Rais Magufuli amfukuza kazi Mtumishi wa Serikali aliyechana Juzuu Amma huko Kilosa

Rais Magufuli amfukuza kazi Mtumishi wa Serikali aliyechana Juzuu Amma huko Kilosa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Rais Magufuli akiwa leo anazindua Jengo la Manispaa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigamboni amemsifu Waziri Jafo kwa kumsimamisha kazi lakini amesema yeye amemfukuza kabisa.

Amesema "Juzi nilimsikia Waziri Jafo, Mtu mmoja kule Kilosa nafikiri alichana Kitabu Kitabu Kitakatifu. Nashukuru ulichukua hatua ya kumfukuza kazi. Lakini mimi namfukuza moja kwa moja muandikie barua ya kumfukuza moja kwa moja"

Ameongeza "Ashinde kesi asishinde huyo si mfanyakazi wa Serikali. Hatuwezi tukakaa na Wafanyakazi Wapumbavu. Katika Serikali hii."

Umechukua jukumo lako la kumsimamisha kazi mimi namfukuza kabisa. Akitoka huko kutumikia adhabu aende akatafute maisha.

Amemalizia "Hili nilikuwa nachomekea tu....."

Kwa taarifa zaidi, tembelea Mtumishi wa umma mbaroni kwa kuchana na kuchoma Quran, Waziri Jafo aagiza asimamishwe kazi
 
Ila na hawa ndugu zetu wanadeka sana.

Hapa tumeogopa mengi.

Unaweza kukuta kichaa huyo akasababisha watu wakavaa mabomu au kuchoma makanisa.

Mpumbavu ni mpumbavu anaweza kuwa huku au kule ni kuwadhibiti mapema.

Lakini ninajiuliza kwa nini kila siku iwe kitabu hiki tu cha waislamu ndiyo mara kinachanwa mara kinachoma moto, kwa nini lakini?

mbona biblia inachanwa na hata kuchomwa moto . watu hawana shida kwa maana wanamuachia Mungu.

Ila kwa nini hikikitabu tu kiteswa mara kwa mara.
 
Angesubiria hatua za kinidhamu zikamilike ili nayeye apewe haki ya kusikilizwa halafu maamuzi yafanyike,Jafo alikuwa sahihi katika hili.

Vinginevyo hio itakuwa mihemko ya kuelekea Uchaguzi.

Kwanza inahisiwa hata mtu mwenyewe hakuwa katika akili timamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kulewa isiwe sababu ya kufanya ujinga Alafu nyie walevi bwana mnafanya ujinga mnataka muachwe eti tu umelewa
Mkishikiswa adabu mtakunywa kwa ustaarabu mkichekewa mtafanya zaidi ya hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na ndipo hapo maamuzi ya kukurupuka yanapojidhihirisha
Hilo ni agizo! Utekelezaji wake utahusisha mamlaka yake ya nidhamu ambayo ni Baraza la madiwani. Unaweza kukuta shitaka ni tofauti na kuchana kitabu kitukufu wakamfukuza kwa kutoonekana kazini kwa siku 5 mfululizo nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila na hawa ndugu zetu wanadeka sana.

Hapa tumeogopa mengi.

Unaweza kukuta kichaa huyo akasababisha watu wakavaa mabomu au kuchoma makanisa.

Mpumbavu ni mpumbavu anaweza kuwa huku au kule ni kuwadhibiti mapema.

Lakini ninajiuliza kwa nini kila siku iwe kitabu hiki tu cha waislamu ndiyo mara kinachanwa mara kinachoma moto, kwa nini lakini?

mbona biblia inachanwa na hata kuchomwa moto . watu hawana shida kwa maana wanamuachia Mungu.

Ila kwa nini hikikitabu tu kiteswa mara kwa mara.
Kama kuna mtumishi wa Umma alifanya hivyo mtaje nae apigwe chini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom