Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Kule hawatibu watu ?

Wanadaiwa ?, Wamelipa hawajalipa ?, kuliko kufungia hospital / mtu anayetibu watu pia ni rahisi sana kwenye mkataba wa mkopo waseme kwa miaka kadhaa lazima ufanye kazi ya serikali sehemu yoyote utakayopelekwa (hapo mtu anakuwa anabanwa kwa mkataba) sio aina hii ya sheria / maamuzi kutoka kwenye kinywa cha mtu
Nanuonea huruma huyu daktari. Imagine kama angekuwa amejwenda nje ya nchi.... Nafikiri ingemlazimu abaki huko huko mpaka Jamaa atoke madarakani.
 
Ye mbona aliacha ualimu si angeendelea kukomaa hapo kwenye ualimu,wenzie kutafta riziki imekuwa shda,nawatuma jamaa zake kamwambieni tumechoka drama zake
Narudia tena nakemea kitendo cha raisi kuingilia maisha binafsi ya watu
 
Sijawahi ajiriwa ko sijui. Kitaani ili uache kaz ya utumishi wa umma bila longo longo n inabidi uwe mtovu wa nidhamu, wakikupa warning ya mdomo, unarudia kosa, wanakupa warning ya makaratasi tena unarudia kosa lilie lile, wanakupa suspension ya miez kadhaaa😆 ukirud job tena unarudia kosa lile lileeeee, hapa wanakufukuza kazi kilainiiii na unapewa stahiki zako vzr😆 unafanya mishe zingne. Ko sijui kama utaratibu wa kuacha kaz upoje but kuna muda ukitaka kufwata utaratibu unacheleweshwa sanaaa na hapa ndipo tunatumia kale kakauli ka SHERIA ZIMEWEKWA ILI ZIVUNJWE😆, unaweza ukawa unaandika barua hazijibiwi, sasa what next😅😅😅
Sheria zimewekwa ili watakaozivunja washughulikiwe
😂😂😂😂😂😂
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
Not Fair at all, labda kama halipi mkopo wake, so wapo madakitari wengi wanazungusha CV zao maofisini kutafuta kazi wawape hiyo kazi. Kwamba mtu akiajiliwa serikalini kama kasomeshwa na serikali hapashwi kuacha kazi hata kama masilahi kiduchu, mbona watu wanaacha kazi ya uwalimu na kuomba ubunge. Professional wangapi wameacha kazi serikalini na kujiajiri.
 
Mamaee 100 tena mpaka mkome nyie misukule wa lumumba , maana hivyo vichwa ngumu havielewi , mnawekwa wendawazimu kama huyo madarakani halafu mnaoropoka kama nguruwe anajamba
 
Kila mtu anangalia maslahi yake
Mtu kapata connection nzuri unafikiri atabaki hapo anapolipwa laki 3
Mbona wao wanasiasa wanajilipa mihela kibao

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Kuondoka sio shida, shida ni je, alifata taratibu za utumishi na maadili ya kazi yake?
 
Mkuu kumbuka huo mkopo sio kila mdaiwa anarejesha cash yeye binafsi. Sheria inamtaka mwajiri kukata kutoka mshahara wa mtumishi na kuremit serikalini. Hivyo hapa tuna hakika kama huyu dr. alikua na mkopo then alikua anarejesha accordingly.
 
Kwani akiwa huko hospitali binafsi, si anarejesha mkopo!? Ama mimi ndiye nimeingia kwenye uwanja wa mpira na shoka!!!
====
Kuna uwezekano mkubwa Rais amenukuliwa vibaya, ngoja nitafute chanzo halisi.

Yani mzee karopoka mpaka wasifiaji hamuamini kama ni yeye kaongea huo ujinga.

Mmeishia kusema kanukuliwa vibaya Kazi ipo!!
 
Mengine watu washaongea uwezi kwenda kufungua hospitali kubwa kila sehemu, kuna maeneo hayana motisha kwa wafanyakazi kuishi hasa medical consultants.

Binafsi nimetabiri hospitali inayojengwa Chato itashushwa hadhi soon as Magufuli leaves office, kwa sababu Chato sio sehemu ya kuweka consultants.

Ni bora waiongeze ukubwa hospitali ya Geita mjini ije kuwa ya kanda the area as the right population density na ni mji mkubwa. Lakini Chato bora wajikite na hospitali ya wilaya I do not see senior consultants wenye demand kubwa ulimwenguni kuishi Chato.
Wataishi Kwa lazima. Watake wasitake.
Hapa ndipo tulipofikia.
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
Mitano tena
 
Back
Top Bottom