Rais Magufuli amteua Asha-Rose Migiro kuwa Balozi nchini Uingereza

Rais Magufuli amteua Asha-Rose Migiro kuwa Balozi nchini Uingereza

Mama yetu huyu anapenda sana nafasi za kuteuliwa mweee jamani, yaani yeye kusema ajaribu angalao hata kugombea ubunge wa jimbo wapi, anasubiri dezo tu jamani
Umesahau kua aligombea urais
 
Najiuliza hili povu la wana UKIWA hapa linasababishwa na kitu hasa?
 
Wadhifa kama Naibu Katibu Mkuu UN hazina kupanda cheo au kushuka cheo. Asha Migiro anafaa kuendelea kuitumikia nchi yake Tanzania, na ubalozi huko Uingereza ni uteuzi wa hekima na muafaka toka kwa raisi. Wajibu wangu naona ni kusema," Hongera Bibi Asha Rose Migiro!"
 
Wadhifa kama Naibu Katibu Mkuu UN hazina kupanda cheo au kushuka cheo. Asha Migiro anafaa kuendelea kuitumikia nchi yake Tanzania, na ubalozi huko Uingereza ni uteuzi wa hekima na muafaka toka kwa raisi. Wajibu wangu naona ni kusema," Hongera Bibi Asha Rose Migiro!"
Kwahiyo kumbe kuna tofauti kati ya balozi wa Tanzania nchini burundi na uingereza ?
 
Halafu unakosea me sio chadema, kuhusu Migiro haijaniuma kitu, ila niliuliza tu, kuwa hakuna wengine wenye sifa? Maana yeye km kuitumikia Tz ameitumikia INA tosha sasa apumzike, ni zamu ya wengine
Huu sasa ni wivu,siasa Ina kustaafu kwani?
 
Umejipanga vipi kuzungusha kiuno 2020!?
Huyu Magufuli vipi? huyu mama hana uwezo wowote alishashindwa huko UN kwani huko wizarani hakuna ma career diplomats? huyu atafanya economic diplomacy gani aliishia kufanya vitu vya Tayoa miaka yote aliyokua UN kwa nini watanzania tuko hivi? Napinga kwa nguvu zote uteuzi huu ndio maana tulitaka katiba mpya hizi kazi watu waawe wanazipigania, this is foolish
 
It is only in africa where a person can walk 100 steps ahead and go back 150 steps and praises him/herself that he/she is improving

It's only ignorant people who don't know that to serve their countries is to live (and sometimes die) with a sense of purpose. This lady has accomplished a lot and cheo means nothing to her. Service is the gift we give to the world. It’s what makes us human. It is also what gives our lives meaning. Serving our countries is part of serving humanity.
 
Kule UN Ban ki Moon alijuta kuwa na subordinate ambaye hakuenda na spidi yake ya kazi ndo maana alimtema pre mature!
 
It's only ignorant people who don't know that to serve their countries is to live (and sometimes die) with a sense of purpose. This lady has accomplished a lot and cheo means nothing to her. Service is the gift we give to the world. It’s what makes us human. It is also what gives our lives meaning. Serving our countries is part of serving humanity.

This mama has never been productive!
 
This mama has never been productive!

It depends on your defintion of "being productive". She was able to do something significant in life, something positive. She served in the National Service (JKT), volunteered in her community, earned academic achievements, lecturer, minister for two presidents, UN assistant Sec General, and most importantly she's a “Mom.” Relationships are what count most in life. Need I say more?
 
It depends on your defintion of "being productive". She was able to do something significant in life, something positive. She served in the National Service (JKT), volunteered in her community, earned academic achievements, lecturer, minister for two presidents, UN assistant Sec General, and most importantly she's a “Mom.” Relationships are what count most in life. Need I say more?

Ndo nini hicho ulichoandikaa? kama yote hayo amepitia bila kuleta faida kwa nchi azidi kuteuliwa tu? hukumbuki hata alivyopwaya vizara ya sheria na katiba?

Kweli waTz mnayo matatizo sana kichwani mwenu.
 
Njaa tu inayomsumbua na kujidhalilisha maana haiwi uwe na cheo cha Unaibu than umalize mda wako upewe cheo cha Ubalozi wa Nyumba kumi angejifikiria kwanza huzo bibi ni bora angebakia mstaafu Naibu tuu ili alinde heshima yake
 
ASHA Rose Migiro, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), muda wowote kuanzia sasa, atatangazwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Taarifa za ndani kutoka katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa zinaeleza kuwa, jina la Dk. Migiro ambaye aliwahi kutumikia nafasi mbalimba ndani na nje tayari limefikishwa Uingereza kwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Februari mwaka huu Rais John Magufuli kutangaza kwamba, Dk. Migoro atateuliwa kuwa balozi bila kutaja nchi atakayokwenda kuiwakilisha Tanzania.

