Hata asingeteuliwa Dr. Kipilimba, mwingine angeteuliwa. Hata angeteuliwa mwingine, pongezi zingetolewa. Na kashifa nyingine zingetolewa. Dr. Kipilimba ni mtu mzima. Katika safari yake ya maisha miaka yote hiyo hawezi kukosa makandokando. Ni kanuni za maisha tuu.
Otherwise, ningefurahi kama waTanzania tungejitahidi kupata mfumo ambao nafasi nyeti kama hizi zinaidhinishwa na bunge. (confirmation). Hiyo ndo njia pekee ya kupata viongozi waadilifu. Na siyo kumlaumu JPM. Tanzania ni kubwa kuliko sisi sote. Miaka 50 ijayo inawezekana 70% tukawa hatupo dunia hii. Tujifunze kujenga misingi imara ya taifa letu kwa faida ya leo na vizazi vijavyo.
Tumpongeze Dr. Kipilimba na tumtakie heri katika kulitumikia taifa letu.