Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amnadi Patrobas Katambi, aahidi kumpa kazi nyingine Stephen Masele

Magu anapanga safu ya vibaraka wake, ndio maana katambi alivyorudi tu Dodoma akaita kamedia uchwara eti ana mjibu TL, kuwaonesha
Mabwana zake kuwa kazi wanayoenda kumpa anaimudu, hovyo!

Katambi ni kati ya vijiwanasiasa ambavyo havijawahi kukubalika, kinajua tu kujipenyeza, watapata sana shida kumnadi.

Masele kama anapatana na viongozi wa chama mkoa na wilaya awatumie kumwangusha katambi mbona mwepesi tu, Wamuunge mkono mgombea wa upinzani kimya kimya pwetelea pwete! 😀
 
Hapo ndo mjue Raisi Magufuli ni genius, unaweza ukazani kamsahau mtu ama kamuonea kumbe anampango naye mwingine mkubwa, mfano ni huyo Steven Masele.

Ambaye anaweza kuwa balozi kuwakilisha nchi kwenye taifa jingine, ama SADC, AU, na UN.

Mkuu unajua maana ya neno genius? Ama Ni spelling error?
 
Hapo ndo mjue Raisi Magufuli ni genius, unaweza ukazani kamsahau mtu ama kamuonea kumbe anampango naye mwingine mkubwa, mfano ni huyo Steven Masele.

Ambaye anaweza kuwa balozi kuwakilisha nchi kwenye taifa jingine, ama SADC, AU, na UN.
Upuuzi mtupu, kabla ya kura za maoni tuliambiwa watakaotoa rushwa watakatwa na wote waliokatwa walitoa rushwa, sasa mwenye dhambi ya hivo unamrudishaje kwe serikali yako.
 
Angalia kifua Cha Masele na Cha Katambi..Kana Kama utapiamlo..lol
katambi bana bora angetulia kuu mkuu wilaya maana mishahara ndo ile ile the same 3M tofauti ni kwamba mkuu wilaya kila siku lazima awahi kazini yan kama mwanafunzi ila mbunge anakua free na uhakika wa miaka mi5 bila kuguswa ila ukuu wilaya mkuu akiamua chap tu nyuma geuka
 



!
!
Kwani ubunge ni swala la mtu binafsi au swala la jamii? na vipi akiukosa uraisi! Masele aligombea ili kuikwamua jamii yake, sasa kumpeleka akawe mkuu wa mkoa wa Mbeya inaleta picha gani?
 
Dawa ni kukataa miswaada ya hati za dharura.
 
Magufuli hatoshinda uchaguzi huu , huo ukuu wa mkoa atakaompa Masele atautoa wapi ?
Without any form of alliance ni Ndoto kuitoa CCM madarakani.Mnavyosema atashindwa uchaguzi ni kuwa mmeamua kujitoa ufahamu au mmechanganyikiwa??
 
Ndo mana jamaa hajoa mpaka leo

Akienda Arusha atapata mke kama tatizo ni hayo meno, maana watu wa Arusha wengi meno yao yana rangi. Kuweka record sawa, meno kuwa na rangi haimaanishi yameoza au hupigi mswaki, bali ni madini yaliyo kwenye maji ambayo huchangia meno kushika rangi na sio kuoza. Sehemu kubwa ya Arusha na maeneo kadha ya mikoa ya Kilimanjaro, Manyara na Singida kuna tatizo hili.
 
Hakuna yeyote mwenye hofu ya Mungu anaweza kuchagua Magufuli
Kwani Magufuli anahitaji hofu ya Mungu au dola,NEC na wakurugenzi?
Umeona coverage ya kampeni za upinzani ipoje kwenye vyombo vya habari?Je kule vijijini wana tweeter na Insta??...
Hilo ni piga lingingine.Kingine turn up ya audience kwenye hizo kampeni ni kubwa baadhi ya miji tu.Je katika jamii yenye watu wengi wasiosoma kama tz kweli kukosa 'kivutio' cha public figures fulani au squad ya wasanii fulani kidogo tu sio fatal mistake?
CcM inapita kilaini sana mwaka huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…