Uteuzi wa Dk. Migoro uliibua mjadala kutokana na kushika kwake nafasi mbalimbali za kidiplomasia ambapo mjadala huo ulijielekeza kuwa ‘ameshuka ama amepanda?’

Miongoni mwa nafasi za juu za kidiplomasia alizowahi kushika Dk. Migiro ni pamona na kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).

Aliteuliwa tarehe 5 Januari 2007. Dk. Migiro aliteuliwa na Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) kushika nafasi hiyo akiwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo baada ya Louise Fréchette, mwanadiplomasia wa Canada aliyeongoza kuanzia Aprili 1997 hadi Aprili 2006.

Dk. Migiro alichukua nafasi hiyo iliyoachwa na George Mark Malloch Brown wa Uingereza. Dk. Migiro alishikilia wadhifa huo kwa miaka mitano. Julai 2012 nafasi yake ilichukuliwa na mwanadiplomasia wa Sweden, Jan Elliason.

Mapito ya Dk. Migiro

Dk. Migiro alizaliwa tarehe 9 Julai 1956 katika Wilaya ya Songea, Ruvuma. Alisoma Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, Dar es Salaam mwaka 1963 hadi mwaka 1966.

Dk. Migiro alihamia Shule ya Msingi Korogwe, Tanga ambapo aliendela na elimu ya msingi mwaka 1967–1969.

Baadaye akajiunga kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Weruweru, Kilimanjaro mwaka 1970 hadi 1973 na Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari Korogwe mwaka 1974 -1975.

Dk. Migiro alikuwa mmoja wa wasichana waliofaulu vizuri Korogwe Sekondari na alipojiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1977, alichukua masomo ya sheria na kuhitimu Shahada yake (LLB) mwaka 1980.

Baadaye aliajiriwa UDSM kufundisha masomo ya sheria kama Mhadhiri Msaidizi. Alifanya kazi hiyo kwa miaka miwili kabla ya kuendelea tena na masomo ya juu ya sheria mwaka 1982–1984 hapohapo UDSM na kutunukiwa shahada ya uzamili (LLM).

Kati ya mwaka 1985–1988, alifundisha UDSM. Mwaka 1988 alikwenda Chuo Kikuu cha Konstanz, Ujerumani ambako alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika masuala ya Sheria mwaka 1992.

Dk. Migiro alirejea Tanzania akiwa Mhadhiri Mwandamizi na aliendelea kufundisha katika Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi mwaka 2000 alipoingia kwenye siasa.

Akiwa UDSM kati ya mwaka 1992 – 1994 Dk. Migiro alikuwa Mkuu wa Idara ya Sheria za Katiba na Utawala.

Kati ya mwaka 1994 – 1997 aliongoza Idara ya Sheria za Makosa ya Jinai (Idara zote zipo katika Kitivo cha Sheria UDSM).

Dk Migiro ni mzungumzaji mzuri katika lugha ya Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani. Ni mke wa Profesa Cleophas Migiro na wana watoto wawili wa kike.

Dk Migiro alianza na siasa za kujijenga akitokea katika taaluma. Mwaka 2000, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alimteua kuwa waziri kwenye Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.

Alitumikia wadhifa huo hadi mwaka 2005 bila kubadilishwa akisimamia mambo mengi ya kisera na kimiundombinu, bila kusahau utekelezaji na upiganiaji wa haki za wanawake na watoto.

Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005, alimteua kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje, Januari 2006 na kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kushikilia wadhifa huo. Katika kipindi cha mwaka mmoja tu, alifanya kazi nyingi za kimataifa zilizomweka katika anga nyingine kisiasa.

Januari 5, 2007, aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu (UN) mpaka 2012 alipomaliza muda wake. Januari mwaka 2013, Dk Migiro aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Desemba 2013 aliteuliwa kuwa mbunge katika Bunge la Tanzania.

Januari 2014 aliteuliwa kuwa Waziri wa Sheria na Katiba, nafasi ambayo alidumu nayo mpaka Rais Kikwete alipomaliza muda wake mwaka jana.

====================

Updates 1800HRS;

===================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Dkt. Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani.

Dkt. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dodoma

04 Mei, 2016
View attachment 344749
Huyu dada namkubali mno tokea nilipomsikia siku ya kuomba kura kwenye tatu za urais kupitia CCM, hotuba yake ilinikuna sana kwa mpangilio na uwasilishaji wake. Kwa kuwa ni mjuzi wa lugha hizo tatu za Ulaya nadhani alikuwa anafaa awe balozi wetu kwenye Umoja wa Mataifa.
 
Huyu bibi huwa anapenda ushindi wa mezani....... Hawezi kabisa ku struggle. Hata urais alitaka apewe out of sympathy.
 
Back
Top Bottom