Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Tatizo lako wewe uelewi hata kwanini serikali inafanya aina fulani za investment.

Serikali inajukumu la kugharamia ‘merit goods’ maana yake nini serikali isiposomesha, kujenga shule, kutoa huduma za afya na uwekezaji mwingine wenye faida za jamii watakaofaidika ni wachache wenye hela.

Sasa serikali imekusomesha kwa faida ya jamii maana yeye ndio mtoaji huduma pia kwa watanzania maskini tulio wengi.

Mtu anatakiwa akaitumikie jamii ambayo inamuhitaji kama sababu za kusomeshwa kwake na kupewa experience. Anafika huko anaona hakufai sijui amepewa offer yenye maslahi mapana zaidi yule aliyekutengeneza unamuona fala.

Na unadhani Drs are entitled to that wakati kupata replacement yake ni shida.

Magufuli yupo right hapa huyo daktari ateme hela ya serikali tena anaondoka bila ya kujali kama kuna mtu wa-ku replace nafasi; halafu mnataka achekewe.
 
This man is mad
Amekuwa mwenda wazimu kwa kutaka tu kanuni zifuatwe? Nimeeleza kanuni husika katika Uzi Na. 25. Mimi mwenyewe nilisomeshwa na serikali mpaka shahada ya kwanza na kwa masomo ya juu zaidi nilisomeshwa na Umoja wa Mataifa. Mfadhiri wangu huyo alisisitiza nitie sahihi mkataba kwamba baada ya kuhitimu nirudi nchini kwangu na kufanya kazi nitakapopangiwa na serikali kwa kipindi kisichopungua miaka mitano. Vivyo hivyo na wenzangu waliofadhiriwa na mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali. Sasa yote hayo tuyaseme kuwa ni wenda wazimu?
 
Ukitenda dhambi kabla hujawa mchungaji, ukiwa mchungaji hutaacha kuikemea hiyo dhambi eti kwa kuwa na wewe uliwahi kuitenda???

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Hata hivyo kabakiza miaka minne tu achomoke.
 
Bwan na magufuli wako.
 
Inawezekana alipata Grant sio Mkopo... Grant kuna amsharti yake
Basi angesema kama huyo daktari alipata grant! Asikimbilie kusema tu tumekuwa mkopo 100%. Kwani ukinipa mkopo lazima nifanye kazi serikalini? Huyu mzee aache unyanyasaji wa kijinga wa Kisukuma! Maana unaponipa mkopo ni sawa na nimejisomesha mwenyewe maana hiyo ni pesa nitakayoilipa, ni sawa tu na serikali inapokopa hela Ulaya halafu inatutangazia kwamba tunajenga kwa fedha zetu?
 
Hospital binafsi pia anatibu watanzania wale wale.Kwani hospital binafsi anatibu warundi? Bado anatumika kwa wale wale waliomsomesha.
 
Huyu kabakiza miaka minne tu, achomoke tuvute subila tu
 
Wewe nawe,, unaweza kutuwekea hiyo kanuni hapa? Kwa nini mnapendaga kutetea ujinga? Hilo la kufanya kazi serikalini au kwenye shirika la umma ilikuwa enzi za zamani wakati wasomi wakiwa wachache! Halafu kumbuka wakati huo watu walikuwa wanasoma bure!
 
Na mm naunga mkono arudi ale vumbi la chaki [emoji1787][emoji1787][emoji1787], sihami Tanzania raha tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…