Rais Hussein Mwinyi kawa waziri wa Naibu waziri enzi ya Mkapa
Waziri wa Muungano enzi ya JK
Waziri wa Ulinzi enzi ya JK
Waziri wa Afya enzi ya JK
Waziri wa Ulinzi tena enzi ya JPM

Kwa maelezo ya JPM wakati ameteuliwa na Mkutano Mkuu CCM 2020, alisema chaguo lake la mgombea mwenza alikuwa Dr. Hussein Mwinyi, isipokuwa "akashauriwa" aende na SSH.
Kwa maelezo yale, kama hili la March 17, 2021 lingetokea basi Hussein Mwinyi angeapishwa tar 19 March na sasa angekuwa mkazi wa magogoni au chamwino.

Hata hivyo kwa kuwa SSH tunae na anakusudia kuliungisha mpaka 2030, kule Zenji Dr. Mwinyi nae tenure yake ya pili itakuwa inakoma na kwa uzoefu wa miaka 10 ya urais wa Zbar, he can make a very good and experienced president kuliko wote waliowahi kutokea.

Tuombene heri, ila yale mafigisu, zengwe na uchawi yanayosewa yasikatishe tamaa watu wenye uwezo mzuri na upeo mkubwa wa uongozi ili waweze kutuongoza na kukusanya kodi zetu na kuongeza chachu ya shughuli za kimaendeleo.

Ijumaa kareem
 
China hawana hilo lakini wana Rais wa wengi
Rais wa China sio wa wengi anatokana na chama cha kikomunisti cha China chenye wanachama milioni 95 tu wakati China ina watu bilioni 1.3. Huwezi kuwa na Rais wa wengi bila sanduku la kura linalohusisha watu wote angalau wenye kuanzia miaka 18 na kusimamiwa na tume huru ya uchaguzi.
 
Kama unamkubali sana waambie chama chako akimaliza kutawala miaka 10 Zanzibar aje kutawala miaka 10 Tanzania.
 
Nawashangaa hoja zinazoletwa humu ambazo zinakuwa very shallow and short sightedness indeed. Qualifications za Urais sio kushusha bei ya kuunga umeme tu. We have to be realistic in things with impact in our economy or economy of TANESCO. Tutayauwa haya mashirika ya umma. Vitu vingine vifanyike kwa uhalisia sio kisiasa hata kidogo. Kweli tulilishwa matango pori mengi na mwendazake tokea ujenzi, mnunuzi, Covid, na hata ustawi wa mashirika yetu. Kila kitu kilikuwa siasa zenye mrengo wa kujinufaisha kisiasa na wala sio uhalisia wa kiuchumi it was very wrong.
 
Tunasubiri siku atakayoshuka malaika kuja kutawala. Na hata hivyo tutaendelea kulalamika tu.
 
Umenena vyema sana
 
Who care about covid now? Au mwenzetu umejifungia?

Unajua kwenye utawala wa JPM TANESCO wamefungia umeme watu wangapi?unajua TANESCO since then wanakusanya shs ngapi kwa mwezi?
 
Tunasubiri siku atakayoshuka malaika kuja kutawala. Na hata hivyo tutaendelea kulalamika tu.

Ndio kawaida yetu sisi binadamu katika dini yetu sisi waislam inaonesha pia watu walikuwa wakiwakataa mitume na manabii kwa style hii hii
 
Ulishawahi kuona Rais wa China anahangaika kujaza tumbo lake?
 
Asante mkuu....
Na wakumbuke pia kuwa wakati lile dege la kijeshi la Qatar linaingia nchini kinyemela na 'kuiba' wanyama hai 103 (?) na nyara nyingine za serikali, huyo mtu wao ndiye alikuwa waziri wa ulinzi!
Na hakuwajibika kwa namna yoyote.....
 
Kabisa kabisaaaa

Ila ndo haiwezekani tena
 
Ataachaje kufanya hivyo angali nasikia sikia walipewa Bilionee za koviifidii
 
Ulishawahi kuona Rais wa China anahangaika kujaza tumbo lake?
Nchi nyingi kusini mwa jangwa na sahara, ruksa kujimegea kwa kadri ya urefu wa kamba, ila tahadhari imetolewa "wasivimbiwe". Bila shaka ndani ya muda mfupi watu wamejimegea "mapande makubwa ya minofu"
 
Nchi nyingi kusini mwa jangwa na sahara, ruksa kujimegea kwa kadri ya urefu wa kamba, ila tahadhari imetolewa "wasivimbiwe". Bila shaka ndani ya muda mfupi watu wamejimegea "mapande makubwa ya minofu"
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mapato ya bara si ndio yanapelekwa uko Mwanakwerekwe kuleta maendeleo kwahyo zenji lazima kuwe Kama Dubai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…