Rais Magufuli afungua mkutano Mkuu wa Chama cha Waalimu, Corona imeisha, Shule za Msingi kufunguliwa karibuni

Kada ya ualimu si mbaya kama tunavyoendelea na mjadala huu naona vijana wengi wanaponda sana na kuwalaumu walimu ambao kimsingi hawana kosa lolote isipokuwa kosa ni mfumo tulionao, walimu hawa wanafanya kazi ktk mazingira magumu sana hasa kwa shule za serikali ambazo miundombinu yake kiuhalisia ni mibovu sana na kwa kweli kunahitajika juhudi si tu za ziada bali uamuzi wa dhati kabisa kuhakikisha kwamba mazingira ya kazi ya walimu yanaboreshwa vzr ili yaweze kuleta tija na kuongeza uthamani wa Elimu kwa ujumla.
 
Salaam Wakuu,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania-CWT.

Mkutano huo utafanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, huku watu wote wakitakiwa kuzingatia na kuchukua tahadhari za kujikinga na Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Tayari, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-Takukuru, Mkoa wa Dodoma, imetangaza kuwa itashughulika na watu watakaojihusisha na vitendo vya rushwa katika Uchaguzi huo.

Nitawaletea Updates kwa kila kitakachojiri.

Karibuni.

===
UPDATES:

Mkutano huu umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako, Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa mingine na viongozi wengine wengi.

Tayari M.h Rais Magufuli ameshawasili katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambaye tayari kwa ajili ya kuja kufungua Mkutano huu wa Chama cha Waalimu Tanzania ambapo amefika na kuwasalimia na kuwapungia mkono Waalimu wote waliohudhuria.

Wimbo wa Taifa unaimbwa kabla ya Rais kuketi na kufungua mkutano huu.

Kabla ya kukaribishwa Mh. Rais kuzungumza Mkutano huu umeanza kwa maombi kutoka kwa Sheikh na Mchungaji Davidi kalinga ambao wameanza kwa maombi kwa kumshukuru Mungu kisha kuomba amani na furaha katika mkutano huu pamoja na kumuombea Rais na viongozi wengine.

Katibu Mkuu wa chama cha Waalimu ameanza kwa kuzingatia itifaki na kuwatambulisha viongozi mbalimbali waliohudhuria katika Mkutano huu na kisha ameanza kusoma risala iliyoandaliwa.

Risala hii imeanza kwa kumshukuru Rais kwa kukubali kuwa Mgeni Rasmi mkutano huo kisha kumpongeza rais kwa miradi mbalimbali ambayo Rais ameitekeleza katika kipindi hiki cha miaka mitano, Katika sekta ya elimu Rais amepongezwa kwa kuongeza miundo pamoja na samani.

Aidha, katika suala la upandishaji wa mishahara na urekebishaji wa mishahara kwa Waalimu Mh. Rais amepongezwa kwa kuruhusu zoezi la upandishaji mishahara na vyeo kwa zoezi ambalo lilikwama kuanzia mwaka 2014 ambapo inaelezwa kuwa hadi kufikia tarahe moja June 2020 serikali ilikuwa imeongeza mishahara na kuwapandisha vyeo Waalimu wapatao 121, 534.

Aidha kuhusu malimbikozo ya madeni yasiyo ya mishahara Mh. Rais amepongezwa kuwa hadi kufikia December 2019 serikali anayoiongoza ilikuwa imelipa kiasi cha Tsh Bilioni 12.05. Huku malimbikizo ya mishahara yakilipwa.

Aidha, risala hiyo imebainisha changamoto ambazo waalimu wanakumbana nazo ikiwamo ukosefu wa nyumba za waalimu na pia rasala hiyo imemuomba rais kuwapandisha cheo waalimu kundi la waalimu walioajiriwa mwaka 2013/ 2014 wapandishwe cheo katika bajeti ya ya mwaka 2020/2021.

Sambamba na hilo, risala hiyo imemuomba Rais kuongeza ajira kwa waalimu ili kukabiliana na idadi kubwa ya Wanafunzi iliyotokana na kuwa elimu bure.

Zaidi ya hayo, waalimu wamemshukuru kwa tamko lake la kutia moyo ambapo aliwambia watumishi nchini wakiwamo waalimu kuwa ataendelea kulipa mishahara hata kama waalimu watakaa nyumbani kutokana na janga la Corona. Pia, Waalimu wamempongeza Raisi pamoja na Wizara ya Afya kutokana na hatua walizozichukua kupambana na Corona na kuwafanya Wananchi kuondokana na hofu ambayo ni mbaya kuliko Corona yenyewe.

