Rais Magufuli ajibu hoja za Marekani, Asijifiche kwenye hoja za uzalendo, Kwanza sio Mzalendo

Unataka akujibu wewe ama Marekani? Kama ni Marekani ameshajibu tena kwa kutuma mtu.
 
Maneno haya ungemwambia Kabudi na Mh. Rais.

Hivi unaelewa kwa nini Kabudi alienda na ujumbe wa Rais Magufuli US unaosema uchaguzi utakuwa huru na haki? Kama huelewi, usikate tamaa. Ujinga huondoka kwa kujifunza toka kwa wenye uelewa
 
Wewe marekani ni nani kwako... Wewe anaweza jibu hoja zako... Katiba yetu inamtambua mtu anaitwa mmarekani hadi rais wetu ajibu hoja... Au unafikiri marekani ana urafiki na wewe.? Ungejua ya nyuma ya pazia ya marekani wala usingeongea.
Kama Marekani siyo rafiki yetu, rafiki yetu atakuwa ni yule anayeteka watu, anayesingizia watu kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha haramu, anayepoteza watu na anayeshambulia watu kwa risasi kwa sababu wamemkosoa?

Ubaya wa Marekani hatujauona lakini ubaya wa anayeua watu, kuteka watu, kuwapoteza watu, kubambikia watu kesi zisizo na dhamana, timeuona na tunaujua. Kama una mashaka na hilo, kaitembelee familia ya Ben Saanane, Azory Gwanda, Tundu Lisu, na wale wote waliorundikwa Segerea kwa uonevu, na kuamriwa wakiri na kulipa pesa walizopangiwa ili watoke.
 
Swali dogo tu plz naomba jibu hivi Magu anawajibika kwa marekani hadi ajibu hoja zao?
Usiishie kujiuliza hilo tu. Jiulize pia, hivi Marekani, ni Baba yetu hadi Magufuli amtume Kabudi kwenda kuomba fedha?
 
Tinajidhalilisha zaidi kama Taifa, tunapokuwa na viongozi ambao hawatendi haki kwa watu wake.

Tunakuwa ni sawa na nguruwe maana nguruwe akiwa na njaa huweza kula hata watoto wanapozaliwa.
 
We la Marekani hulioni unaona la Tanzania tu?
Hivi kwenye haki za binadamu unaweza kumquote Marekani kweli?
Mmekuwa brainwashed utafikiri hamjasoma?
Mnatia kichefuchefu!
Utawala wa Marekani nao hiwa wanateka wananchi wao wanaomkosoa Rais? Mbona Trump anasema kila siku lakini hatusikii waliotekwa?
 
Unayoyasema hatuna uhakika nayo lakini tuna uhakika Marekani hawawateki wala kumpoteza mtu yeyote anayemkosoa Trump. Trump anajibizana na wakosoaji wake kwenye tweeter kama wanadamu wenzake. Hawapotezi watu.

Hapa kwetu JF imekuwa maarufu kutokana na hofu ya watu kuwa huwezi kuwakosoa watawala wala serikali kwa uwazi, na ukajulikana, na ukawa na uhakika wa 100% utakuwa salama.
 
Mkuu wewe ni mmoja wa watu ninaowaheshimu hapa jf kutokana na uwezo wako wa kujenga hoja... Pia hoja yako nakubaliana nayo japo sio 100%....Sisi bado hatujafikia uwezo wa kuuona ubaya wa marekani... Bado tunamuona kama mtu mzuri kwetu kutokana na misaada yake...

Tumekuwa tukiangaliwa sana na marekani kwa siku za karibuni hasa kutokana na baadhi ya mambo uliyoyataja hapo juu..in general tuseme haki za binadamu...Lakini tujiulize huyu tunayemuangalia kama kioo kwa upande wa haki za binadamu anafuata kweli hiyo misingi ya haki za binadamu? US haoni shida kumpoteza mtu asiye mwananchi wake au anayeingilia masirahi yake...

