Unajua ukubwa wa Rwanda na idadi ya watu? Unahisi ni kitu sawa kutengeneza udhaifu na morali ya kutafuta kwa wananchi? Utakula na kuishi kwa jasho lako popote duniani hapa,na huwezi fananisha maisha ya nchi moja na nyingine duniani kote,ni ufinyu wenu tu wa kifikra
Binafsi sipendelei serikali kuwajengea watu nyumba. Serikali haina uwezo wa kujengea watu wote nyumba na suala zima haliko sustainable.
Napendelea serikali kuwa na sera za kuwawezesha watu kujijengea/ kununua nyumba.
Kwa mfano, hakuna sababu yoyote ya muhimu ninayoielewa ya kuzuia mfumo wa mortgage, watu wakauziwa nyumba kwa mfumo wa kulipia kidogo kidogo katika miaka kadhaa. Na wakishindwa kulipia kwa mwaka nyumba inapigwa mnada.
Shirika la Nyumba lingefanya utafiti kwa ushirikiano na benki zetu kuhusu mfumo huu, watu wengi sana wangeweza kumiliki nyumba.
Unakopa benki kununua nyumba, unalipa kidogo kidogo, with interest. Collateral ni nyumba.
Wewe unapata nyumba bila kulipa hela nyingi kwa pamoja. Benki inapata interest, shirika la nyumba linapata faida kwa kuuza nyumba. Nchi inaondokana na watu kukaa kwenye makazi hafifu.
Mtu anafanya kazi ya kawaida miaka 30, anachukua mkopo mwanzo wa kufanya kazi, akistaafu amemaliza kulipia nyumba, anarithisha familia nyumba. Huyo mfanyakazi wa kawaida tu. Hahitaji kuchukua rushwa wala dili kujenga nyumba.
Kwa kiasi kikubwa, serikali ya Tanzania imeshindwa katika yote hayo mawili. Imeshindwa kuwajengea watu nyumba, na imeshindwa kuweka sera za kuwawezesha watu kujenga au kununua nyumba. Mpakq mtu kuwa na nyumba inaonekana ni tajiri. Wakati nyumba bora ni hakinl ya kila mtu.
Mfano mzuri wa karibuni kuhusu kushindwa kwa serikali kuwa na.sera nzuri kwenye ujenzi wa nyumba ni kupanda kwa bei ya sementi.