Rais Magufuli amteua Asha-Rose Migiro kuwa Balozi nchini Uingereza

Rais Magufuli amteua Asha-Rose Migiro kuwa Balozi nchini Uingereza

Nauliza hivi,huyo migiro kule un alipokuwa anafanya kazi kama naibu katibu mkuu je ali staafu au muda wake ulikatizwa?na kama ulikatizwa ni kwa sababu zipi?
Haya mzigo huo pakuwa sijui itakuaje na wewe kiingereza ni msiba mzito

Tanzania took office as UN Deputy Secretary-General on 1 February 2007, and her term ended on 30 June 2012. She was the third person to occupy the post since it was established in 1997 and the first African woman to do so.Prior to joining the UN, Ms. Migiro served as her country’s first female foreign minister, from 2006-2007. In addition to her extensive experience in government service, she also pursued a career in academia in Tanzania.On the eve of her departure, Ms. Migiro spoke with UN News Centre about some of the challenges she faced during her tenure, as well as issues she worked closely on such as the Millennium Development Goals, the global anti-poverty targets with a 2015 deadline, and the ‘Delivering as One’ initiative launched in 2007 to test how the UN can provide more coordinated development assistance in eight pilot countries – Albania, Cape Verde, Mozambique, Pakistan, Rwanda, Tanzania, Uruguay, and Viet Nam.UN News Centre: You are the first African woman to serve as Deputy Secretary-General of the United Nations. What is the significance of this?Asha-Rose Migiro: I humbly acknowledge that fact. You know very well that here at the UN any of the issues we deal with pertain to Africa – development, peace, security, health, education – and so it is important that when you have such issues, you also have a person who can give voice to those issues. Yes, I am the first African woman to serve in this position. I feel humbled and honoured. It is also, on the other hand, a reflection of Secretary-General Ban’s commitment to Africa and to the empowerment of women.
 
CCM ni ile ile, msitegemee chochote kipya kutoka CCM, Tatizo ni mfumo!
 
Teeeeeeh teeeeeeeeeh, hicho Kingereza kweli ni msiba mzito sana hapa Tanganyika ndio maana kuna watu wakubwa wanawakimbia hao wanao zungumza kiingereza
 
duuh jf kiboko,ilianza kama tetesi hatimae hata siku haijaisha mzigo upo hewani
 
Sasa Professor anamfuata Uingereza au vipi.Dah,ndoa nyingine ni vilio tupu.
Kutoka naibu Katibu Mkuu UN hadi kuwa balozi ni free fall. Kama sio ni kwa ajili ya njaa sidhani kama kuna motivation nyingine kwa huyo mama kukubali hiyo post. Wazo la kustaafu kwa heshima ni gumu sana kueleweka kwa hawa jamaa

ASHA Rose Migiro, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), muda wowote kuanzia sasa, atatangazwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Taarifa za ndani kutoka katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa zinaeleza kuwa, jina la Dk. Migiro ambaye aliwahi kutumikia nafasi mbalimba ndani na nje tayari limefikishwa Uingereza kwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Februari mwaka huu Rais John Magufuli kutangaza kwamba, Dk. Migoro atateuliwa kuwa balozi bila kutaja nchi atakayokwenda kuiwakilisha Tanzania.

Uteuzi wa Dk. Migoro uliibua mjadala kutokana na kushika kwake nafasi mbalimbali za kidiplomasia ambapo mjadala huo ulijielekeza kuwa ‘ameshuka ama amepanda?’

Miongoni mwa nafasi za juu za kidiplomasia alizowahi kushika Dk. Migiro ni pamona na kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).

Aliteuliwa tarehe 5 Januari 2007. Dk. Migiro aliteuliwa na Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) kushika nafasi hiyo akiwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo baada ya Louise Fréchette, mwanadiplomasia wa Canada aliyeongoza kuanzia Aprili 1997 hadi Aprili 2006.

Dk. Migiro alichukua nafasi hiyo iliyoachwa na George Mark Malloch Brown wa Uingereza. Dk. Migiro alishikilia wadhifa huo kwa miaka mitano. Julai 2012 nafasi yake ilichukuliwa na mwanadiplomasia wa Sweden, Jan Elliason.

Mapito ya Dk. Migiro

Dk. Migiro alizaliwa tarehe 9 Julai 1956 katika Wilaya ya Songea, Ruvuma. Alisoma Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, Dar es Salaam mwaka 1963 hadi mwaka 1966.

Dk. Migiro alihamia Shule ya Msingi Korogwe, Tanga ambapo aliendela na elimu ya msingi mwaka 1967–1969.

Baadaye akajiunga kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Weruweru, Kilimanjaro mwaka 1970 hadi 1973 na Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari Korogwe mwaka 1974 -1975.

Dk. Migiro alikuwa mmoja wa wasichana waliofaulu vizuri Korogwe Sekondari na alipojiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1977, alichukua masomo ya sheria na kuhitimu Shahada yake (LLB) mwaka 1980.

Baadaye aliajiriwa UDSM kufundisha masomo ya sheria kama Mhadhiri Msaidizi. Alifanya kazi hiyo kwa miaka miwili kabla ya kuendelea tena na masomo ya juu ya sheria mwaka 1982–1984 hapohapo UDSM na kutunukiwa shahada ya uzamili (LLM).

Kati ya mwaka 1985–1988, alifundisha UDSM. Mwaka 1988 alikwenda Chuo Kikuu cha Konstanz, Ujerumani ambako alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika masuala ya Sheria mwaka 1992.

Dk. Migiro alirejea Tanzania akiwa Mhadhiri Mwandamizi na aliendelea kufundisha katika Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi mwaka 2000 alipoingia kwenye siasa.

Akiwa UDSM kati ya mwaka 1992 – 1994 Dk. Migiro alikuwa Mkuu wa Idara ya Sheria za Katiba na Utawala.

Kati ya mwaka 1994 – 1997 aliongoza Idara ya Sheria za Makosa ya Jinai (Idara zote zipo katika Kitivo cha Sheria UDSM).

Dk Migiro ni mzungumzaji mzuri katika lugha ya Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani. Ni mke wa Profesa Cleophas Migiro na wana watoto wawili wa kike.

Dk Migiro alianza na siasa za kujijenga akitokea katika taaluma. Mwaka 2000, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alimteua kuwa waziri kwenye Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.

Alitumikia wadhifa huo hadi mwaka 2005 bila kubadilishwa akisimamia mambo mengi ya kisera na kimiundombinu, bila kusahau utekelezaji na upiganiaji wa haki za wanawake na watoto.

Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005, alimteua kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje, Januari 2006 na kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kushikilia wadhifa huo. Katika kipindi cha mwaka mmoja tu, alifanya kazi nyingi za kimataifa zilizomweka katika anga nyingine kisiasa.

Januari 5, 2007, aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu (UN) mpaka 2012 alipomaliza muda wake. Januari mwaka 2013, Dk Migiro aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Desemba 2013 aliteuliwa kuwa mbunge katika Bunge la Tanzania.

Januari 2014 aliteuliwa kuwa Waziri wa Sheria na Katiba, nafasi ambayo alidumu nayo mpaka Rais Kikwete alipomaliza muda wake mwaka jana.

====================

Updates 1800HRS;

===================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Dkt. Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani.

Dkt. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dodoma

04 Mei, 2016
View attachment 344749
Leo naona Amna aidha

Nshazoea uteuzi kamahuo unaendana NA aidha raisi amemteua pdidy kuwa mwekahazina wa
 
siwangemchagua (lizabon) maana huyu amepiga domo sana huku mitandaoni.
 
Back
Top Bottom