Rais Magufuli amchenjia Makonda?

Rais Magufuli amchenjia Makonda?

Alafu kwa sisi makamisaa kumbuka kasema kama anabembeleza.
Nukuu;makonda kama kweli hiyo hela umeichukua irudishe ,nasema tena kama ni kweli urejeshe:mwisho
Kwa kauli hii ingekuwa sio patna wake anamsema hivyo labda mkuu mwingeni wa mkoa leo hii hii pale pale ngetoa tamko.

Ingekuwa mwingine angetumbuliwa palepale.

Mambo ya ‘kama ni kweli’ yasingekuwepo!

Sad.
 
Nyani Ngabu,
Duh mfalme wa Dar ametajwa tena leo.Lakini hana wasiwasi maana hakuna tsunami lenye uzito wa kumtingisha.Nasema Makonda chapa kazi.
 
2074663_kwinyara___ByIaUpZA8Tq___.jpeg


5e2be86d4c02b991028e5a979fd72227.jpg

Kama ni miaka hii sioni tatizo!
 
Labda ingependeza kama ungeelezea kwa kifupi makosa ya huyo bwana mdogo DAB ili ruweze kuchangia kwa uhakika zaidi. Karibu kiongoz
 
Ingekuwa mwingine angetumbuliwa palepale.

Mambo ya ‘kama ni kweli’ yasingekuwepo!

Sad.
Yaani katoa onyo la kurudisha sio la kukaripia lile la kufanya maamuzi sio kama la wengine wanavyofanyiwa hadharani
 
Vidokezo navyo tunageuza kuwa mijadala wakuuu ile ilikuwa kidding
 
Nyani Ngabu,
Kwakuwa hao wawili wana maagano yao Magu hana uwezo wa kumwajibisha Makonda kama ambavyo anavyowawajibisha wengine. Magu mpaka anaingia kaburuni hawezi sahau Makonda alichomfanyia. Makonda kashika mpini na Magu kashika makali huo ndiyo ukweli mchungu!!!!
 
Rais Magufuli leo kasema, kama Makonda alizitumia fedha za TASAF, basi na azirudishe.

Vilisikika vicheko hafifu na vya chinichini baada ya Rais kusema hivyo.

Kamera nazo zikamwonyesha Makonda, aliyekuwa kakaa mbele pamoja na viongozi wengine, akitabasamu kana kwamba hana wasiwasi wowote. Yaani hakuna baya litalomtokea [sababu yaweza kuwa ni kwa sababu hakuzitumia kabisa hizo hela, au, alizitumia lakini anajua kuwa Rais hatomfanya chochote, n.k.]

Kamera pia ziliwaonyesha marais wastaafu wote watatu.

Kwa kuwasoma lugha yao ya mwili, ni kama vile walikuwa ‘embarrassed’ na alichokisema rais.

Ni kweli Rais Magufuli alimaanisha alichokisema au kasema vile ili kuonyesha tu kuwa ‘hampendelei’ Makonda?

Binafsi naona kama vile kasema tu ili kuonyesha ‘hampendelei’ jamaa huku kiuhalisia hakuna lolote atalomfanya maana jamaa ana madhambi mengi na makubwa kuliko hilo la kutumia fedha za TASAF.

Bofya video umsikie Rais alivyosema kuhusu Makonda. Kuanzia dakika ya kwanza hadi ya pili.


Magufuli kwa mara nyingine ametuonesha alivyo weak.

Zile tumbua tumbua zote zilikuwa ni show ya kibabe kwa wasio na hadhi, kakutana na Makonda imebidi amuombe kiupolepole kama mwanamke anayemuogopa mumewe.

Mara ya kwanza niliona weakness hii kwenye issue ya Makonda kuingiza makontena bila kulipa kodi.

Hii ni mara nyingine.

Pia, rais mzodoaji watu hatakiwi kuanza kuongelea habari za "kama", hususan ikiwa Makonda mwenyewe yupo hapo.

Ile style yake Magufuli ya kuendesha mahakama majukwaani kwa nini haitumii kwa Makonda? Kwa nini hakumtaka Makonda ajieleze?

Na zaidi, ikiwa Makonda atarudisha hela, kitatokea nini?

Ndiyo utakuwa mwisho wa habari? Au atachukuliwa hatua zaidi?

Asipochukuliwa hatua, rais atakuwa anatuma ujumbe gani? Kwamba watumishi wa serikali wafuje mali za umma na kuiba tu, wasikamatwe, na wakikamatwa hawachukuliwi hatua, wataambiwa warudishe walichoiba tu?
 
Labda kuwe na other forces toka juu zaidi, maana kama kumtumbua kwa mamlaka yake kama rais bas angekua kashamtumbua siku nying sana.
Huyu jamaa amefanya mengi ambayo hayapaswi kufanywa na kiongozi achilia mbali utata wa elimu yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila kweli it's unlikely to happen.... Kuna muda hata mkulu anaonekana kumtumia kwenye mission zake.
 
Back
Top Bottom