Mkuu chukua hao wanafunzi,ambapo ikama inasema kuwa kila mwalimu ahudumie watoto 45 , kwa idadi hiyo ya watoto 250 ukigawanya kwa walimu 6 unakuta kila mwalimu anapaswa kuhudumia watoto 41 ,kwa ikama inavyotaka utagundua kuwa walimu katika shule hiyo wamezidi na wanapaswa kupungua ili ikama ya idadi ya watoto 45 izingatiwe.
Kwa huo mfano ulioutoa ngoja na Mimi nikupe wa kwangu,hapa ninapofundisha Mimi shule yangu ina watoto 320 na idadi ya walimu 24, ikiangalia ikama na idadi ya vipindi unakuta kila mwalimu anahudumia watoto 13, na kwa mwalimu mwenyewe vipindi vingi kwa shule hii ni vipindi 12 ,wakati ikama inataka kila mwalimu awe na vipindi 24 kwa wiki,huoni hapa kuwa kuna ziada ya walimu zaidi ya 5-9?
Sent using
Jamii Forums mobile app