Rais gani atakuja kumaliza tatizo sugu la mgao wa Umeme?

Rais gani atakuja kumaliza tatizo sugu la mgao wa Umeme?

Sasa Swali langu he ni nani atakuja kutumalizia tatizo hili Sugu/Cronic la mgao wa Umeme, huku ndani ya tatizo Hilo tukiwa na tatizo jingine la kukatika katika kwa umeme ambalo halisababishwi na mabwawa kupungua maji.
Rais atakayekuja kumaliza tatizo la mgao wa umeme ni yule atakayekuwa yuko madarakani Bwawa la Umeme wa Maji la Mwalimu Nyerere litakapoanza kufanya kazi
 
Tatizo ni sheria zilizopo zinazoipa serikali monopoly kwenye hii biashara ya umeme, waruhusu sekta binafsi kufanya hii biashara in full, kwa wasiolewa Tanzania sekta binafsi hairuhusiwi kuuza na kusambaza umeme moja kwa moja kwa wateja, unaweza kuzalisha na kuiuzia TANESCO na wanakupangia bei ila huwezi kuuza kwa wananchi au wazalishaji, hakuna mtu mwenye pesa anaweza kufanya biashara kichaa kama hiyo, ni sheria na sera zetu ndio zinaleta matatizo yote haya, imagine biashara ya simu ingekuwa TTCL peke yake ndio anaruhusiwa kuuza huduma za simu
Usimamamizi na uendeshaji wa mashirika ya uma hukosa ufanisi kwa sababu ya siasa (asilimia kubwa ya wanasiasa ni wajinga na hata wapumbavu wenye kiburi cha madaraka, hawajali utaalamu).
 
Alitaka hilo tatizo lipungue kwa kujenga bwawa la maji ambapo unaambiwa tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi?! Au angeleta mvua zake?
Ndio nyie mmejaa makamass kichwani Marekani na maendeleo yao yote umeme wa maji wanatumia sasa huku tukajazwa ujinga na sisi km kondooo ndo tunakubali tu
 
Jiwe alitakiwa kujenga kinyerezi 3&4,umeme wa uhakika wa gesi,akakimbilia rufiji,gharama kubwa,maji si uhakika
Alitaka umeme wa rufuji maana ni wa gharama ya chini mwananchi angekua anapata umeme kwa bei nafuuu kabisa ww gas leo ipo hapo mtwara je bei imepungua si ndo tunakandamizwa bei yule jamaa basi tu Mungu ampumzishe kwa amani
 
Una uhakika gani kuwa umeme huo ungekuwa wa bei rahisi? Mbona ndege ni zake lakini bei ya usafiri ilikuwa ghali kuliko fast jet?
 
Tatizo la Mgao wa Umeme limekuwepo kwa muda mrefu sana, Toka enzi za Nyerere, na Sasa tatizo hilo linaendelea kuwepo , sisi watu wazima tumeona mgao Kwa Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa mgao upo kwa Samia.

Hili ni Tatizo kubwa sana, japokuwa Wamebadilishwa mawaziri na watendaji wakuu wa TANESCO Mara kwa mara bado tatizo limeendelea kuwepo na wananchi wanazidi kulalamika.

Kipindi cha Magufuli ulitumika ujanja ujanja Ili kupunguza Makali ya mgao , japo mabwawa yalikauka na mgao ulikuwepo, kwa maana kilichofanyika Serikali ilitoa maelekezo kwa watumiaji wachache ambao wana matumizi wakubwa ya umeme kuzima mitambo hali iliyopelekea watumiaji wengi/wapiga kura kuonja kidogo makali ya mgao, ila athari zilikuwapo sana kiuchumi mana uzalishaji ulipungua.

Kwa mwaka huu tumekuwa na mgao wa umeme Toka January kwasababu mbalimbali hasa hitilafu za mitambo na mabwawa kukauka maji.

Sasa Swali langu he ni nani atakuja kutumalizia tatizo hili Sugu/Cronic la mgao wa Umeme, huku ndani ya tatizo Hilo tukiwa na tatizo jingine la kukatika katika kwa umeme ambalo halisababishwi na mabwawa kupungua maji.
Mmmm sijui! Pengine ni mpaka Upinzani utinge IKULU, lakini sio Lissu- nakazia tu. Upinzani chagueni wagombea MAKINI, msirudie tena kutuletea makapi yaliyotupwa na CCM. Na wala wakereketwa design ya LISSU.
 
Alitaka umeme wa rufuji maana ni wa gharama ya chini mwananchi angekua anapata umeme kwa bei nafuuu kabisa ww gas leo ipo hapo mtwara je bei imepungua si ndo tunakandamizwa bei yule jamaa basi tu Mungu ampumzishe kwa amani
Marekani Kuna mgao wa maji Sasa hivi,vyanzo vimekauka,umeme wa maji hauaminiki Tena sababu ya mabadiliko ya tabia nchi,south Africa waliingia gizani baada ya bwawa kukauka,mwaka Jana mvua hazikutosha,na mwaka huu mvua hakuna,jakaya alileta wabrazil kufanyia tathmini rufiji,lakini akaona kwanza tuwe na umeme wa gesi wa uhakika kwanza,akamwachia mwamba mipango,mwamba mjuvi
 
Shida ya umeme ni ya kutengeneza wanamhujumu mama hali hii wajue kukua kwa uchumi kwa 5.4 % utateremka sasa hivi uzalishaji na upatikaji wa maji mh mh mh ..
 
Una uhakika gani kuwa umeme huo ungekuwa wa bei rahisi? Mbona ndege ni zake lakini bei ya usafiri ilikuwa ghali kuliko fast jet?
Umeme wa maji ni umeme rahisi duniani kote swala la ndege tuliache tuongeleee kitu kinachogusa maisha ya kila mtanzania
 
Manyumbu yaliyomtusi MAGUFULI yanapita kimya kimya kwa aibu.

Hii ndio raha ya DEMOKRASIA. Tunakula DEMOKRASIA chini ya MAMA SAMIA SULUHU HASSAN.

Ukweli na uwazi. Asali na haki ya mazungumzo.
 
Marekani Kuna mgao wa maji Sasa hivi,vyanzo vimekauka,umeme wa maji hauaminiki Tena sababu ya mabadiliko ya tabia nchi,south Africa waliingia gizani baada ya bwawa kukauka,mwaka Jana mvua hazikutosha,na mwaka huu mvua hakuna,jakaya alileta wabrazil kufanyia tathmini rufiji,lakini akaona kwanza tuwe na umeme wa gesi wa uhakika kwanza,akamwachia mwamba mipango,mwamba mjuvi
Sasa huo wa gas umeishia wapi na swala la maji kukauka ni hali ya kawaida tu sio endelevu mvua lazima inyeshe tu sema ni kuzuia tu uharibifu wa mazingira.Lakini gas mpaka sasa hata hatujui ni ya nani maaan mikataba wanaingia kimya kimya.
 
Siku CCM na wanyonyaji wake wakifa ndio hii nchi itapona
 
Mnaosema mgao hauishi napata ukakasi maana tuliambiwa bwawa la Nyerere litazalisha megawati 2500 Tena tutakuwa na surplus ya megawati 1500 Sasa mgao Ni njama za Watu au Ni uhaba was nishati Hapa ndipo sielewi
 
Back
Top Bottom