Tetesi: Rais kujichimbia Arusha neema ya Sukari inakuja . . .

Tetesi: Rais kujichimbia Arusha neema ya Sukari inakuja . . .

Huyu jamaa akiwa ziarani mikoani lazima kuna jipu limeiva.akirudi lazima alitumbue
 
Leo ni siku ya tatu tangu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli atinge mkoani Arusha, Kumekuwa na tetesi kuwa kuna papa lingine la sukari nchini ambalo limeweka maskani yake mkoani humo hivyo Rais Magufuli ameamua kulizukia na kulitumbua mwenyewe live ili kuwatumia taarifa mapapa wengine wadogo wadogo waachie bidhaa hiyo irudi sokoni . . .

Inasemekana Papa huyo wa sukari nchini alisomba tani za kutosha za bidhaa hiyo kutoka TPC moshi na kuipiga lock kwenye ghala lake lisilo kifani mkoani arusha, Hivyo basi simba wa vita Rais Magufuli amemtimbia huko huko Arusha ili akalale nae mbele na kurudisha bidhaa sokoni . . .
Umeandikama kama ongea ya Magufuli bila hiyana nami nikarudia kusoma kwa sauti ya Magufuli nikajikuta nacheka mwenyewe kama ambavyo huwa nacheka kwenye hotuba zake anavyo ongea! Hicho ni kipaji hongera
 
Swali la kujiuliza wewe mwerevu ni haki raisi wa nchi kumfuata muuzaji wa sukari awe mkubwa au mdogo kwa sababu amefungia tani kwa tani stoo kwake? Raisi wa nchi hawezi kutoa order akiwa kitandani kwake amelala na akasikilizwa especially kama anajua anachofanya ni sawa? Hizi ni dharau kwa kiongozi wa nchi, Eti anamfuata muuzaji wa sukari!!!!!!!!!!!

Atafuata wangapi? Leo hii watokee watu wabinafsi kama hawa wanaoficha sukari wakaficha chumvi je atawafungia safari?

Hayo ndio maswali machache mtu mwerevu angepaswa kujiuliza. Sio kushangilia drama na maigizo yasiyoisha ilhali mimi na wewe hatuoni unafuu wowote kwenye maisha yetu.

Wewe kuna mahali umemwona Rais amekwenda kwenye ghala la mtu? Yeye Kazi yake ni kutoa msimamo wa Serikali na kuagiza vyombo vya dola kuchukua hatua stahiki... Acha kupotosha kinacho fanyika . Kama yuko Arusha na akatoa tamko kuhusu mhujumu uchumi aliyeko Arusha haimaanishi yeye ndiyo anaenda kumkamata..! Au ulitaka arudi kwanza Dar ndiyo atoe tamko?!! Hamtashinda safari hii... Kaeni mkao wa kuchomwa sindano tu....
 
Distortion! Completely its unworth article
 
Swali ni je ni sawa yeye kufunga safari kumfuata muuzaji wa sukari? Ninavyofikiri angekuwa busy yeye na watendaji wengine kuhakikisha hiki kitu hakijirudii, sukari iliyofichwa ikiisha nini kitafuata......?
Hii ndio aina ya uongozi ya JPM, anasukuma mambo kwa nguvu hataki kuwa mtu wa kulala kitandani na kutoa order, Walishatokea viongozi wa kulala kitandani na kutoa order ila nini kilitokea . .???
 
King David of Tz. Hashindwi vita. Mungu ako mbele yake milele.
 
Kwa hiyo kama asingekuwa na safari ya arusha huyu muuzaji wa sukari asingetumbuliwa? Tuacheni utani, hii ni nchi haiongozwi kwa kutishana na maigizo. Mimi ni mtanzania mwenye uchungu, maisha yangu ya kuunga unga sindano nachomwa kila siku. Kinachofanywa na uongozi huu hadi sasa hakijaonyesha dalili ya kubadilisha maisha ya mtanzania wa hali ya chini. Huo ndio ukweli.
Wewe kuna mahali umemwona Rais amekwenda kwenye ghala la mtu? Yeye Kazi yake ni kutoa msimamo wa Serikali na kuagiza vyombo vya dola kuchukua hatua stahiki... Acha kupotosha kinacho fanyika . Kama yuko Arusha na akatoa tamko kuhusu mhujumu uchumi aliyeko Arusha haimaanishi yeye ndiyo anaenda kumkamata..! Au ulitaka arudi kwanza Dar ndiyo atoe tamko?!! Hamtashinda safari hii... Kaeni mkao wa kuchomwa sindano tu....
 
Unajua kuna watu wanafikiri JPM anafanya sinema au michezo ya kuigiza
Sisi Watanzania wazalendo tunamuunga mkono kwa nguvu zote mtetezi wa wanyonge
Baada ya kuzuia safari hizo tumeokoa mabilioni mengi ambayo yameingia kwenye budget ya 2016 2017 na ndo maana unaweza pesa nyingi zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo
Na bila kusahau mahakama ya mafisadi inakuja ambapo DPP atapeleka Mashauri yote ytasikilizwa... Kuna watu wakiona Rais anafanya juhudi wao roho zinawauma akati maendeleo ni kwa wote

Ivi katika historia ya marais wote mmewahi kuona Rais anazungumza mbele ya watu huku akionyesha hasira zake kwa mafisadi.... Uzuri ni kuwa mnaomtetea fisadi mkono wachache hivo hamfiki mbali sisi tuna songa mbele
Yaani akina Chenge eti?
 
Kwa hiyo kama asingekuwa na safari ya arusha huyu muuzaji wa sukari asingetumbuliwa? Tuacheni utani, hii ni nchi haiongozwi kwa kutishana na maigizo. Mimi ni mtanzania mwenye uchungu, maisha yangu ya kuunga unga sindano nachomwa kila siku. Kinachofanywa na uongozi huu hadi sasa hakijaonyesha dalili ya kubadilisha maisha ya mtanzania wa hali ya chini. Huo ndio ukweli.

Ulitegemea mabadiliko gani ndani ya miezi bila ya kusafisha kwanza uozo na kuwekana sawa...... Kama ulitegemea miujiza basi kaa kimya...
 
tumuombee rais wetu kama anavyotuomba kila siku, haya mambo yanarisk maisha yake sana.
 
Back
Top Bottom