Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mbadilishe Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu hatoshi

Yaani wewe ni bumunda kweli. Hivi preintetnship mantiki yake ni ipi hada? Kinachofanywa kwenye Logbooks hua ni kitu gani au kinasaidia nini?
Pre-intership imepangwa na MCT kuhakiki ubora wa MD aliyemaliza shahada...hapo kuna mengi wanapata na kugundua.....(yako mapendekezo ya maboresho ya elimu yetu yanatoka hapo).

Katika Pre-Internship ni kumwezesha mtahiniwa kufuzu kupewa (PROVISIONAL REGISTRATION)....ili aende akafanye INTERNSHIP(mafunzo ya utarajali).

Post-Internship ni kumtahini daktari aliyekwisha kupata cheti chake cha kumaliza INTERNSHIP(mafunzo ya utarajali katika hospitali husika) kuweza kupewa LESENI na MCT(full registration)....ili akaanze kutibu...

Sasa wewe zwazwa unataka bodi ya madaktari isiwe na vigezo vyao* vya kuboresha huduma zetu za afya kwa MACHUJIO hayo?!!!

Sakala wewe[emoji1787][emoji1787]
 
Yaani wewe ni bumunda kweli. Hivi preintetnship mantiki yake ni ipi hada? Kinachofanywa kwenye Logbooks hua ni kitu gani au kinasaidia nini?
Sikiza wewe hobobo....

Hivi unajua kuwa wako wanafunzi wanatunukiwa SHAHADA zao za udaktari na kutokwenda kufanya INTERNSHIP na kuingia mitaani kubangaiza njia nyingine za kimaisha(hatakiwi kutibu)...japo anabaki kuwa ni "DAKTARI...ILA ASIYETIBU"

Kwa sababu ya hili ndio maana MCT wakaweka utaratibu wa PRE-INTERSHIP EXAMS ili kuwafanya wale wahitimu wanaotaka KUTIBU wawe na mipango ya NIDHAMU bora ya kimasomo toka wakiwa mavyuoni...unapewa "pepa" ili uweze kupata cheti cha kwenda kufanya INTERNSHIP(mafunzo ya utarajali) kinaitwa PROVISIONAL REGISTRATION....

Huko katika mafunzo ya utarajali hupewa vitabu(log books) wanatakiwa wakishamaliza internship wavipeleke MCT...pamoja na cheti cha taaluma Kutoka hospitali waliofanyia mafunzo ili "wakishatahiniwa" wapewe FULL REGISTRATION &LESENI YAO...sasa wako ambao wanapita njia za panya(hawako serious huko mafunzoni ,wako wanaofoji kujaza hizo LOG BOOKS hata kwa kubebwa....rushwa tofauti....).

Ukiyakusanya hayo utamaizi kuwa MCT haijakosea kuweka hatua hizo na WAZIRI UMMY MWALIMU hana kosa lolote...

Umesikia "pungerrr sese" ?!!

Sawa "pungerrr sese"?!!!

Umeelewa wee "pungeeer"?!!
[emoji1787][emoji1787]
 
Hawataki mitihani wakati wanajiona wajuaji sana. Angalia waliopo makazini utaelewa nasema nini. Mitihani iwepo ni muhimu sana kuchuja na hii italeta nidhamu kazini. Wakiajiriwa utasikia wanaanza kudai nyongeza za mishahara bila kujali kwamba wao ni watoa huduma siyo wazalishaji.
Mitihani iwepo na tena iwe migumu na kila mwaka itungwe mipya ili kwenda na wakati, wasiache mtihani ukawa ule ule utachuja kisha itakuwa siyo haki kwa waliotangulia maana wafuatao wataanza kuyafahamu maswali na kuacha kujifunza badala yake wakaanza kusoma kufaulu mitihani.
Hili la mitihani liwe kwa kada zote nchini, hakuna mshahara unaonyesha kama mvua. Wahitimu watahiniwe ili tupate wataalamu wenye kuleta tija, badala ya wasaka tonge.
Na mitihani isiwe rahisi, maana tunaona nchi inavyochezewa, unakuta wanunua vyeti ndio viongozi wakuu, kapachikwa na aliyekuwa kiongozi mkuu ama kwa rushwa, au kujuana. Hatutaki haya yajirudie.
 
Hata kama hataki ujumbe umeshafika. mitihani lazima hata kama wakipewa mitihani ya USMLE wafanye tu, wao si wamehitimu? sas wa prove kwamba wako tayari, ujanja ujanja ndio tatizo la nchi yetu hii. Kuna watu wanasoma wako makazini, mitihani wananunua na wanfaulu kuliko hata wale wanaojituma haswa. Hakuna kulegeza MCT isimame imara, hatutaji madaktari mabishoo sisi.
 
Acha vijana wafanye mitihani, hiyo mikopo yao ya HELSAB isiwe kigezo cha kulegeza, wakaze tupate vijana bora. Hatutaki kila siku wananchi tukimbilie India, tunataka ngoma ziishie hapa hapa mkuu.
 
Wewe unayalalamika ni mjinga sana. Zamani Medical Drs walisoma kwa mwaka then final exam ya mwaka but baadaye wakasoma kwa semester kitu ambacho kinapelekea kuwa na medical doctors wabovu (baadhi). MCT wapo sahihi na ndiyo maana nchi zilizoendelea kuwa medical doctor siyo suala la kujaribu. Fanyeni hiyo mitihani muache ujinga. Nayajua mengi sana sema sima muda ila MCT wapo sahihi na mitihani lazima mfanye, kutibu siyo kujaribu!
 
Binafsi jana nilileta uzi humu kulisemea hili humu MCT kwa kiburi chao wakaandika taarifa kwa umma wakijua itawasaidia. Hili baraza bure tu lipanguliwe
Wewe ni idiot, MD lazima wapimwe. Eti unakuta doctor ana google ugonjwa kama raia. Nyie MD wa semester mnasumbua ndiyo masna vifo vingi
 
S

Shit, USA wana Pre and post USMLE?
Mantiki ya pre internship ni kupima utayari wako wa kutoa huduma chini ya usimamizi na una pata "provisional licence" na mantiki ya post intern ni kupima utayari wako kwenda kuachiwa mgonjwa mwenyewe bila usimamizi na unakuwa registered rasmi you are on your own ... Ukifeli hapo maana yake wewe bado ...
 
Yaani Issue ya interns ndio iondoe mtu

Naona mmevimba vichwa hata kabla hamjapewa vibali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…