Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mbadilishe Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu hatoshi

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mbadilishe Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu hatoshi

Pole sana mkuu umetoa point ya msingi sana suala la afya ni lakuzingatia sana kma taifa
 
Hakuna hoja ya msingi hapo, Waziri hawezi ingilia Balaza ambalo lipo kisheria na pia Baraza linajiendesha kisheria na sio kiholela.

Mwisho hao watu kama wako smart na hawajatendewa Haki waende Mahakamani sio kusingizia Waziri.
Tatizo lako wewe huwa unajibu kiholela. Tumia akili yako vizuri
 
Acha kumsagia mwenzako kunguni.
Umri wa Mtanzania kuishi umeongezeka.
Hiyo ni indicator mojawapo inayoonesha kuwa anatosha...
 
Nyie wadogo hamna shule tu. Mnataka wanasiasa wawabebe. Unajua TCU ilianzaje? Baada ya utitiri huu huu wa vyuo, na bado inashindwa kusimamia. Mabaraza yaendelee kukaza uzi.
 
Mhe Rais kwanza nikupe pole na heshima yako na nikupongeze sana Mama kwa uwajibikaji wako katika kulisaidia Taifa hili kwa kuliponya kutoka katika mazingira magumu miaka 8 iliyopita. Hakika tunaweza kusema ya kwamba mabadiliko ni makubwa sana katika sekta zote ispokua baadhi ya Watendaji wako ndio wanaokuharibia na kuendelea kukuchelewesha kufika kule mbali unakotazama.
Bila hiyana wala unafki kwakweli kongole Mama![emoji122][emoji122]

Mhe Rais tunafahamu kwamba falsafa yako kubwa katika utendaji ni kuwaacha watendaji wako wafanye kazi wenyewe kwa kujisimamia bila pressure yeyote ya mamlaka tena kwa ubinifu mkubwa. Hii ndio misingi ya kweli ya kiutawala.

KWANINI WAZIRI UMMY ABADILISHWE?

Mhe Rais, nikiwa kama Mtanzania Mzalendo,Mdau katika masuala ya Afya na kada/kiongozi mtiifu katika chama cha Mapinduzi, sipendi tuharibikiwe nitaelezea mambo kadhaa muhimu ambayo pengine Mhe Waziri hakuambii ukweli au watendaji walio chini yake hawamwambii ukweli kwa vile yeye siyo mwanataaluma katika sekta ya Afya.

KUSHINDWA KUSIMAMIA NA KUTATUA KERO NA MALALAMIKO YA MADAKTARI TARAJALI(INTERNS) KUTOTENDEWA HAKI NA BARAZA LA MADAKTARI TANGANYIKA(MCT).

Mhe Rais wangu, ikumbukwe kua Madaktari tarajali waliwahi kukuandikia Barua ya wazi kwamba hawatendewi haki na Baraza la Madaktari Tanganyika(MCT) wakilalamikia mambo kadha wakadha ambayo nitayabainisha hapa.Lakini baada ya Barua hiyo Mhe Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alimtuma Naibu waziri wake Dr Godwin Moleli ambaye alikutana na Watarajali hao na kisha kueleza kero na changamoto zao. Baadaye Mhe Waziri Ummy Mwalimu alitoa taarifa kuunda tume ya kiuchunguzi kushughulikia changamoto hizo, lakini cha ajabu mpaka sasa hakuna mrejesho na walalamikiwa wanaendelea na kile kile kinacholalamikiwa.

Mhe Rais, katika mambo yanayolalamikiwa na watarajali hawa ni kama ifuatavyo;

(i)Kunzishwa kwa mitihani ya Pre-intetnships ambayo haieleweki msingi wake ingawa baraza lilidai kuwapima watarajali hao kutokana na kutilia shaka vyuo vikuu waliotoka. Lakini swali la kujiuliza ni kwamba, TCU kikiwa kama chombo cha kupima ubora wa vyuo vikuu kina kazi gani? Huyu Mwanafunzi aliyesoma miaka yote 5 chuoni kisha akafuzu mafunzo yote ya nadharia na vitendo hospitalini miaka yote anapimwa kitu gani hasa? Unampimaje kwa maswali 150 ya nadharia ya kuchagua masaa peke yake masaa 3 ambapo kwa vitendo hujui ataenda kufanya kitu gani?
Mhe Rais, Kazi ya baraza ni kupima ubora wa mwanafunzi kabla ya kuanza mafunzo au mpaka amalize mafunzo ya hospitalini kwanza?
Ni taifa gani wana mfuno huu wa Pre and post Internship ikiwa hata mwongozo wa WHO hausemi hivyo?
Kwanini tusihisi kwamba hii ni janja janja ya kujikusanyia pesa wanazolipa watarajali hawa kabla ya kujisajili kufanya mitihani hiyo bila sababu za msingi?
Kusu hili Mhe Waziri hajui kabisa chochote Mhe Rais.

