Rais hajui kuzungumza na wananchi, ziara za njiani zisitishwe

Hayo matatizo unayoeleza yanapaswa kutatuliwa na madiwani, wabunge, wakuu wa wilaya na mawaziri. Jaribu kujifunza kazi za Rais ni zipi.
Mie naona Rais atusaidie kubana matumizi, kwa kuondoa vyeo vya hao wasaidizi wake kama hao,ambao siku zote wanashindwa kumsaidia kutatua kero za watumiaji na kusubiri kila kitu Rais mpaka aje atatue. Na ili kusave pesa ya kodi tunaowalipa ya mishahara ya bure wanayolipwa hao mabwana bila tija, ni afadhali pesa hiyo ielekezwe na ikasaidie kujenga matundu ya vyoo vya shule vijijini....
 
kusikiliza kero za wananchi ni mambo ya kishetani?
Kero za wananchi hazitakiwi kufika kwa rais moja kwa moja kuna utaratibu wake , ndio maanabkuna madiwani na wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa nk. na hii ni ili kuepusha maamuzi ya ukandamizaji na unyanyasaji yasiyo na utu, maana maamuzi na kauli ya rais kwa mtu yeyote yule sio jambo la mchezo ,

wananchi wengi wamejawa na majungu na chuki dhidi ya watumishi wa umma na hilo halina pingamizi hicho ndicho alicho kuwa anakifanya magufuli na wafuasi wake, hatutaki mfumo ule ujirudie! Kero za wananchi zitatatuliwa kwa utaratibu unao takiwa na sio majukwaani kutukana wasaidizi na watendani wa chini mbele ya jamii inayo shangilia na kupiga miluzi ya furaha na kutaka sifa , watu wameumizwa sana wakati wa magufuli tena wengine bila hatia,watu wamedhalilishwa na kutwezwa utu wao, watu wamevunjiwa heshima mbele ya wanao waongoza na familia zao eti kisa tu mwananchi tabulalasa asiye jua utaratibu kalalamika jambo ambalo ni la kitaalamu na sio nguvu au siasa.

Rudini kwenye mifumo ya uongozi na sio mifumo ya utawala na mzilazimishe akili na fahamu zenu zitambue kwamba mnatakiwa kuongozwa na sio kutawaliwa
 
Kwenye hili Mkuu naungana na wewe moja kwa moja..

Kuna haja gani kusimama mtaani kwetu na kutusababishia foleni na shughuli za kiuchumi kusimama alafu mwisho wa siku shida,kero zetu unazipiga denge?
 
Tatizo mlisha zoeshwa tabia za kishezi na hilo ndilo tatizo mlisha sahahu uongozi mkazoeshwa utawala.

Kwako wewe presidential materia ni kufokea fokea na kutukana wasaidizi wako hadharani kwenye majukwaa au kwa wewe presidential material ni ipi maana yawezekana hata qualities of president hujui hata moja ila una linganisha tabia binafsi ya magufuli na tabia binafsi ya mama samia kitu ambacho si kipimo sahihi cha presidential characteristics.
 
Tukubaliane kwamba nchi iko mikononi mwa mtu kwa mda.

2025 tufanye jambo.
 
Mlizoea tabia za hovyo Na kuropokewa na Ahadi hewa.....!!! Anapopita zote zinaandikwa Na kufanyiwa kazi kwenye sehemu husika.
 
vipi endapo hao uliowataja hawazitatui?
 
Hizo alikuwa anaziweza shujaa magu, mchele unamwagwa hadharani....
 
Waziri Mkuu ndiyo mtendaji mkuu wa Serikali, na yeye akifika sehemu fulani huwa tayari analo jambo lake. Hii ni tafauti na Raisi kusimama njiani tu na kuanza kutoa hukumu. Matukio kama haya mara nyingi yanaleta kudanganywa.
 
Samia ni dhaifu,acha kujificha kwenye mazoea,tangia amepata urais ameisha tatua shida hipi?Labda kufungulia alishababu na Mafisadi, sasahivi rushwa imerudi kwa mwendo wa 5g
wewe ulishaacha kula rushwa toka lini?
 
Mwaka 2024 utaona wanazikumbuka mbinu alizotumia hayati Magu.
Kutakuwa na copy ya mambo mengi sana.
 
Mwaka 2024 utaona wanazikumbuka mbinu alizotumia hayati Magu.
Kutakuwa na copy ya mambo mengi sana.
JPM alikua sehemu kubwa ya tatizo la nchi hii na CCM, paka leo SSH ni victim wa uongozi wake. Mtu yoyote anae jua utawala demokurasia na utawala wa sharia hawezi kumiga au kumkumbuka Magu.
 
Rais hayuko kwenye ziara za kusikiliza kero,na hata afanyaje kero haziwezi kuisha
 
Binafsi huwa nauliza kwa nini vitu vidogo kama hivyo vinahitaji Rais?

Viongozi wa Nchi hii wanakwama wapi? Imagine wananchi wanamueleza Rais tatizo la vyoo stand aisee kama ni DED upo nakufukuza mara moja huu ni utoto.
 
Mh.Rais wala hakosei....

Yuko sahihi kabisa....

Mh.Rais hawezi kuwa na "style" ya hayati JPM....


#SiempreJMT
#SiempreChifuHangaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…