Tatizo ni sheria zilizopo zinazoipa serikali monopoly kwenye hii biashara ya umeme, waruhusu sekta binafsi kufanya hii biashara in full, kwa wasiolewa Tanzania sekta binafsi hairuhusiwi kuuza na kusambaza umeme moja kwa moja kwa wateja, unaweza kuzalisha na kuiuzia TANESCO na wanakupangia bei ila huwezi kuuza kwa wananchi au wazalishaji, hakuna mtu mwenye pesa anaweza kufanya biashara kichaa kama hiyo, ni sheria na sera zetu ndio zinaleta matatizo yote haya, imagine biashara ya simu ingekuwa TTCL peke yake ndio anaruhusiwa kuuza huduma za simu