Rais akicheka siku ya mkesha wa mwaka mpya ni dalili njema kwa mwaka ujao wa 2020, utakuwa ni mwaka wa vicheko, tena kwa msiojua mambo ya kihabari, big names makes news, hivyo inapofikia hatua hata rais akicheka tuu ni news tena yenye catch line " Rais Magufuli Acheka!, haya ni maendeleo makubwa kwa sekta yetu ya habari.
Sisi wa zamani tangu enzi za Nyerere, Mwinyi, Mkapa na JK, enzi hizo Press Release ya Ikulu ikitoka ni something big credible na serious, rais alikuwa akienda kanisani/msikitini kusali/swali haijawahi kuwa news, siku hizi rais akienda kusali kanisani ni news tena ya press release!, sasa leo rais amecheka, press release!, this is a big development kwenye sekta yetu ya habari, natamani nishauri Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na timu ya Dr. Abasi wafanye ziara za kimafunzo kwa wenzetu waliotangulia, lakini sishauri ili tusiige mambo, tufanye yetukama ilivyo demokrasia yetu ya uchaguzi huru na wa haki, watu wamepita bila kupigwa hivyo watu hawakupiga kura, lakini matokeo ni ushindi wa asilimia 99.9% na watu tunashangilia ushindi wa kishindo!, hii ndio demokrasia yetu!.
P