Rais Kagame amejenga nyumba kwa wasio na uwezo wa kujenga makazi bora, wengi wao ni wazee.

Kuna hali za maisha hutokea mtu akashindwa kulipa mortgage, mfano kufiwa na mwenza ambae ndiye mwenye kipato kikubwa, kupata redundancy kazini, kuugua ugonjwa wa muda mrefu.

Kwa hali kama hizi social housing zinasaidia jamii. Nyumba zinazopangishwa chini ya gharama za soko la nyumba mtaani. Mradi raia akidhi vigezo vya kupata nyumba hizo.

Nyumba bora husaidia kuimarisha afya ya jamii na afya njema hukuza uchumi.
 
Hivi Rwanda ina wazee na wasiojiweza wangapi? Na Tanzania tunao wangapi na wako wapi? Tunaweza kusema Kagame amefanya jambo kubwa sana kuliko yanayofanyika hapa TZ na tumuige? Kagame si ndio alibadili katiba aendelee kutawala? Tumuige?
 
Hivi Rwanda ina wazee na wasiojiweza wangapi? Na Tanzania tunao wangapi na wako wapi? Tunaweza kusema Kagame amefanya jambo kubwa sana kuliko yanayofanyika hapa TZ na tumuige? Kagame si ndio alibadili katiba aendelee kutawala? Tumuige?
Wale jamaa unaowaambia, bahati mbaya sana, kwa masikitiko makubwa, hawana full view ya matukio wala hawafikiri katika dimensions zote 16, na mduara wa nyuzi 360. Mtazamo wao ni wa ^kisaidi mira^ ya motokaa, na lazima kuna blind spots zinawakosesha kufanya tathmini na mrejesho uliokamilika. Wanastahili, siyo kubezwa na kukosolewa na kupuuzwa, bali kuonewa huruma, kusikitikiwa na kufundishwa kama tutoto tudogo labda huenda pengine possibly kuna some hopefulness kwao huko mbeleni sana; vinginevyo, ^adios!^
 
Huko umeenda mbali, basic mortgage tu sijaona ikitumiwa kwa kiasi kikubwa Tanzania.

Kitu kimoja naona hatuna credit bureaus/ history kuangalia creditworthiness in a systemic way.

Lakini, mtu akishindwa kulipa mortgage ya nyumba si collateral ipo nyumba yenyewe, hapo kuna tatizo gani?
 
Katika miji mingi mikubwa duniani ndiko kuna familia zinazoishi katika umasikini uliokithiri. Tabaka la watu hawa ndiyo linalotumiwa na wafanya biashara na wawekezaji wakubwa kupata faida katika uwekezaji wao. Jamii hii hulipwa ujira mdogo kwa ajira ya masaa mengi.

Wazazi hulazikimia kutokuwepo nyumbani muda mrefu wakisaka hela za kodi ya nyumba, chakula na mavazi. Hata katika nchi zilizoendelea ambako kuna socia housing, jamii hii inahitaji jicho la karibu kwani kuna uwezekano mkubwa ya vizazi vyao kuishi maisha haya haya. Watoto wanatumiwa na wafanya biashara haramu kufanya biashara zao kwasababu wazazi wao hawawezi kuwapa malezi, muda mwingi wako makazini.

Kwa nchi kama zetu jamii hii, baba unamkuta ameajiriwa anauza duka mjini, mshahara kwa mwezi ni laki mbili. Mke wake anaamuma kuuza mboga mboga mtaani siku nzima. Wamepangisha chumba kimoja na wana watoto. Watoto usiku wanaombewa kulala kwa jirani. Kumbe jirani anawatumia vibaya watoto usiku, wakiume wana lawitiwa na wakike kupata uja uzito.

Mtu anaepata mshahara laki mbili kwa mwezi atapa mortgage gani au anaweza vipi kupata hela ya deposit?
 
Zi lazima kuwapa mortgage watu wote, kutaka kila mtu awe na nyumba ni moja ya sanmbabu iliyopelekeq kutokeq kwa mortgqge crisis late 2000s.

