Imemshinda Zanzibar yenye wakaazi Mil moja atawezaje Jamhuri ya Muungano , tusihadaike na majina ya watoto wa viongizi wengine hawana uwezo wala maono ya uongozi
 
Naomba nikili Mimi ni mfuasi sanaaa wa utendaji kazi wa Rais wa Zanzibar hata kabla hajawa Rais wa Zanzibar tangu akiwa mbunge wa huko Pwani. Kwa maana ya Bara mpaka anakuwa Waziri hakika nilianza kumfatilia kitambo,

Jambo moja kubwa liliromshinda,kuliratibu vizuri akiwa Waziri wa Ulinzi ni kukomesha jeshi letu wa wananchi kuondoa ajira za undugulization hili lilimshinda kwa sababu nyingi ipo siku tutazitaja maana zipo wazi na tunaishi nazo kila uchwao.

Baada ya ndugu Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar Bado nimeendelea Tena nimezidisha mara tele kumfuatilia ninayoyaona ni majonzi. Rais Mwinyi amekuwa mwingi wa majonzi dhidi yale anayoyatamani ayafanye ila watumishi walio chini yake wanamkwamisha sana kwa sababu ya nature of Zanzibar they are very slow in decision making even hata wakiamua ni wazito kutenda.

Mwinyi anatamani Sasa apate majembe kutoka Bara kama akina Juma Aweso sidhani kama kuna kijana anayekimbia huku kama yeye,waende Zenji wamsadie kuwaamsha wazanzibar hakika lakini hata Rais Mwinyi anatakiwa kutambua ya kuwa exposure aliyonayo ni kwa sababu ya kufanya kazi Bara na kutumika ndani na nje ya Tanganyika.

Kimsingi ukimsikia Mwinyi utaona kabsa anatamani walau achukue wabara kadhaa awapeleke zenji wakawakimbize mchaka mchaka watumishi wa kule Ili waamke.

Je sheria inamruhusu? Nahisi kama anabanwa na vifungu hivyo vya Muungano Serikali ya Jamhuri ni chuo cha kupika wazenji wakae sawa ila walioko huko wengi wao huwaza rojo hata muda kunywa chai.

Mwinyi alifaa kuiongoza Bara jamhuri walah angekata kiu yake ya kutukimbiza mchakamchaka na Mwinyi angetawala baada ya Magufuli hasingediriki kuondoa mchaka mchaka kama ulivyoondolewa na Mama yetu akidhani ni tiba kumbe ni TOBO leo anajua anatamani arudishe kumbe too late watu washampiga vya kutosha wanasubiri afurukute wasepe maana mafao washajilipa.
 
Hii ni mada chonganishi! Wala haina heshima kwa viongozi wetu wakuu wa JMT na SMZ. 🙏🙏
 
Kipindi cha nyerere kulikuwa na maslahi gani???
 
Point 100%
 
Wewe umeona wapi? Ulipie vitu vyote hivyo halafu mwisho wa siku vinakuwa mali yao? Yaani ni malipo kandamizi.
Elfu 27 inatosha kabisa kwa sababu hawawezi kutuuzia vifaa halafu viwe vyao. After all tunakuja kulipia umeme kwa miaka 100 vijukuu na vitukuu. Ni kama vile kampuni za simu zinagharamika kutengeneza line za simu (chip) lengo likiwa ni kupata wateja lukuki bila kujali gharama halisi, unanunua line kwa 1,000, siyo gharama halisi, wangeweza kutuuzia kwa 20,000 lkn wanajua wasingekuza client base, watakuja kufaidi pale unapoweka bando, unapopiga simu, sms, vifurushi mbalimbali, hapo hatujazungumzia makato ya mobile money, internet banking etc.
Utafikiri hatuna watu wa uchumi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…