Hotuba ya Rais wa Chama cha Waalimu (Bi. Leah Ulaya)
Ameanza kwa Kumshukuru Rais kutenga muda wake kuhudhuria tukio hilo kama Mgeni Rasmi pamoja na kumpongeza Rais kwa kuendelea kufanikisha na kuendeleza Sekta mbalimbali za kimaendeleo nchini.

Sambamba na hilo, Rais wa Chama cha Waalimu amempongeza Rais kuwa na uthubutu na kuweza kufanya mambo mengi makubwa ambayo wengine yanaonekana ni magumu.

Amekazia kwa kumshukuru Rais kwa upendo wake mkubwa kufuatia Rais kuruhusu Watumishi na Waalimu kuendelea kuwalipwa mishahara japokuwa zaidi ya miezi miwili hawakwenda kazini kutokana na janga la Corona.

Ameongeza kwa kumsifia Rais kwakuwa na Muadilifu, Mtu mwenye Upendo, jasiri, Mtu mwenye utashi, mvumilivu, Mchapakazi na mcha Mungu

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI
Rais ameanza kuwashukuru Vingozi wote kwa kuhudhuria Mkutano huu. Kisha ameanza kwa kutoa Nukuu ya za wanafalsafa ili kuonesha namna ambavyo waalimu wana umuhimu katika maisha ya Wanaadamu. Rais Magufuli amesema "Mmoja wa Wanafalsafa mashuhuri duniani Aristotle aliwahi kutamka kuwa watu wanaotoa elimu au maarifa kwa watoto wanapaswa kuheshimiwa zaidi kuliko wazazi"

Sambamba na hilo, amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kuwakutanisha katika viwanja hivyo. Vilevile RaisMagufuli amemshukuru Rais wa chama cha Waalimu kwa kumpa heshima na kumualika katika Mkutano huu. Raisi amesema kuwa "Hii inadhihiriwa kuwa bado Waalimu wenzangu wanamkumbuka". Raisi ameeleza kuwa anatambua kuwa mkutano huo ni muhimu sana katika kufanya uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Waalimu Taifa.

Aidha, katika suala hili Rais Magufuli amesema "kusema ukweli nisingependa hata kidogo nionekane kuwa napiga Chapuo kwa Mgombea yoyote, hata hivyo nukweli lazima usemwe".

"Uongozi huu wa CWT ambao unamaliza muda wake umejenga uhusiano mzuri sana na Serikali nanayoiongoza. Na hili nasema kwa Dhati bila upendeleo"

Sambamba na hilo, Rais Magufuli ameleeza mahali palipo na Migogoro hata wao (Rais, Wazir Mkuu na viongozi wengine) ambao walikuwa Waalimu wasingeweza kufika katika ngazi hizo

Rais aahidi kutowatupa walimu
“Ndiyo maana baadaye nilizungumza kwamba hata Corona hata ikikaa mwaka mzima, hata ikae miaka 10, sitakosa mshahara wa kuwalipa walimu hata wakiwa nyumbani. Hii isitafsiriwe kama kampeni. Ninazungumza yale ya ukweli, na msema kweli ni mpenzi wa Mungu”

"Nataka niwahakikishie ndugu zangu walimu, siwezi nikawatupa walimu wa Tanzania. Tunajenga nyumba moja. Nafahamu shida za walimu, kwasababu hata mimi nimeyaishi. Kuwakana walimu ni kuikana nafsi yangu, kitu ambacho siwezi kufanya ndugu zangu walimu."

Rais Magufuli pia amawaasa walimu kutokufanya kazi kwa uhasama na uadui.

Kuhusu Mambo yaliyofanywa na serikali miaka 5 iliyopita katika sekta ya elimu
  • Kutoa elimu bila malipo toka Shule ya Msingi hadi sekondari
“Kimsingi, siyo kwamba tunatoa elimu bila malipo, la hasha! Kinachofanyika ni serikali kubeba jukumu la kugharamia. Tumetoa jukumu hilo kutoka kwa wazazi na kulileta serikalini”

“Tangu utaratibu uanze Desemba 2015 hadi Februari 2020 tumetumia Trilioni 1.01 kugharamia”
  • Ongezeko la idadi na ukarabati wa shule za msingi na sekondari
“Tumeongeza shule za msingi Kutoka shule 16,896 mwaka 2015 hadi shule 17,804 mwaka huu (2020)”

“Shule za sekondari zimeongezeka kutoka 4,708 mwaka 2015 hadi shule 5,330 mwaka 2020”

“Vilevile, tumekarabati shule kongwe 73 kati ya shule kongwe 89”

“Tumejenga mabweni 253 na nyumba 227”

