Rais Hussein Mwinyi kuongea na Serikali ya Muungano ili Zanzibar ianzishe mfuko wa kusaidia Waislam

Umeshtushwa nini sass?
Off course inashtua. Serikali kughalamikia safari binafsi ..... Na Waroma ambao huwa wanakwenda kuhuji Roma nao wakiomba wawezeshwe itakuwaje ......!!?

Waislamu wanatakiwa kwenda Hijja pale wanapokuwa uwezo huo .... Kama huna unabanana humuhumu. Hili la kuwawezeshana litatarget watu wachache tu na siyo sustainable. Anataka kujipatia umaarufu bila sababu ya maana .....!!
 
Muungano hauna mapato, bali yale mapato ya Tanganyika hubatizwa na kuitwa mapato ya Muungano!!
Kiasi ujambe hivyo kwani mapato yote ya bait la jaibu Na sehemu Za historia Zanzibar yanapelekwa Tanganyika Na Pia pesa Za viza zote Za wanaingia Airport Na bandarini zinakwapuliwa Na Tanganyika pesa Za Wazanzibari walioko nje zinaingia Tanganyika nk
 
inaitwa Sadakatil jaria,katika dini ya Kiislamu kuna sadaka za aina nyingi..

Kumpeleka mtu Makka ni moja katika hizo sadaka..

Dangote anawapeleka zaidi ya wailamu 50 kwenda Makka kuhiji kila mwaka..
Tafsir ya Hijja ni pana sana. Mi huwa nacheki zaidi Quran na Hadithi , Just imagine huna kazi , una madeni na huna pesa ya kuhudumia familia ila kuna dili la kupelekwa hijja for free!

Unaenda Makka na kurudi home kwenye maisha ya msoto na dhambi zinaendelea kufanyika maana mtu maskini anafanya dhambi nyingi!

hiyo imekaaje sheikh!
 
Amegundua huko Zanzibar wanaimani kubwa kwenye uislamu, hivyo namna pekee ya kuwaziba macho ni kuwawezesha kwenye jambo linalogusa imani yao. Na alifanikiwa hilo ataweza kukaa madarakani kwa kunajisi uchaguzi, huku akiwa ana kinga ya kujali uislamu.
 
Lakini mbona Viongozi wa Ulaya na Marekani sijawahi kuwasikia wakizungumza mambo ya Dini wala kuwenda kanisa ni?
ha ha ha!
Ulaya na Marekani hakuna Mungu boss! Kanisani ni mahali pa kufanyia mikutano na sherehe!!waumini unawatafuta kwa tochi, wale wazee vikongwe! tembea uone mkuu!
maybe 1 to 10 percent ya wazungu ndo wakristo na waislam
The Modern White race hasa vijana believe in science and not faith (vitu visivyoonekana kwa macho!
 
Ili kuondoa upendeleo,huo mfuko uwe kwa kila anayetaka kwenda kuhiji(hata wakristo huenda hija,Israel).
Kama vile serikali ikiombwa huwa inapunguza Kodi au kutoa ruzuku kwa taasisi za kidini,kama hospitari na shule.basi huo mfuko usiwe kwa Islam peke yao,hiyo pesa ni Kodi ya umma,haiwezi kutumika kuendeleza dini moja,
 
Ahadi za kuendana na mazingira na wakati aliopo Rais, tusubiri utekelezaji
 
Mkuu mbona unamsakama sana mheshimiwa Rais kwa mambo mazito hivyo?

Issue ya (a) visiwa kila akikutana na wanahabari huwa anagusia maana maswali huwa hayakosekani, but yeye ndiye wa kwanza kufanya hivyo?.

(b) masoko na barabara yanayojengwa bububu, kwerekwe ni pesa mliyokuwa mnapiga kuruhusu mizigo ya rafiki na ndg zenu pale bandarini au uwanja wa ndege.

Pale darajani ni mkataba kati wa watu binafsi, serikali na chama cha mapinduzi.
 
Sasa nini kinawazuia kutoa pesa si wampe tu kama wana nia njema?
 
Amegundua huko Zanzibar wanaimani kubwa kwenye uislamu, hivyo namna pekee ya kuwaziba macho ni kuwawezesha kwenye jambo linalogusa imani yao. Na alifanikiwa hilo ataweza kukaa madarakani kwa kunajisi uchaguzi, huku akiwa ana kinga ya kujali uislamu.
Ni kosa kubwa kujenga popularity yako ya kisiasa kwa kujenga hoja za kidini
 
Zenji iko huru ina bendera yake..rais wake unataka uhuru gani.?

#MaendeleoHayanaChama

Uhuru wa kusaini mikataba ya kimataifa, uhuru wa kuwa na mwakilishi UN, uhuru wa kuwa na benki kuu yetu, sarafu yetu, uhuru wa kuchagua tunayemtaka siyo hao vibaraka wenu mnaotulazimishia mpaka mnauwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…