenu. Zitto
View attachment 1643490
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Maalim Seif Shariff Hamad, kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar kuanzia leo Disemba 06, 2020.

=====

Taarifa kwa vyombo vya Habari

Kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 9(3) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984,kinachosema kwamba “Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa na Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia”.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 6 Disemba,2020
View attachment 1643495
 
Hujui upizani wa Wazanzibar we
Nyinyi mnajua upizani ni kama mchezo wa kuvuta kamba unavuta tuuu.
Mabadiliko yatakayo TOKEA znz hamtaamini macho na masikio yenu . Hizi ni karata zishachezwa tulieniiiiiii.?
Hahahaaa mkuu naamini na ww ni mmoja kati ya wale walioaminishwa mwaka 2015 kua Maalim Seif ataapishwa uraisi na hatimae katimkia ACT
 
Ama kweli unafiki ni KIPAJI. ACT Wazalendo mmekusanya ushahidi na kupeleka katika taasisi za Kimataifa ICC, UNHRC na kwingineko kuwashtaki madhalimu wa maccm. Hata kabla hamjajibiwa MMEKURUPUKA kudandia madaraka! Chama cha wasaliti na waroho wa madaraka. Haya sasa jipongezeni kwa usaliti wenu. Zitto
Kwani kuna chama hakitaki madaraka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom