ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,424
- 4,954
Tatizo la Mgao wa Umeme limekuwepo kwa muda mrefu sana, Toka enzi za Nyerere, na Sasa tatizo hilo linaendelea kuwepo , sisi watu wazima tumeona mgao Kwa Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa mgao upo kwa Samia.
Hili ni Tatizo kubwa sana, japokuwa Wamebadilishwa mawaziri na watendaji wakuu wa TANESCO Mara kwa mara bado tatizo limeendelea kuwepo na wananchi wanazidi kulalamika.
Kipindi cha Magufuli ulitumika ujanja ujanja Ili kupunguza Makali ya mgao , japo mabwawa yalikauka na mgao ulikuwepo, kwa maana kilichofanyika Serikali ilitoa maelekezo kwa watumiaji wachache ambao wana matumizi wakubwa ya umeme kuzima mitambo hali iliyopelekea watumiaji wengi/wapiga kura kuonja kidogo makali ya mgao, ila athari zilikuwapo sana kiuchumi mana uzalishaji ulipungua.
Kwa mwaka huu tumekuwa na mgao wa umeme Toka January kwasababu mbalimbali hasa hitilafu za mitambo na mabwawa kukauka maji.
Sasa Swali langu he ni nani atakuja kutumalizia tatizo hili Sugu/Cronic la mgao wa Umeme, huku ndani ya tatizo Hilo tukiwa na tatizo jingine la kukatika katika kwa umeme ambalo halisababishwi na mabwawa kupungua maji.