Kama angekuwa anafuata misingi ya hizo haki basi asingewatishia majaji na officials wa ICC kuwawekea vikwazo na kuwapiga pini wasiingie US kama wangeendelea na uchunguzi wao wa kesi ya askari wa marekani nchini afaghanistan...huyu mtu yupo kimasirahi zaidi... Note sipingani nawe,nakubali kwamba demokrasia nchini imeshuka....But si sahihi kabisa kuanza kumtegemea na kumpigia magoti US eti aingilie mambo yetu ya ndani... Yaani to the extent rais ainuke ajitetee kwenye media!!! Mimi sikubaliana nalo... Au unasemaje kiongozi?
 
Ilikuwa lzm innocent watolewe kafala ili wwe ubakie Salama,Bila hivo ungeshalipuliwa Na magaidi kitambo,msitetee umwagaji damu sababu ni wanufaika
 
Wewe marekani ni nani kwako... Wewe anaweza jibu hoja zako... Katiba yetu inamtambua mtu anaitwa mmarekani hadi rais wetu ajibu hoja... Au unafikiri marekani ana urafiki na wewe.? Ungejua ya nyuma ya pazia ya marekani wala usingeongea.
Hatuwwezi jisimamia nguvu ya nje dhid ya uovu ni muhimu.Kama mnatenda haki hofu ya nn
 
Unfortunately umeandika kwa hasira na hivyo ukawa umeshindwa kutenganisha hisia na facts. Kuhusu watu kutekwa na kuteswa, ungejua yaliyomkuta Dr Ulimboka ni zamani sana tunaweza kuwa tumesahahu. Kuhusu watu kupigwa risasi ungejua watu waliopigwa risasi Mwembechai ni zamani sana, tunaweza kuwa hatujui tena.

Ungejua kuhusu vyombo vya habari Tanzania kuwa Mwanahalisi liliwahi kufingiwa, ni zamani sana hatukumbuki tena. Umeandika kama vile matukio hayo ni ya leo tu. Wakati yanatokea enzi hizo Marekani hiyo haikusema lolote, ila yanapotokea leo inakuwa ni kama smokescreen tu kes Marekani kuishambulia serikali ya sasa.

Siyo kwamba matukio hayo ni mazuri, ila yemekuwa kwenye system yetu muda wote huo na na yalivumiliwa na Marekani, hivyo wao leo hawawezi kuja kutuambia la kufanya. Ni sisi wenyewe kujiangalia na kujiweka utawaraibu wa kisheria kuachana na mambo hayo.
 
Unfortunately umeandika kwa hasira na hivyo ukawa umeshindwa kutenganisha hisia na facts. Kuhusu watu kutekwa na kuteswa, ungejua yaliyomkuta Dr Ulimboka ni zamani sana tunaweza kuwa tumesahau. Kuhusu watu kupigwa risasi ungejua watu waliopigwa risasi Mwembechai ni zamani sana, tunaweza kuwa hatujui tena.

Ungejua kuhusu vyombo vya habari Tanzania kuwa Mwanahalisi liliwahi kufungiwa, ni zamani sana hatukumbuki tena. Umeandika kama vile matukio hayo ni ya leo tu. Wakati yanatokea enzi hizo Marekani hiyo haikusema lolote, ila yanapotokea leo inakuwa ni kama smokescreen tu kwa Marekani kuishambulia serikali ya sasa.

Siyo kwamba matukio hayo ni mazuri, ila yamekuwa kwenye system yetu muda wote huo na yalivumiliwa na Marekani, hivyo wao leo hawawezi kuja kutuambia la kufanya. Ni sisi wenyewe kujiangalia na kujiwekea utaribu wa kisheria kuachana na mambo hayo.
 
Sasa Sisi hiyo mikataba si tuliiridhia Kwa hivyo hi wajibu wa watawala wetu kina magufuli kuitekeleza kama ilivyo siyo anavyoona yeye inafaa.
 
Usitetee uovu sababu Leo Uko Salama,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…