"Tumekarabati vyuo 18, tumjenga upya vyuo 2 – cha Burutunguru na Kabanga, na tumepeleka kompyuta 1550 kwenye vyuo vya ualimu kwa lengo la kuimarisha ufundishaji"

"Tumeongeza vyuo vya ufundi (VETA) kutoka 672 mwaka 2015 hadi 712 mwaka huu. Tumekarabati vifaa na miundombinu ya kufundushia katika vyuo 54 vya maendeleo ya wananchi (FDC)"

"Vilevile, tumejenga hosteli, kumbi za mihadhara, mabwalo ya chakula na maktaba kwenye vyuo vikuu"

"Tumeongeza pia bajeti ya mikopo ya elimu ya juu kutoka Shilingi Bilioni 341 mwaka 2014/15 hadi Shilingi Bilioni 450 mwaka 2019/20."

"Uandikishaji wa darasa la kwanza umeongezeka maradufu, kutoka wastani wa wanafunzi milioni 1 mwaka 2015 hadi kufikia milioni 1.6 mwaka 2020"

"Idadi ya kidato cha kwanza hadi cha 4 imeongezeka kutoka 1,648,359 mwaka 2015 hadi 2,185,037. Lakini la kufurahisha zaidi ni kwamba ufaulu katika shule za msingi na sekondari nao umeongezeka."

“Bila walimu, mafanikio yote haya yasingeweza kupatikana. Hivyo, tunawashukuru sana kutokana na kazi kubwa ambayo mumeifanya. Na ndiyo maana tumeendelea kuwalipa hata katika kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kufuatia ugonjwa wa Corona.”

“Mukumbuke ndugu zangu katika wafanyakazi wote ambao tunawalipa mishahara kila mwezi ambayo ni karibu bilioni 600, nusu ambayo ni zaidi ya bilioni 300 inaenda kwa walimu.”

“Unaweza kujiuliza, bilioni 300 unatoa kama mishahara kwa Walimu amabao hawaendi kufundisha shule. Hii ni thamani ya walimu kwa serikali iliyopo madarakani”

Aidha Akiongelea kuhusu Majanga ya Zika, Ebola na Corona la Corona hapa nchini Rasi Magufuli amesema kuwa "Wakati tunaingia madarakani tuliambiwa Tanzania kuna ugonjwa wa Zika, aliyetangaza na aliyetumiwa kutangaza nikamfukuza kazi (bahati mbaya ni Mgogo); Baada ya kumfukuza yule Mgogo aliyesema Tanzania kuna Zika na waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi, mpaka leo miaka karibu mitano hapajawahi kuwa na kesi hata moja ya Zika hapa Tanzania.

"Baada ya uzushi wa Zika kupita na kumfukuza kazi aliyesema kuna ugonjwa huo, tukakaa baadaye tukaambiwa kuna Ebola, walijua wakisema tuna Ebola Watalii hawatokuja, tukasema sisi hatuna Ebola wala Mjukuu au hawara yake Ebola, hatujaona Ebola wala nani amekufa kwa Ebola hapa Tanzania."

"Ulipokuja Ugonjwa wa Corona watu wakakimbilia ndani wakafunga Makanisa na Misikiti. Ile ni kufuru > Mnakimbilia ndani badala ya kumkimbilia Mungu? Tulitaka kumpa utawala shetani badala ya Mungu aliyetuweka duniani!"

"Umekuja ugonjwa wa Corona Virus wakawa wanasema kwamba maiti zitazagaa barabarani hasa Afrika. Tuliomba siku 3, Corona imekwisha (Tanzania). Waziri wa Afya juzi amesema Dar palikuwa na wagonjwa wanne tu ila uzushi utatolewa wa kila aina".

Aidha, Rais Magufuli amesisitiza Watanzania kumtanguliza Mungu katika kulikabili janga la Corona na ametoa tahadhari kuhusu kupokea vifaa vya Corona ikiwamo barakoa kwa sababu amesema vifaa hivyo vinaweza kutumika kueneza Corona.

Ameonyakuwa kama ukihitaji Barakoa shona yako. Hivyo Watanzania wameonywa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona na kuepuka kutumia vifaa vya kupewa.

"Nilipofunga vyuo na shule kwa sababu ya Corona nikapigiwa simu na Rais wa CWT, Leah Ulaya - Akaniomba nisifanye kama mataifa mengine kwa kutolipa mishahara. Nikamwambia hata Corona ikikaa mwaka mzima au miaka 10 sitakosa mshahara wa kuwalipa walimu"

Aksante baba. I'm totally avoiding every imported product!
 
miaka kumi
 
Hapo yatajazana kuulizia nyongeza ya mshahara, hii kada sjui Kwa nn tu, ina member wenye low IQ sana. Bora ukauze maembe kuliko kuwa mwalimu.
We unaakili za kuvukia bara bara tu. Yaani hujajua umuhimu wa Elimu/katika taifa?
 
