Rais Kikwete afanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu watano wapya

Rais Kikwete afanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu watano wapya

Katiba inasemaje kuhusu uteuzi?tusome kwanza halafu tu coment,Watanzania hodari sana wa kukariri.Tuwe makini jamani.
 

Attachments

  • 1445677349917.jpg
    1445677349917.jpg
    33 KB · Views: 146
Mambo ya mtandao,ukawa wanakurupuka na kutoa kauli zisizo na maana,inatakiwa kwanza kupata source na ukweli wa habari yenyewe,hapo mkapa hakukosea kuita malofa na mbumbumbu
 
Somaibara ya 42 (3)(a) ya katiba ya jamhuri ya muungano uone madaraka ya rais yanakomea wapi .na kama huju hata kesho anaweza kufanya uteuzi hata mara baada ya kura kupigwa
Sheria inaendana na busara. Dibagula, alipofungwa kule Morogoro, sheria ilifuatwa. Akahukumiwa; lakini mazingira ya uvunjifu wa amani uliifanya Mahakama ya juu ione busara ya kufuta kabisa ile hukumu kwa mkosaji. Unachoona hapo ni kwamba pamoja na sheria kuwa ilitumika vizuri, bado busara ilitawala na ikaifanya nchi ikatulia.
Kwa hili la JK kuendelea na uteuzi hadi dakika za majeruhi ni kweli Kikatiba yuko sahihi, lakini busara inagoma kabisa! Huwezi kuwa unajindaa kuondoka madarakani wiki moja ijayo halafu ukaunda safu unazotaka wewe. Hii ni gharama. Kumbuka, huyo anayekuja anaweza kupangua wote hao, na wakalipwa mafao! Mzigo ni kwa mwananchi maskini. Yeye atakuwa anakula maisha yake ya ustaafu kama kawaida. Fikiria, mtu dhaifu kabisa kama Kipande anampa madaraka baada ya kuvuruga Bandari! Huyu Rais ni wa pekee, si kwa Afrika Mashariki na Kati pekee, bali ulimwengu mzima. Tulipomuunga mkono mwaka 2005 hatukujua tunaunga mkono aina hii ya kiongozi! Mungu atusamehe. Watanzania watusamehe, na zaidi ya wote; Dk. Salim Ahmed Salim atusamehe!!
 
Raisi wa nchi hii mpaka sasa ni Jk kikwete. Ana haki na wajibu kikatiba kuteua. Nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa katiba, sheria,kanuni na taratibu. He is absolutely right and correct.
 
hii kampuni ya ccm inazidi kuweka watendaji waliofeli katika management yao ya sasa ili waendelee tena... anyway labda kwa ajili ya magawio makubwa, maana wata i liquidate kesho watu wapewe vyao wasepe.... CCM OUT
 
Anaweweseka.
Huo uteuzi hauna faida kwa wananchi.
Ni kulipa fadhila kwa mtandao wake wa kifisadi.
 
Yaani huyu TeziDume ni Mburula kabisa. Dunia nzima inamshangaa!
 
Eeehhh.. OMARI CHAMBO...!!!

Omari CHAMBO..

OMARI CHAMBO... huyu ni shemeji wa JK...na a total failure ktk UONGOZI... Dr. MWAKYEMBE alimkataa kabisa kabisaaa ktk Wizara ya Uchukuzi, akapata kashfa kibao Wizara ya UCHUKUZI... akashushwa cheo baada ya makelele ya kila sehemu.. akapelekwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara..!!!

Leo Omari Chambo anarudishwa Wizara nyeti kama ya MADINI NA NISHATI kulinda maslahi ya JK...!! Ya gas na mafuta...!!!


🙆🙆🙆😨😨😨😨❌❌❌❌❌

CCM jamani.. bado imemrudisha MASWI tena...!! 😨😨😨

CCM out.. out.. out..!!!
 
Anaweweseka.
Huo uteuzi hauna faida kwa wananchi.
Ni kulipa fadhila kwa mtandao wake wa kifisadi.
 
Magufuri kawekwa kama boya tuu.angeheshimiwa kama raisi ajaye kimsingi angeachwa kuja kufanya teuzi mwenyewe,lakini kwa vile JK kasoma upepo kuwa magu hatashinda na pia kapata fununu kuwa Raisi Lowasa hatawaondoa watumishi wa umma kwenye nyadhifa zao akaona afanye kuwateua haraka kwa masilahi yake.
 
Wakuu ikulu ni shangwe Jk anadhihirisha serikali yake ni ya kishikaji amemteua shemeji yake Omar chambo Katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini

Omari Chambo ni Mzigua Huo ushemeji na kikwete Umetoka Wapi Mkuu
 
Maelfu ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM, uliofanyika leo kwenye Viwanja hivyo mjini Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohammed Shein akisalimiana na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu hassan baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.
Mgombea wa Urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein akimsalimia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar leo. Wengine ni Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Waziri Kiongozi Mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha
Mgombea Mwenza Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo katika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar.
Kijana wa Kimasai anayeishi Zanzibar, akishangilia kwa dhati wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal akihutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akizungumza kwenye mktano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Blal akimpongeza kwa hotuba nzuri Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi baada ya kuhutubia mktano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar
Dogo Aslay akitumbuiza wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo Kibandamaiti mjini Zanzibar
Shabiki wa CCM akishangilia kiaina wakati wa mkutano wa kufunga kapnei za CCM uliofanyika leo kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar leo

Mgomea Mwenza wa Urais kwa tikei ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar.
 
JK ATEUA MAKATIBU WAKUU WANNE NA MANAIBU KATIBU WAKUU WATANO WAPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbali mbali.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu wawili.
Kwa mujibu wa uteuzi huo,

Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Aidha, kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ndugu Zidikheri M. Mundeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Wengine walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Walioteuliwa kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa ni Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Katibu Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Naibu Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya kutoka Wizara ya Uchukuzi na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Wateuliwa hao wote wataapishwa asubuhi ya leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es Salaam.

Allah atusaidie.
 
Back
Top Bottom