Rais kuitwa mtukufu na kuabudiwa hadharani bila kukemea inaashiria nini?


Wasiojiweza ndio hupenda kujikweza na kukwezwa na wasiojiweza.
Barikiwa ndugu.
 
Nijuavyo mimi hata kama si mjuzi sana wa mambo ya dini lakini mwenye cheo cha utukufu ni Mungu pekee si binadamu mwenye nyama,


Siyo kweli, Utukufu ni cheo anachoweza kuitwa/ kupewa mtu pia, na siyo utukufu tu bali pia kuna vyeo vingine anavyoweza kuitwa mtu na hapo hapo Mungu akawa navyo, mfano Ukuu nk ni cheo anachoweza kupewa mtu lakini pia Mungu ila tifauti ni hii kwa upande wa Mungu vyeo vyake vinayohadhi kubwa sana isiyoisha wala kupimika kinyume na binadamu vyeo hivyo vinaweza kupungua na kuisha na vinaweza kulinganishwa/kupimwa kati ya binadamu mmoja na mwingine, hiyo ndiyo maana ya maneno; "na tuumbe mtu kwa mfano wetu" au "tujipake rangi ya Allah"--- maneno "mfano' na "rangi" katika hayo maandiko ya Mungu ni sifa za Mungu ambazo binadamu anaweza kuziiga, kujifunza na kuzitekeleza katika upeo wake wa kibinadamu.
 
Nilisoma kisa cha Mtanzania mmoja aliyekuwa anaishi na kufundisha moja kati ya technical college huko Norway na alikuwa mkuu wa department ya Metallurgy. Rais Mkapa akawa ameenda kwenye ziara huko na alikuwa anapota hapo chuo, lengo mojawapo ilikuwa ni kumshawishi jamaa arudi ili kuanzisha hiyo department hapa UD.

Bahati mbaya sana jamaa aliondoka Tanzania wakati wa Mwinyi. Wamekutana na Mkapa akamuita "mtukufu Rais". Jamaa anasema Mkapa alikasirika vibaya mno. Meeting ikavurugika, hakuna kilichoongelewa, na plan nzima za kumshawishi kurudi kwa hiyo kazi zikawa zimeishia hapo.
 
Maswali ya kitoto
 
Kwa hili tuwe fair..Marais Nyerere na Mwinyi waliitwa hivi pia bila kuzuia. Ni Rais Mkapa ndiye aliyekuja kukataa kuitwa hivyo. Naandika hivi kwa lengo la kuweka historia sawa tu.
Nyerere hakuwahi kuukubali ujinga huo. Ndiyo maana aliitwa "NDUGU" Rais . Neno mheshimiwa limekuja wakati wa Mwinyi na kuendelea crocodile
 
Mtoa post hujawahi ona MAJALIWA akipita huyu jamaa mbele yake huinua had mikono kuonesha utukufu wa huyu kanjanja yaaan PM huinama kama yupo altare kabsa, inaleta simanzi sana.
Simanzi ya nini kunyenyekea ndo kumemfikisha hadi kuwa PM Endelea na ujeuri
 
Kwa hili tuwe fair..Marais Nyerere na Mwinyi waliitwa hivi pia bila kuzuia. Ni Rais Mkapa ndiye aliyekuja kukataa kuitwa hivyo. Naandika hivi kwa lengo la kuweka historia sawa tu.
Nyerere hakuwai kuitwa mtukufu, alikataa kabisa na akawa anasisitiza aitwe Mwalimu, rudi kwenye historia usome vizuri
 
Waafrika aliyeturoga hajafa, yupo hai na bado anakoroga dawa, na kutuchezea manyanga.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Utukufu,ni jinsi mtu atakavyo,sasa kwa jinsi jiwe anavyoobgoza nchi hii,ni mtukufu,na ili upate utakacho muite hivyo
 
Wafanye wawe masikini ili uwatawale.Kila ajaisujudiae na kukuabudu ataepuka njaa.
Ukisujudia na kuniangukia miguu pangu nitakupa fahari na miliki zote za dunia.Yesu akamwambia Shetani enenda zako imeandikwa msujudie Mola wako tu.
 
Wazee wa escrow wakianguka na kusujudu kwa unyenyekevu ndipo pilato atawarudishia uhuru wao.
 
Ndio mazingira alioyatengeneza kiongozi wetu.......kuogopwaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…