Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Mimi natoa pole kwa Majaliwa (PM), Kijazi(KMK), Samia(VP) na Diwani(DGIS). Poleni sana kwa majukumu mazito ya kulitumikia Taifa.
 
Nafikiri kabla ya kutoa hukumu, swali tujiulize daktari huyu amekua akilipa mkopo? ama la.... tatizo la WTZ baadhi yetu hukimbilia kulaumu kama ya kujua route cause, mpaka mheshimiwa anatoa tamko hilo huwezi jua , huenda ana data zake zote sometimes busara itumike badala ya kukimbilia ku point finger.
Kama halipi mkopo na anafahamika alipo hapo kosa ni la nani?
 
Kuna madaktari na manesi walipata shavu huko uk na australia alafu bonge la shavu,sasa walitaka barua toka wizara ya afya hapo sasa zengwe lake [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Tabora ni mji mdogo Mimi naona ndicho kilichomponza jamaa na hasa kwa wasomi kama yeye, huko ndiko waalimu , madaktari , wanasheria, mahakimu , polisi bado they command authority,

Sasa mfano akaondoka mtu kama huyo anacause chaos hapo alipotoka kwa maana kwamba anavuruga kabisa utendaji kazi wa eneo alikotoka. Sasa hii inavyoonekana ilileta shida.

Ila maeneo kama dar au kwingineko akiondoka mtu hata huwezi feel the pinch maana replacement inakua immediately.

Vijana wenyewe wakipewa kazi hawataki kwenda maeneo kama hayo, kisa watapoteza ramani.

Rais sio wakulaumiwa wakati mwingine, it's the system we established.

We need to change.
 
Kusomea udaktari kunaanza na uwezo na utashi wa mtu.

Daktari kugharamiwa masomo na serikali na hata kupata ujuzi kwenye hospitali za serikali haina maana kuwa serikali inaweza kujipa hatimiliki juu ya akili( na mwili) za huyo daktari na hii ni kwa taaluma na fani nyingine zozote.

Inaonekana wazi serikali ya Tanzania ya awamu hii inataka sana kutawala akili za wananchi wake wote.

Hilo ni jambo ambalo halitawezekana.

Say no to moratorium on brains.
 
Uonezi

Alikopa, analipa riba ya mkopo,
Na KWA dunia ya leo huwezi kumkataza asitafute sehem yenye maslahi mazuri et uzalendo ,so far bado wanaohudumiwa ni watz,
Kama ndo hivyo wabunge wate,mawazari ,wakaludi kwenye kazi zao why pro kabudi,BASHIRU, n.k wameacha kazi zao wameenda kwenye siasa?? Nao sio wazalendo?
Why jpm mwenyewe alikua mwalim,akaenda ubunge,then amekua waziri Mara kadhaa,kabla ya kua rais,KWA nini hakukataa, Kama sio kutafuta nafasi nzuri zaidi so naye sio mzalendo?, Jpm mh Sana hachana na haya Mambo?
Mbona mpaka mda huu wapo waliokua wakuu wa wilaya wanaenda gombea ubunge,na wengine wabunge,watumue Basi wamefata nini huko?maana nao sio wazalendo!
Mr dactari Kama hupo hum be strong ,huu ni uonevyo, unaweza fanya kazi nchi yoyote sio lazima tz ,pita chocho lala zako mbele,tz Kama wanajua umuhim wenu hasa serikali wakatoe stahiki zenu mnazostahili,sio vitisho,uzalendo ,uzalendo so what Kama mtu ashibi
Rais Magufuli leo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma?, hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”-JPM
“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”-JPM

My take.
Kuna maslahi madogo hasa ya kimshahara katika utumishi wa serikalini, naomba serikali iongeze mishahara kwa watumishi ili kuepukana na changamoto hii. La sivyo serikali itaendelea kupoteza mapato kwa watu kukimbia utumishi wa umma serikalini.
 
Kwani huyo daktari amekimbia fani ya udaktari, au amehama tu toka kutibu kwenye sekta ya umma, na kwenda kutibu kutibu watanzania kupitia sekta binafsi? Ingekuwa kahama nchi na hataki kutibu watanzania hapo wangalau. Ulevi wa madaraka ni tatizo.
Daktari amemkimbia aliyemgharamia elimu, hata kama alipewa mkopo 100% na bodi ya mikopo bado serikali inamchango mkubwa kwenye elimu yake
 
Hii nchi tunakoelekea ni kubaya zaidi.

Huyu mwalimu wa science tena kipindi kile walimu wa science shule za vijijini walikuwa wachache sana ila aliamua kuacha wanafunzi na kugombea ubunge. Masilai ya ualimu aliona ni kidogo. Ubunge wenyewe aligombea awamu mbili bila kufanikiwa.

Hayati Benjamini william Mkapa ndyo akampa support baada ya kuitenga chato ndipo Rais JPM alifanikiwa kuwa mbunge.

Leo hii daktari wa serikali kaacha kuwa mtumishi wa serikali na kaenda kufungua hospitali binafsi ambayo imeongeza huduma katika jamii ila Rais Magufuli kwa Roho ya kwanini anataka awaingize matatani.

Nakumbuka Rais mstaaf J. Kikwete aliwahi kuzungumza juu ya katiba inavyompa Rais nguvu kubwa na hivyo inahitaji busara sana kuendesha nchi kama Tanzania.

Kusema ukweli hii busara magufuli hana kabisa. Na waliopo karibu naye wanashindwa kmweleza ukweli ilimradi vibarua vyao visiote nyasi au wanasubiri aboronge ili akiondoka wamsengenye.
Mkuu, pia alishawahi kunukuliwa na vyombo vya habari akiwaambia watumishi wa umma wanaonung'unika kwa kutokuongezewa mshahara toka awamu ya tano ilipooingia madarakani. Na akasema yule asiyeridhika na aache kazi.

Leo kibao kimewageukia tena wale ambao hawakuridhika na kuchukua hatua. Kauli hizi tata na zenye kukinzana na msimamo wa awali uliotolewa na serikali yenyewe zitazidi kutolewa mpaka lini?
 
Kwani huyo daktari amekimbia fani ya udaktari, au amehama tu toka kutibu kwenye sekta ya umma, na kwenda kutibu kutibu watanzania kupitia sekta binafsi? Ingekuwa kahama nchi na hataki kutibu watanzania hapo wangalau. Ulevi wa madaraka ni tatizo.
Daktari amemkimbia aliyemgharamia elimu, hata kama alipewa mkopo 100% na bodi ya mikopo bado serikali inamchango mkubwa kwenye elimu yake
Angeaga kwa uzuri yote hayo yasingetokea
 
Back
Top Bottom