Kwenye hili mzee John Pombe Magufuli, amesoma uelekeo wa upepo na kuona wazi kuwa utampeperusha na kumtupia shimoni......
Na upande wa pili tayari hasimu wake mkubwa kisiasa [aliyejaribu kum - assassinate mwaka 2017 kwa risasi za SMG ya kivita] akiwa ametangaza kupambana naye kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 kupitia chama kikuu cha upinzani - CHADEMA....
Honestly, amefanya vyema kuipiga pin kanuni hiyo ya kikokotoo na tunaweza kusema kwa hakika kuwa yuko ndani ya box la 18 akitafuta upenyo wa ku - shoot ili afunge goli.....
Upenyo wenyewe ni kufanikiwa tu kupiga chenga wachezaji wanne tu walio mbele yake kabla ya kuwa uso kwa uso na kipa na nyavu.....
Wachezaji wenyewe ni:
1. Nyongeza za mishahara
2. Promotions za kisheria za watumishi wa umma
3. Kulipa madai ya madeni mbalimbali ya watumishi wa umma na
4. Kufungua geti la auto - annual salary increaments za wafanyakazi wa umma
Na ili afunge goli la karne hili (na uwezo huo anao), basi hadi hatua hiyo atakuwa uso kwa uso na goli na kipa....
Sasa hapo, akiamua kupaisha, kwa kweli itakuwa ni shauri lake, sisi tutakuwa hatumo....!!