Rais Magufuli afungua mkutano Mkuu wa Chama cha Waalimu, Corona imeisha, Shule za Msingi kufunguliwa karibuni

Kada ya ualimu si mbaya kama tunavyoendelea na mjadala huu naona vijana wengi wanaponda sana na kuwalaumu walimu ambao kimsingi hawana kosa lolote isipokuwa kosa ni mfumo tulionao, walimu hawa wanafanya kazi ktk mazingira magumu sana hasa kwa shule za serikali ambazo miundombinu yake kiuhalisia ni mibovu sana na kwa kweli kunahitajika juhudi si tu za ziada bali uamuzi wa dhati kabisa kuhakikisha kwamba mazingira ya kazi ya walimu yanaboreshwa vzr ili yaweze kuleta tija na kuongeza uthamani wa Elimu kwa ujumla.
 
Aksante baba. I'm totally avoiding every imported product!
 
miaka kumi
 
Hapo yatajazana kuulizia nyongeza ya mshahara, hii kada sjui Kwa nn tu, ina member wenye low IQ sana. Bora ukauze maembe kuliko kuwa mwalimu.
We unaakili za kuvukia bara bara tu. Yaani hujajua umuhimu wa Elimu/katika taifa?
 


Rais Magufuli amewataka Watanzania kutotilia maanani baadhi ya maneno ya uongo kutoka kwa watu wa nje, kuhusu milipuko ya magonjwa mbalimbali huku akisimulia namna alivyomfuta kazi kiongozi mmoja wa taasisi ya umma baada ya kutangaza taarifa za uongo kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Zika nchini Tanzania.

Akizungumza leo Ijumaa, Juni 5, 2020, katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania unaofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Rais Magufuli amesema Watanzania wasitishwe wala wasiwe na hofu kuhusu Ugonjwa wa Corona kwani unaelekea kuisha kabisa.

β€œWakati tunaingia madarakani tuliambiwa Tanzania kuna ugonjwa unaitwa Zika, aliyetangaza na aliyetumiwa kutangaza nikamfukuza kazi, bahati mbaya ni Mgogo

β€œBaada ya kumfukuza yule Mgogo aliyesema Tanzania kuna Zika na waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi, mpaka leo miaka karibu mitano hapajawahi kuwa na kesi ya Zika hapa Tanzania.

β€œBaada ya uzushi wa Zika kupita na nilipomfukuza kazi aliyesema kuna Zika,tukakaa baadaye tukaambiwa kuna Ebola, walijua wakisema tuna Ebola watalii hawatokuja, tukasema sisi hatuna Ebola, wala mjukuu au hawara yake Ebola, na kweli hatujaona mgonjwa amekufa kwa Ebola Tanzania.

β€œUmekuja ugonjwa wa Corona walikuwa wanazungumza kwamba maiti zitazagaa kwenye barabara hasa Afrika, wao walikuwa watabiri walishindwa kuelewa Mungu analipenda taifa la Tanzania pamoja na Afrika,” amesema
 
Hili lichama la Walimu😑😑😑

Yaani wanalitumia hili lichama kutafutia madaraka na siyo kuwatetea Walimu,inakera sana.
 

Sasa ukisema hivyo, kwa hiyo huyo mwalimu mmoja ndio atafundisha masomo yote!!!??
 
Halafu sasa najua kwa nini nchi hii haipigi hatua. Inaongozwa na walimu wa msingi na sekondari. Inaongozwa na watu ambao hata kombi za kidato cha nne hazikukubali. Wengine walikwenda half-combi. Watu wenye akili zao kwa nini wanaogopa siasa?
 
Kuna mwalimu aliyepata division two form four? Ni wakuhesabu wengi division four uongo?
 
Nawaheshimu sana walimu kwa mimi leo nipo hivi kwa ajili ya muda na taaluma zao walizozitumia "seamlessly" hata pia wengi wetu wakafikia hapo walipo. Ni vyema wakipata fursa kama hii ya leo, tena kwa kumkaribisha Mkuu wa Nchi mwenye taaluma kama yao, wasijipendekeze bali wasimame ktk uhalisia wa changamoto zao za kazi na maslahi yao.
 
Pamoja na mapambio yote yale waliyoimba wameambulia dash? Kwi kwi kwii πŸ˜πŸ˜€πŸ˜‚πŸ˜‚ Acha mambo yawe hivyo hivyo maana Walimu ni moja ya Jumuiya za CCM.

Siku hizi Walimu hata bei za bia hawazijui, wanajinywea ulanzi, chimpumu, na mataputapu mengine. Ukiwauliza wanajifanya Masters wa Mazingira;eti "Sisi Walimu ni wabunifu na tunaweza kuishi kulingana na mazingira yaliyopo ", my ribs πŸ˜±πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…