Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli leo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma?, hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”-JPM
“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”-JPM

My take.
Kuna maslahi madogo hasa ya kimshahara katika utumishi wa serikalini, naomba serikali iongeze mishahara kwa watumishi ili kuepukana na changamoto hii. La sivyo serikali itaendelea kupoteza mapato kwa watu kukimbia utumishi wa umma serikalini.
Umehitimisha vizuri sana mkuu
 
Wakutosha kusambaza kwenye hospitali zote zenye sifa ya kuwa na bingwa, huwezi kupelekwa bingwa mahali pasipo na vifaa tiba muhimu
They also need to work and live in an environment which raises their morale, hilo nalo ni muhimu.
 
Private Sector Acheni Kuajiri Madaktari waliosomeshwa Kwa Mkopo Maana Hamjui wametoka Wapiii hospital Zenu Zisije Zikafungiwaa.
 
Anatafuta Daktari aliyekimbia hospitali kufuata masilah na mazingira bora ya kazi

Anayetoa maagizo yeye pia alikimbia ualimu na kwenda kuwa mkemia kwa kufuata masilah Mazuri, licha ya kusomeshwa na Serikali buree bila hata kurejesha shilingi huku hata nauli na Mikate wakipewa buree.

Mtoa maagizo hajaridhika hapo akaacha ukemia akaingia kwenye siasa kula kwa mrija sasa, amesahau alipotoka. HAPO NANI NI MZALENDO?
 
Hapo mnamlipa 1.4 anakatwa makato mpaka bima take home 500,000 leo hospital binafsi 4m na mkopo analipa sasa shida yake nini
Ingekuwa amesomeshwa bure sawa Mkopo duuu naomba tuwe tunamwandikia JPM hotuba
 
Anatafuta Dr. aliyekimbia hospital kufuata masilah na mazingira bora ya kazi,anayetoa maagizo yeye pia alikimbia ualimu na kwenda kuwa mkemia kwa kufuata masilah Mazur, licha ya kusomeshwa na serikali buree bila hata kurejesha sh. huku hata nauli na MIKATE wakipewa buree.Mtoa maagizo hajaridhika hapo akaacha ukemia akaingia kwenye siasa kula kwa mrija Sasa, amesahau alipotoka. HAPO NANI NI MZALENDO?

JPM bado ni mtumishi wa umma, amehama idara tuu hajaenda ACT 😂😂😂
Mtumishi namba1 wa serikali
 
Serikali ingekuwa haijui umuhimu wake ingemsomesha bure?

Nchi inatumia tsh 700 billion kwa mwezi kulipa mishahara tu ya wafanyakazi, serikali hiyo hiyo iwatafutie vifaa tiba na majengo; ni hivi karibuni tu ndio imekuja na bima kujitua baadhi ya mzigo.

Hizo hela mnazotaka watu waongezewe kila siku au ajira mpya zitengenezwe, mnataka funds zitoke wapi? Wakati huo huo amtaki watu wadaiwe kodi.

Kuna taaluma wakubali ni wito, kama unataka kufanya kazi private as M.D wajisomeshe wenyewe basi na waende huko huko private kutafuta practice experience. Lakini uitumie serikali kuvuka daraja ukishafika ulipokusudia uanze ngebe hilo hapana.

The government made them they need to show respect and be loyal..
Aiseeee. Mbona mkubwa wako anajidai kwa kauli zake za hii nchi ni tajiri! Mkuu wakati wanaomba kuchaguliwa kipindi cha kampeni si husikika wakisema tunaongea yaliyoandikwa kwenye ilani ya chama chao? Kuhusu mapato nakupinga, kwan kila siku yanakusanywa, tena wanakusanya na mapato kwa watu ambao kwa akil ya kawaida hustahili kuwaomba kodi. Alafu hizo hela tunazotoa kwenye kodi zetu ndo hizo mtu anaenda nazo chato, ndo hizo mtu anafanyia miradi ambayo inatuumiza, miradi ambayo watesi wake waliipga posp coz walitambua watu lzm waumie. Ko lengo la jamaa n kutuumiza kwa mgongo wa mkopo kipind tunasoma? Alafu mkopo ile ni biashara ya kinyonyaji, sitaki tuingie huko mana huko ndo wanatunyonya waz waz. Moreover mkopo hatukupewa bureeee. Alafu mkopo unalipwa, so hasara iko wapi?
Hivi zisingekuwepo hizo hospital za private serikali ingeweza kuhudumia watu vzr kweli?
Na mshukuru hizo hospital zinasaidia kupumguza idadi ya unemployed doctors na manesi wengi.

Muwe mnajua na kushukuru nyinyi nyang'au
 
Sipati picha jinsi wananchi walivyokuwa wanashangilia baada ya kusikia hii kauli kiukweli wanasiasa wengi peponi watapita hiviii subirini tu muda utaongea
 
Back
Top Bottom