(ii)Watarajali kupewa mitihani ambayo haikutathminiwa wala kufanyiwa utafiti matokeo yake hali hii ilipelekea zaidi ya nusu kufanya vibaya kwenye mitihani hii.
Kulikua na kigezo cha mtarajali kwenda kufanya mafunzo mpaka afaulu mtihani huo kwanza, lakini mhe Waziri alipoona kuna malalamiko makubwa na hali ni mbaya sana mahospitalini hakuna madaktari wa kutosha ampapo kimsingi hawa watarajali ndio nguvu kazi kubwa kwenye mahospitali yote nchini, akaondoa zuio hilo la kwenda mafunzoni hadi mtarajali afaulu mtihani huo, ikawa sasa wafaulu wasifaulu wataenda mafunzoni tu na mtihani lazima ufanyike. Mtu unajiuliza, ni ipi sababu ya kuwapima kabla ya ilikua ikiwa wote wanaofeli na wanaofaulu wanaenda mafunzoni? Mantiki ya kipimo hapa ni ipi? Kwanini tusichukulie kua mitihani hiyo ninkitega uchumi tu cha baraza?

Kwenye hili Mhe Waziri Ummy alisema aneunda tume ya kuchunguza Malalamiko ya Watarajali hao na kutoa majibu ndani ya muda mfupi, lakini Mhe Rais Mpaka naandika hivi sasa ni zaidi ya Mwezi mmoja tume hiyo haijatoa mrejesho wala taarifa yeyote na Mhe Waziri yupo kimya.
Mhe Rais, Mpaka sasa Baraza hili ambalo linalalamikiwa na limeundiwa tume kuchunguzwa linaandaa mitihani mingine ya Preinternship, Watarajali hawa wanajiuliza, kuna usalama na uhalali kiasi gani kwenye mitihani hiyo?
Ni sahihi Baraza kuendelea na uandaaji wa mitihani wakati wanachunguzwa?

(iii)Kwanini ni taaluma ya Udaktari kuna mitihani miwili ya Pre and Post internships tofauti na taaluma ziingine ambazo watarajali huenda kufanya mafunzo ya vitendo kwanza chini ya Wasimamizi ambao ni wanataaluma waandamizi kisha baadaye mitihani ya kumaliza hufuata na kupatiwa leseni zao?
Kama hoja ilikua ni kutilia shaka uwezo wa vyuo vikuu kuandaa wataalam, kada zingine wamesomea vyuo gani? Kwanini baraza la madaktari Tanganyika wanafanya kitu ambacho yumkini hata wao hawajui maana yake?

(iv)Kuhusu watarataji waliofeli mitihani yao ambao kwa rekodi ya mtihani uliopita nibzaidi ya nusu ya waliofanya watahiniwa, wao kuendelea kukaa mtaani huku hawana leseni hadi mwaka mzima wakisubiri hadi wengine wamalize ndio waje wafanye mitihani pamoja, tunajiuliza huu ni utaratibu wa wapi kwa vijana hawa ambao tayari wana mikopo ya HESLEB ina mkataba baada ya muda flani kutakiwa kurejesha pesa walizokopa? kama wataendele kukaa mtaani maana yake hawana leseni hawawezi kufanya yeyote ile, siyo hasara kwa serikali iliyowakopesha?

USHAURI KWAKO MHE RAIS
Ikiwa vijana hawa waliandika barua ya wazi kwako Mhe Rais, Mhe Waziri akawahadaa kwa nia ya kuwapooza kwa kuunda tume ambayo mpaka sasa haijatoa mrejesho wala ripoti yeyote huku walalamikiwa wakiendelea na yale ambayo yalilalamikiwa.Kabla vijana hawa hawajakuangukia kwa njia ambayo pengine leo watahitaji tena kukutana nawe ana kwa ana, Mhe Rais wangu chukua hatua ya kumbadilisha Mhe Waziri kwenda wizara nyingine au uamuzi wowote utakaoona unafaa kwa mamlaka yako.
Hii inatafsiriwa ya kwamba amepuuza malalamiko ya wataalam hawa ambao taifa hili linawahitaji kwa kiasi kikubwa maana wamesomeshwa kwa gharama kubwa sana.
Mbona Wizara ya katiba na sheria walichukua hatua haraka baada ya Shule ya sheria(School of law) kulalamikiwa kutotenda haki kwa watahiniwa wa kada hiyo? Wizara ya Afya kuna nini?

Yangu ni hayo Mhe Rais.
Kazi endelee kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waache kupenda mteremko....

Hiyo mitihani ni kwa ajili ya kuwapima uwezo wao kwa kuwa :

1)Log Books za kipindi cha internship wako wanaozifoji....wako wanaobebwa nje ya taaluma na kupewa GRADES wasizostahili.....

