Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
RAIS John Magufuli amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, kuwapunguzia mishahara watumishi wote waliokuwa wakifanya kazi Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) ambao umefutwa na kuhamishiwa Wizara ya Madini, kwa sababu kazi waliyoifanya wakiwa TMAA ilikuwa ya hovyo
Amesema watumishi hao wa TMAA ambao hawataridhika na uamuzi huo wa kupunguziwa mishahara, waache kazi wakafanye kazi zingine.
Alitoa maagizo hayo jana Ikulu Chamwino jijini Dodoma baada ya kumuapisha Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukrani Manya.
Magufuli alisema aliamua kulizungumza jambo hilo hadharani ili asijetafutwa ‘mchawi’ wa TMAA, kwa kuwa watumishi hao walipokuwa TMAA walikuwa na mishahara mizuri, lakini baada ya kuhamishiwa wizarani wamekuja na mishahara yao.
“Hiyo mishahara Katibu Mkuu Kiongozi ipunguzwe. Wale walitakiwa kupunguzwa kazi, kwa sababu kazi waliyokuwa wakiifanya TMAA ilikuwa ya hovyo. Ila hatutaki kuhukumu kwa ujumla, kwa hiyo wamerudi huku. Haiwezekani upelekwe Tume ya Madini wakati umetoka kule na mshahara wa shilingi milioni 10, ukamzidi hata mkurugenzi wako, ukamzidi hata mwenyekiti mtendaji, wakati bosi wako anapokea mshahara wa shilingi milioni tano, wewe una shilingi milioni 10.
“Hatuwezi tukafanya hivyo. Anayetakiwa kuzidiwa mshahara ni mimi, mimi napata mshahara wa shilingi milioni tisa lakini mtu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) ana mshahara wa shilingi milioni 15. Nasema mtu yeyote anayefanya kazi vizuri apate mshahara mzuri, lakini wanaofanya vibaya, nataka wakose kabisa au wapate kidogo sana ili iwe fundisho kwao kufanya kazi kwa bidii” alisema Rais Magufuli.