Serikali haiwezi kumsaidia kika mtu, inatakiwa na mtu naye aweke effort kuj8kwamua, kusoma na kupata career, kupata mtaji wa biashara etc.

Hivyo, hakuna sababu watu wenye formal employment na careers kupata shida sana kujenga nyumba, au kujenga nyumbabsehemu mbali sana na mjininwakati kazi zao ziko mjini.

Kwa sasa hivi kujenga nyumba ama kutamchukua mfanyakazi wa kawaida muda mrefu sana ama kuko nje ya uwezo wake kabisa. Kuna watu wengi tu wanalipwa kati ya 500,000 mpaka 1,000,000 na zaidi, wana skills, training na careers, wangewezwa kuingizwa kwenye some sort of a mortgage. Mtu anayelipwa sh 1,000,000 kwa mwezi, ukimpa mkopo wa 100,000,000 aulipe kwa miaka 30 kwa ajili ya nyumba ambayo kasha close, na collateral ni nyumba, atashindwa kulipa? Huo ni kama mshahara wake wa miaka minne tu discounting all else.

Sasa hawa watu wanaolipwa 500,000 mpaka 1,000,000 kwa mwezi wapo wengi hawana nyumba na hawawezi ku afford kulipa 100,000,000 kwa mpigo. Matokeo yake, ili kujenga, wanajiingiza katika mambo ya rushwa na njia za panya makazini.

Hao ndio wangekuwa target market. Ukimsaidia huyo mmoja umesaidia wengi, Kiafrika hiyo nyumba ninnadra yeye kukaa peke yake.
 
Ninaona umeangalia uchumi wa watu wenye kipato cha kati, lakini watu wenye kipato cha chini ni wengi sana na hawa ndiyo wanasaidia uwepo wa watu wenye kipato cha kati.

Kuna dereva aliyajiriwa kupeleka watoto wa boss shuleni,
Mkata majani, housekeeper, house girl. Hawa mishahara yao haizidi laki tatu.

Socialisation pia, kama kukiwa na nyumba za Wilaya, self contained ya vyumba viwili unaipata kwa laki moja na nusu. Itasaidia kuondoa ushamba. Mimi nanaeishi Buza Kwa Mpagale nimezoea choo cha shimo. Leo ninalazwa Mloganzila si ndiyo nitatumia karatasi ya fullscape kujisafishia kumbe inaziba choo.
 
Akili kubwa ni Prezidenti Bulldozer anayewaandaa vijana mapema ili hatimaye waweze kununua viwanja vyao wenyewe

Anawaandaa vijana kwa kuwasomesha chini ya miti na shule zisizokuwa na vyoo? Unawaandaa vijana kwa kuwaminyia uhuru wa kujieleza na kuwa waoga wa kukosoa? Taifa linaloloendelea huletwa na umoja na sio mgawanyiko wa wananchi wake!! Jiwe apende asipende nchi imeganyika kati ya watu wa Chato na wasio wa Chato!!! Wale wa Chato ndio wanaofaidika na utawala wake wakati hao wengine ni watazamaji tu!!!
 
Ukianza kusaidia watu wenye uchumi wa kati, eventually utaongeza watu wenye uwezo wa kusaidia wengine na methodically utanyanyua hata wa uchumi wa chini.

Ukitaka kuanza kwa kusaidia watu wote kwa mpigo, hutapata hata nafasi ya kuanza. Watu hao ni wengi sana.
 
Hata akijenga hakuna jipya. Asipo weza kuachia ngazi nakufanya nchi iwe na utaratibu wakubadilisha madaraka Rwanda haitopona. Rwanda ina hitaji kiongozi atawaponya vidonda vya madhila ya ukabila na kuwaunganisha kuwa wamoja hayo majengo na maendeleo hayatoweza kuwaponya changanya serikali hutus and tutis. Tungeni katiba itaruhusu makabila yote kukaa kwenye kiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…