2)Matokeo pekee ya chuo(MD results) hayatoshi kwani nako kuna "ufukunyuku" mwingi....

Niishie hapa kwa sasa...

#Nchi Kwanza[emoji120]
 
1. pole lakini, ujue tu kuwa taaluma ya udactari wa Binadam ni tofauti kabisa na taaluma nyingine(no try and error). Namaanisha mtu hawezi kupita tu kwani ataishia kufanya majaribio kwa miili ya Binadamu
2. hata hivyo nafikiri ipo haja ya kupitia ubora wa vyuo vyetu hasa kwa kozi sensitive kama hiyo ya Udactari wa Binadamu pengine kuja na mitihani ya mwaka ambayo itafanywa na vyuo vyote ili kuepusha ubabaishaji
3. Mbona watu wa sheria (majaji wanafunzi) wanatahiniwa na kufeli kwa 80% na inaeleweka; Naona wizara ya Afya tayari imeona gap (udhaifu mahala) sasa inajaribu kuona namna nzuri ya kuchuja kuepusha kupitisha watu wa kufanya majaribio kwenye miili ya binadamu. Ungetoa ushauri wa namna nzuri zaidi ya kuwapima ingependeza..
Atalielewa hili yule mwenye akili pekee...[emoji2956][emoji7][emoji109]
 
Nchi nyingi Duniani hakuna Dactari anayeingia moja kwa moja bila ya mtihani wa leseni ... USA wana USMLE ambapo wanafanya hadi oral , India wana FMGE na kadhalika kwa ufupi ni lazima kuwe na lesence exam na hiyo ipo maeneo mengi duniani .. haya malalamiko ya madactari taraji hayana maana vijana wasome .. ila tu kuwe na standard ya mtihani isiwe kama ile ya vyuoni
Comment ya DHAHABU [emoji2956][emoji7][emoji109]
 
Unaelewa kinscholalamikiwa hapo? Watu wanalilia uwepo wa Pre na post internship na Standards zake. Duniani kote hata mwongozo wa WHO upo wazi, ni mtihani wa leseni peke yake ndio unaofanyika. Hivyo mitihani ya MCT ni ya nini?
Kwani WHO haigusi maslahi ya afya nchini Marekani ?!!!

Mbona wao wana USMLE?!!

WHO wamelipinga hilo ?!!![emoji15][emoji15]
 
Ni nchi gani kuna Pre na post internship? Tofautisha mtihani w practical lisence na hii mitihani.
Sasa lengo la Pre-Post internship exams si kwa ajili ya kupewa PRACTICING LISENCE na MCT ?!!!

Unaongea nini wewe jamaa?!!![emoji15][emoji15]
 
Unaelewa Muuguzi hua ana kazi gani? Wao wana pre na post internship?
Law school wana Pre lawa school?
MCT wanasimamia mambo ya LAW SCHOOLS?!! [emoji15]

Unataka bodi ya madaktari inakili taratibu za bodi ya mawakili ?!!
Bodi ya wahasibu ?!!!

Wewe jamaa unaongea hayo kwa hisia na mbango ?!!! [emoji15][emoji1787][emoji1787]
 
Ukweli kuna haja ya kuwachuja sana hao madactari wa Binadamu na ukifuatilia vizuri wapo wachache ukikutana naye huku mtaani, hata kwa mtu asiye na taaluma anapata wasiwasi kuwa kuna kitu hakipo sawa. Ni bora kabisa tuwe nao wachache wanaoijua kazi yao vizuri na umuhimu wake kwa jamii namaanisha waasio ifanisha taaluma yao na mtu mf: anayesomea biashara
Swadaktaaa...

Hakikaaaa [emoji2956][emoji7]
 
Endelea kujidanganya. Tanzania kuna total collapse of the system kiasi ambacho hata uki-fix sehemu moja unakuwa hujafanya kitu. Huyo ''msikivu'' wako naye anatakiwa kuondolewa!
Kuondolewa kimapinduzi ?!!

Kwa faida ya akina nani hao ?!!!
 
Sasa lengo la Pre-Post internship exams si kwa ajili ya kupewa PRACTICING LISENCE na MCT ?!!!

Unaongea nini wewe jamaa?!!![emoji15][emoji15]
Yaani wewe ni bumunda kweli. Hivi preintetnship mantiki yake ni ipi hada? Kinachofanywa kwenye Logbooks hua ni kitu gani au kinasaidia nini?
 
Maoni mazuri sanaa
Nchi nyingi Duniani hakuna Dactari anayeingia moja kwa moja bila ya mtihani wa leseni ... USA wana USMLE ambapo wanafanya hadi oral , India wana FMGE na kadhalika kwa ufupi ni lazima kuwe na lesence exam na hiyo ipo maeneo mengi duniani .. haya malalamiko ya madactari taraji hayana maana vijana wasome .. ila tu kuwe na standard ya mtihani isiwe
 
Back
Top Bottom