Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

View attachment 1690117

Huyo ni government employer kama wizara ya afya kwetu, kwanini unadhani ata huko kwao awachukulii poa watu kuondoka kiholela?

Jioni njema, time for my evening walk.
Kama wamesaini hii contract hakukuwa na haja ya kukimbia ,

Simply angefuata taratibu za kuuvunja huu mkataba.
 
Taarifa imeshatolewa katika ziara ya Mh.Rais leo Tabora .haiwezekani serikali ikukopeshe Ada halafu ukishapata ajira unahamia kwenye maslahi zaidi. Hii haikubaliki .kwahiyo mlioko serikalini na mtakaoapata Ajira mpya za serikali mkae mkilitambua hilo.

Ukiingia umeingia Hakuna kutoka

Nawasilisha.
NIKUKOSA UZALENDOO. MADAKTARI HAWA WAMESOMA KWA KODI ZA LALA HOI WAUZA MAHINDI NA NAMAHARAGWE, HALAFU MNAWAKIMBIA WALIOWAWEZESHAA?? KUNA LAAANA ITAFUATA JUUU YAO
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
View attachment 1689964View attachment 1689965

Huyu mzee ana shida huko upstairs...

Kwani huko walikoajiriwa na hospitali binafsi wameenda kutibu ng'ombe au binadamu hao hao tena Watanzania...?

Unless niwe sijamwelewa au aliyeriooti awe amepotosha. Lakini kama ndivyo hivi, hakuna shaka basi kuwa, Magufuli ana akili za ki - Trump Trump....!!!
 
Hospital gani itakubali ku take risk ya kupigwa kufuli kwa kukuchukua Daktari toka serikalini?
Tahadhari gani?Kwani Magufuli ndiye sheria na katiba?Unaelewa kuwa nchi huwa inaongozwa kwa mujibu wa sheria?Daktari akihama kutoka serekalini kwenda sector binafsi amevunja sheria gani?Nikikuita kuwa wewe ni punguani nitakuwa nimekuonea?
 
Nenda sasa uone kitakachokupata.
 
Hili Rungu la JPM lingehamia kwa watumishi wote wa Umma wakiosomeshwa kwa Mkopo Marufuku kuhamia Private ili Madaktari wasidhan wanafanyiwa hivyo wao pekee
NIKUKOSA UZALENDOO. MADAKTARI HAWA WAMESOMA KWA KODI ZA LALA HOI WAUZA MAHINDI NA NAMAHARAGWE, HALAFU MNAWAKIMBIA WALIOWAWEZESHAA?? KUNA LAAANA ITAFUATA JUUU YAO
 
Wa Mtaani ambao hawana ajira kabisa, mbona wapo wengi

Ni Sawa na kung'ang'ania kurubuni Mke wangu wakati kama Yeye wapo wengi tu mtaani

Ifike hatua Private waweke kigezo cha kutoajiri mtu yeyote aliwahi kufanya kazi serikalini ili wasikwazane na Mamlaka z nchi
Sasa hospital hizo zichukue madaktari kutoka wapi?
 
Hili Rungu la JPM lingehamia kwa watumishi wote wa Umma wakiosomeshwa kwa Mkopo Marufuku kuhamia Private ili Madaktari wasidhan wanafanyiwa hivyo wao pekee
Ajira ni popotee. Kilichomgarimu dactari huyo nikuacha ajira ya serikali na kuwatelekeza rai wanaostahili huduma yake na kukimbilia private.
 
Hii ni thinking ya ajabu sana! Yaani kwa sababu mmempa mkopo 100% ndio haruhusiwi kutafuta kazi yenye maslahi zaidi? Kwani huo mkopo si analipa? Au mikopo wanalipa waliojiriwa serikalini tu?

Huyu Mzee hopeless sana...

Anasema;

"....madaktari hao na hospitali zinazowarubuni watoke katika hospitali za serikali kwa kisingizio cha maslahi zifuatiliwe...."

Kauli ya "zifuatiliwe" maana yake zimefanya makosa kuwaajili madaktari hao na kwa hiyo hatua kali zichukuliwe dhidi ya hospitali hizo..!

Kauli ya namna hii toka kwa Rais Wa nchi inashangaza sana. Badala ashukuru kuwa sekta binafsi inasaidia serikali kuajiri watu wake, yeye anatoa kauli za ajabu ajabu zilizo na harufu ya u - siasa siasa tu kwa ishu serious kama ajira na maslahi ya watu...

After all madaktari mitaani wako kibao. Kwani serikali isiajiri hao?

By the way huko walikoenda hawa madaktari (hospitali binafsi) nako wameenda kuhudumia watu, Watanzania hawahawa. Sasa sijui shida iko wapi...
 
Taarifa imeshatolewa katika ziara ya Mh.Rais leo Tabora .haiwezekani serikali ikukopeshe Ada halafu ukishapata ajira unahamia kwenye maslahi zaidi. Hii haikubaliki .kwahiyo mlioko serikalini na mtakaoapata Ajira mpya za serikali mkae mkilitambua hilo.

Ukiingia umeingia Hakuna kutoka

Nawasilisha.
Samahani jamani mi sielewi kwani madaktari hawahusiki na makato ya HELSB

Naomba kufahamishwa tafadhali
 
NIKUKOSA UZALENDOO. MADAKTARI HAWA WAMESOMA KWA KODI ZA LALA HOI WAUZA MAHINDI NA NAMAHARAGWE, HALAFU MNAWAKIMBIA WALIOWAWEZESHAA?? KUNA LAAANA ITAFUATA JUUU YAO
Kwani akiwa hospital ya private hawahudumii hao wauza mahindi na je kodi na huo mkopo akiwa huko private halipi? Akili zingine aiseeee!!!!!
 
Kwani akiwa hospital ya private hawahudumii hao wauza mahindi na je kodi na huo mkopo akiwa huko private halipi? Akili zingine aiseeee!!!!!
Hivi hizo garama za hispitali za private hao walalahoi waliomsomesha kwa kuuza mahindi na maharagwe wataweza kumudu garama zile?? Yeye daktari yule aliyeajiriwa kwenye hospitali zetu walalahoi, amalize mkataba wetu ili tunufaike tuliomsomesha, kisha akatafute hizo hospitali, ambazo kumuona daktari na lakimoja hukubado hujalipa vipimo na dawa zakee
 
Back
Top Bottom