1591362192827.png

Rais Magufuli amewataka Watanzania kutotilia maanani baadhi ya maneno ya uongo kutoka kwa watu wa nje, kuhusu milipuko ya magonjwa mbalimbali huku akisimulia namna alivyomfuta kazi kiongozi mmoja wa taasisi ya umma baada ya kutangaza taarifa za uongo kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Zika nchini Tanzania.

Akizungumza leo Ijumaa, Juni 5, 2020, katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania unaofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Rais Magufuli amesema Watanzania wasitishwe wala wasiwe na hofu kuhusu Ugonjwa wa Corona kwani unaelekea kuisha kabisa.

“Wakati tunaingia madarakani tuliambiwa Tanzania kuna ugonjwa unaitwa Zika, aliyetangaza na aliyetumiwa kutangaza nikamfukuza kazi, bahati mbaya ni Mgogo

“Baada ya kumfukuza yule Mgogo aliyesema Tanzania kuna Zika na waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi, mpaka leo miaka karibu mitano hapajawahi kuwa na kesi ya Zika hapa Tanzania.

“Baada ya uzushi wa Zika kupita na nilipomfukuza kazi aliyesema kuna Zika,tukakaa baadaye tukaambiwa kuna Ebola, walijua wakisema tuna Ebola watalii hawatokuja, tukasema sisi hatuna Ebola, wala mjukuu au hawara yake Ebola, na kweli hatujaona mgonjwa amekufa kwa Ebola Tanzania.

“Umekuja ugonjwa wa Corona walikuwa wanazungumza kwamba maiti zitazagaa kwenye barabara hasa Afrika, wao walikuwa watabiri walishindwa kuelewa Mungu analipenda taifa la Tanzania pamoja na Afrika,” amesema
 
Hili lichama la Walimu😡😡😡

Yaani wanalitumia hili lichama kutafutia madaraka na siyo kuwatetea Walimu,inakera sana.
 
Mkuu chukua hao wanafunzi,ambapo ikama inasema kuwa kila mwalimu ahudumie watoto 45 , kwa idadi hiyo ya watoto 250 ukigawanya kwa walimu 6 unakuta kila mwalimu anapaswa kuhudumia watoto 41 ,kwa ikama inavyotaka utagundua kuwa walimu katika shule hiyo wamezidi na wanapaswa kupungua ili ikama ya idadi ya watoto 45 izingatiwe.

Kwa huo mfano ulioutoa ngoja na Mimi nikupe wa kwangu,hapa ninapofundisha Mimi shule yangu ina watoto 320 na idadi ya walimu 24, ikiangalia ikama na idadi ya vipindi unakuta kila mwalimu anahudumia watoto 13, na kwa mwalimu mwenyewe vipindi vingi kwa shule hii ni vipindi 12 ,wakati ikama inataka kila mwalimu awe na vipindi 24 kwa wiki,huoni hapa kuwa kuna ziada ya walimu zaidi ya 5-9?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa ukisema hivyo, kwa hiyo huyo mwalimu mmoja ndio atafundisha masomo yote!!!??
 
Halafu sasa najua kwa nini nchi hii haipigi hatua. Inaongozwa na walimu wa msingi na sekondari. Inaongozwa na watu ambao hata kombi za kidato cha nne hazikukubali. Wengine walikwenda half-combi. Watu wenye akili zao kwa nini wanaogopa siasa?
 
Kuna mwalimu aliyepata division two form four? Ni wakuhesabu wengi division four uongo?
 
Nawaheshimu sana walimu kwa mimi leo nipo hivi kwa ajili ya muda na taaluma zao walizozitumia "seamlessly" hata pia wengi wetu wakafikia hapo walipo. Ni vyema wakipata fursa kama hii ya leo, tena kwa kumkaribisha Mkuu wa Nchi mwenye taaluma kama yao, wasijipendekeze bali wasimame ktk uhalisia wa changamoto zao za kazi na maslahi yao.
 
Pamoja na mapambio yote yale waliyoimba wameambulia dash? Kwi kwi kwii 😁😀😂😂 Acha mambo yawe hivyo hivyo maana Walimu ni moja ya Jumuiya za CCM.

Siku hizi Walimu hata bei za bia hawazijui, wanajinywea ulanzi, chimpumu, na mataputapu mengine. Ukiwauliza wanajifanya Masters wa Mazingira;eti "Sisi Walimu ni wabunifu na tunaweza kuishi kulingana na mazingira yaliyopo ", my ribs 😱😂😂😂
 
Back
Top Bottom