Rais Magufuli amteua Dkt. Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS)

Rais Magufuli amteua Dkt. Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS)

Kamteua au katangaza uteuzi wake? Nadhani wao mashushu wanafahamiana wenyewe ki weledi na uzoefu katika shughuli zao na uongozi.

GM aliekuwa anakaimu ndio alikuwa best shoot hapo... Ila kaachwa. Ingekuwa ni 'MTU' tu anaenda kuteua boss pale basi GM angeteuliwa.
Tatizo la Watanzania tunapenda sana kuongea hata masuala yasiyotuhusu
 
Huyu DR si ndio yule alikuwa na Kitwanga kwenye kampuni yao ya ufisadi ya Infosy..?

Lugumi saga
 
Ni mara yangu ya kwanza kuona na kusikia hii nafasi ya mkuu na naibu mkuu kutangaziwa hadharani...
 
Watu wengi wanaofanya kazi ubalozini ni Usalama wa Taifa (Hassy Kitine,Augustine Mahiga,Benard Membe na Othman ) hao wote ni Usalama wa Taifa na walikuwa mabalozi
Pouwa Belo
 
Kamteua au katangaza uteuzi wake? Nadhani wao mashushu wanafahamiana wenyewe ki weledi na uzoefu katika shughuli zao na uongozi.

GM aliekuwa anakaimu ndio alikuwa best shoot hapo... Ila kaachwa. Ingekuwa ni 'MTU' tu anaenda kuteua boss pale basi GM angeteuliwa.
Wanajuana na wewe umemtaja wa kwako tuseme na wewe Mtu wa kazi maalum
 
Hata asingeteuliwa Dr. Kipilimba, mwingine angeteuliwa. Hata angeteuliwa mwingine, pongezi zingetolewa. Na kashifa nyingine zingetolewa. Dr. Kipilimba ni mtu mzima. Katika safari yake ya maisha miaka yote hiyo hawezi kukosa makandokando. Ni kanuni za maisha tuu.

Otherwise, ningefurahi kama waTanzania tungejitahidi kupata mfumo ambao nafasi nyeti kama hizi zinaidhinishwa na bunge. (confirmation). Hiyo ndo njia pekee ya kupata viongozi waadilifu. Na siyo kumlaumu JPM. Tanzania ni kubwa kuliko sisi sote. Miaka 50 ijayo inawezekana 70% tukawa hatupo dunia hii. Tujifunze kujenga misingi imara ya taifa letu kwa faida ya leo na vizazi vijavyo.

Tumpongeze Dr. Kipilimba na tumtakie heri katika kulitumikia taifa letu.
 
Back
Top Bottom