Rais Magufuli aagiza Wajumbe wa NEC kusafiri bure na ndege ya ATCL iliyokuwa inashikiliwa Canada bure kurejea Dar es Salaam

Rais Magufuli aagiza Wajumbe wa NEC kusafiri bure na ndege ya ATCL iliyokuwa inashikiliwa Canada bure kurejea Dar es Salaam

Hilo hawalijui zaidi ya masifa
Imetoka huko ilikotoka ikiwa tupu, kwa sababu inapelekwa kwenye kituo chake, Mapokezi yake kufanyika Mwanza siyo sababu ya kuifanya ibebe abiria kabla ya ratiba yake ya kibiashara kupangwa. Hao wajumbe wa NEC wangeisaidia ATCL vizuri zaidi kwa kulipia nauri ya kurudi Dar na Zanzibar kwa ndege nyingine iliyoko kwenye ratiba ya kibiashara.

Ukisikia biashara zinayumba na baadaye kufa, sababu kuu ni mambo yanayoonekana madogo madogo kama haya. Vipi ikipata ajali na hao wajumbe wakiwemo ikiwa kwenye safari ya kuelekea kituoni ... Gharama za bima kwa vyovyote haziwezi kuwahusu hawa wajumbe zaidi ya marubani na fundi mmoja aliyetajwa. Umakini unahitajika kwenye hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ccm lolote linawezekana maana wana jiona kama miungu
Barafu please come out to clarify this, ndege inaweza kubeba abiria kabla ya kupata certification/authorization from the local aviation authority?
Commercial aircraft inaweza kubeba abiria bila kuwa na insurance?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo hawalijui zaidi ya masifa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi naamini kauli iliyotolewa ni ya utani wa kisiasa tu. Mambo ya namna hii kwenye usafiri wa anga hutokea sana Nigeria na DRC ambapo ndege zinaruka bila kudhibitiwa mienendo yake na mamlaka za anga ambazo ni dhaifu!... Kila uchwao utasikia ndege ya mizigo imeanguka na kuua abiria kibao.

Tanzania ina mamlaka zinazosimamia sheria za usafiri wa anga na ni lazima zihakikishe sheria zinafuatwa kama tunataka kuibadilisha nchi hii kuwa kwenye kundi la nchi zilizoendelea. Chukulia kwa mfano, magari yanayoshushwa bandarini na kisha kuendeshwa kwenye barabara zetu kwenda nchi jirani, kwa nini yasiruhusiwe kubeba abiria? ... Kuna sheria na taratibu...zizingatiwe!.
 
Hakika hilo jambo halipo mbali na hakika litatokea

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu sisi tutatmia zile za kenya, South Africa, Rwanda na Uganda! mawazo ya kipumbavu kweli. Wapinzani watapiga kelele nchi imeshindwa kununua hata ndege moja kama walivyopiga makelele wakati JK, wakati mwingine ni vigumu kujua wapinzani na watanzania wanataka nini!
 
Sisi wajumbe wa nec ya ccm tumepewa shavu la kupanda ndege yetu mpya bureeeee kesho kutoka mwanza kwenda dsm na zenji maana tunatekeleza ilani ya chama chetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndege ya abiria 78 kwa ujinga wenu wajumbe Wa kwanza Wa NEC kupanda watakuwa wajumbe wa nec kutoka mikoa ya mwanza,geita,kagera,musoma,chato,kigoma,tabora,simiyu na burigi
 
Img-1576369309654.jpg


My Take:

Haya ni matumizi mabaya ya madaraka

Kutumia mali za umma kisiasa siyo afya kwa Taifa.

CCM wanapokea ruzuku, kama wanahitaji usafiri, walipie

Kuingilia utendaji kazi wa mashirika ya umma kwa kutoa decree ya kuamua tu shirika lihudumie makada haina tofauti na mapedeshee watoa ofa za "huyu mupe yule muruke" ni business model ya ajabu isiyoweza kutufikisha popote kama nchi!

Kutoheshimu kodi za wananchi kwa mtindo huu ni tatizo, tena ni tatizo kubwa.

Mnasema tunapambana na ufisadi eh?
 
Kuna mtu anahitajika kumkumbusha wazo la 'WANYOGE'.

Nina hakika hili akilipata tu, utasikia 'wanyonge' toka Dodoma wamepelekwa Serengeti kwa ndege yao mpya.

Yule mtu, ...sijui anaitwa nani yule 'Alumnum' au sijui 'Aluminium', yupo hapa?

Jameni, mwiteni haraka akafikishe ujumbe haraka.
 
View attachment 1292780

My Take:

Haya ni matumizi mabaya ya madaraka

Kutumia mali za umma kisiasa siyo afya kwa Taifa.

CCM wanapokea ruzuku, kama wanahitaji usafiri, walipie

Kuingilia utendaji kazi wa mashirika ya umma kwa kutoa decree ya kuamua tu shirika lihudumie makada haina tofauti na mapedeshee watoa ofa za "huyu mupe yule muruke" ni business model ya ajabu isiyoweza kutufikisha popote kama nchi!

Kutoheshimu kodi za wananchi kwa mtindo huu ni tatizo, tena ni tatizo kubwa.

Mnasema tunapambana na ufisadi eh?
Hivi mtazoea lini?

Samahani lakini mkuu Missile, lakini imenibidi maneno hayo niyaandike baada ya kuona hayo uliyoyaandika wewe kana kwamba ungetegemea unayemsema atastuka na kubadilika.

Jamaa tabia yake hii inamsaidia sana, maanake angekuwa ni wa kusikiliza yasemwayo, hali yake hadi wakati huu ingekuwa ni mbaya sana.

Yeye anajisikiliza mwenyewe, na akili yake inapompeleka, ndiko huko atakakokwenda bila kujali matokeo yake! Unazikumbuka korosho lakini? Kassim kabembeleza weee, lakini jamaa alishaona kuna 'popularity' ya bwerere kwa aliyoyaamua, bila ya kujua matokeo yatakuwaje.

Baada ya kuona uharibifu aliosababisha, akina Kabudi haraka haraka wakakimbilia kwa kampuni ya kitapeli ya Kenya ili kufuta matokeo mabaya ya uamzi wake ule.
 
[QUOTE = "sengobad, chapisho: 33783297, mwanachama: 448875"]
Kumbuka ipo ya majeshi !!!
[/ QUOTE]

UHUJUMU UCHUMI UNA KANUNI (formula)?
 
Route hiyo ni ya kutoka kiwandani kuja nchini ! All costs associated are part and parcel of procurement ! Biashara itaanza ikifika Dar, final delivery destination.
Ndege imeshapokelewa na watu wameshaenda Mubashara, unasema mpaka ifike Dsn ndipo inahesabika imefika kwenye kituo husika?
Kwani Mwanza sio Tanzania ambako ndiko ndege inapaswa iende (Tanzania)?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndege imeshapokelewa na watu wameshaenda Mubashara, unasema mpaka ifike Dsn ndipo inahesabika imefika kwenye kituo husika?
Kwani Mwanza sio Tanzania ambako ndiko ndege inapaswa iende (Tanzania)?

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kuropoka hovyo wewe ! I know for sure final destination ni JNIA ndipo inafanyiwa post delivery inspection kwenye hanger na officials and engineers wa Tanzania in the presence of officials wa kiwanda ! Kwanini wasiipeleke kigoma airport kupokelewa huko ?
 
Back
Top Bottom