Rais kuteua makada UVCCM kuwa Wakurugenzi ni kuvuruga Utumishi wa Umma

Hizi sasa ni dharau kwa watanzania hawajali tena ufanisi wala utaalamu.

Kesho utasikia semina elekezi kwa sababu ya makosa ya utendaji yanayofanywa na wakurugenzi wapya.

We are going in circles utopolo aliouweka Magufuli unaanza kupata experience leo wana badilisha kuleta makada wapya; the nonsense is too much.

Teuzi zenyewe kila zikija zinawalakini mara jina limepachikwa tu kama ilivyokuwa TPDC, kule kwa wakuu wa wilaya wakaboronga tena na sasa kuna watu wameteuliwa mara mbili.

Mwenye macho aambiwi tazama team ya mama ni ovyo na aipo makini aiwezekani kwenye kila teuzi ya majina mengi waboronge. Unadhani hawa watu wataweza mshauri vizuri kweli hii miezi minne washaporonga vya kutosha imagine ndani ya mwaka god forbid kuna watu wanafikiria huyo mama awe raisi hadi 2030 mungu wangu.
 
Sawa hayo ndio Majukumu lakini MUHIMU sio Hayo Uliyoyaorodhesha JUKUMU Muhimu kabisa ni KUHAKIKISHA CCM INASHINDA na HAKUNA MGOMBEA wa CHADEMA ANATANGAZWA hiyo ndio Sababu kubwa ya Kuwateua MAKADA na Sio Kuwaletea Wananchi Maendeleo
 
Sawa tu hadi 2030 mbona yule jamaa walitaka awe life president mipango ya mungu ikaamua sivyo
 
Reactions: Qwy
Haya ya kupandisha walishayaacha siku nyingi
 
.
 
Sijui majaji waliona ni sawa hawa maDED kuendelea kusimamia chaguzi wanajisikiaje? Watu ambao jana walikuwa wanahamasisha upinzani ufe, kesho ndio wakasimamie uchaguzi!!

Hii nchi kuja kuitoa CCM ni mpaka vita tu, kwa sanduku la kula haitawezekana.
 
Hapana..katiba sio mwisho wa matatizo..unaweza kuja na katiba mpya na bado watu wakaikanyaga pia..jambo la msingi ni kuchagua watu wenye weledi
Utachaguaje watu wenye weledi wakati walio madarakani kwa katiba iliyopo wana nguvu ya kuwaweka wawatakao na hata wao wenyewe kwa kutumia dola wakawa madarakani!?. Kwa katiba hii, mkuu sahau kuwapata hao unaowaita wenye weledi. Wabunge walioko bungeni sasa, waliopitisha sheria zinazopigiwa kelele, walichaguliwa na nani?
 
Sawa tu hadi 2030 mbona yule jamaa walitaka awe life president mipango ya mungu ikaamua sivyo
Watu washajiandaa kupiga mwambie CAG aende kagua ni watu wangapi walirudisha stimulus package ya JK ule ndio ulikuwa ufusadi karne mchana kweupe.

Leo wanakuja na mikopo rahisi ya 1 trillion kwa wakulima good idea but on the mix BoT pia imelegeza masharti ya kufungua biashara ya kibenki i.e reserve na competence skills requirements.

Sasa hivi kuna watu wataanzisha bank kwa sababu ya kupata hela za kukopesha wakulima na hizo bank zitapotea kama zilivyoanzishwa wakati poyoyo kama wewe huko busy kuchangia majukwaa ya JF kusini huko wenzako wanakomba hela za walipa kodi.

Kama nawaona wahasibu wa halmashauri wanavyochekelea hizi teuzi.
 
Com ishajichokea
 
2 August 2021

Waziri wa TAMISEMI Mh. Ummy Mwalimu atoa ufafanuzi wa ma - DED 184 waliotangazwa:
  • 45 wanaendelea kuwepo ktk vituo vyao
  • 70 wamehamishwa vituo
  • 69 ni wapya nao wamechukua nafasi 15 zilizokuwa wazi huku 54 wamechukua nafasi za waliotenguliwa
Wale 54 walitumbuliwa wataendelea na majukumu ya utumishi wa umma kama sheria za utumishi zinavyosema kwamba kutumbuliwa si kufukuzwa kazi bali wameondolewa ktk nafasi zao hivyo watapangiwa kazi zingine.

Mh. Ummy Mwalimu amesema Serikali kuanda semina elekeze maalumu kwa ajili ya ma-DED ili waweze kutekeleza majukumu yao kazini kwa ufanisi bila migongano na watumishi wengine pia kuwatumikia wananchi ktk maeneo yao.
Source DarMpya TV
 
Kiutaratibu ilikua wanapandisha vyeo kwa aliyekua Muhasibu wa halmashauri (DT)/Mchumi wa halmashauri/Afisa mipango wa halmashauri/Afisa utumishi wa halmashauri (DHRO) au mwanasheria wa halmashauri

Ila toka 2015 tukaanza kudemka
Mama kaamua kufuata trend ya awamu ya tano. Sasa imagine, CD kada, Mkurungezi kada sasa hapo nafikiri Wilaya zitaanza kuongozwa na Wenyeviti na Makatibu wa CCM.
 
Nadhani Wakurugenzi wangekuwa wanapromotiwa wakuu wa Idara,kwa mfano Mchumi/Afisa Mipango,Ustawi,Elimu,nk kuliko kuteua mtu from nowhere
 
Hako cha juu kabisa kamefikisha miaka 18? anyway kwa record zake sitashangaa huyu Rais akimpa ajira under age.

Tuseme ukweli tu, Samia amechoka sana akili ndio maana mambo yake mengi anakosea tu.
Tatizo siyo Rais Samia, ni washauri, wanaopendekeza na wanaomzunguka.
Ni lazima kuwe na succession plan nzuri kwa watumishi wa serikali.
Hawa walitakiwa waandaliwe kwa kupata uzoefu kwenye utumishi.
Madaraka yasiyo ya kisiasa moja kwa moja siyo zawadi inayoweza kutolewa hata kwa watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…