Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Safi sana JPM taratibu watakuelewa wewe ni mtu mwenye roho safi na mpenda MAENDELEO.
 
Unatengeneza tatizo na kulitafutia suluhisho kwa ajiri ya cheap politics! Kofuri Mungu atakulipa unachostahili!
 
Akizungumza hotelini hapo Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya amedai kwamba amepata maelekezo kutoka kwa Rais wa Tanzania kwamba Hoteli hiyo isivunjwe kwa vile inavyo vibali vyote vilivyotakiwa kabla ya ujenzi wake na kwamba vyanzo vya maji vilivyopo karibu na hoteli hiyo havijaathirika , hivyo hakuna sababu yoyote ya kuhujumu hoteli hiyo .

Hotel ya Kisasa ya Desderia inamilikiwa na Joseph Mbilinyi aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini

Niliwahi kuweka uzi humu kuhusu jambo hili lakini ulifutwa kibabe bila hata kuupa nafasi ya kuomba maji ya kunywa , bali nilichojifunza ni kwamba UKWELI HAUFICHIKI , leo kiko wapi ?

Rais huyu huyu aliyeamuru kuvunjwa kwa hoteli ya bilicana iliyokuwa kivutio kikubwa kwa watalii kwa kutaka kumkomoa Mbowe
 
Tunaishi kwa hisani ya jiwe na siyo sheria na taratibu za nchi
Umeongea ukweli mtupu........

Yaani hii nchi kwa hivi sasa inaishi kwa hisani ya JPM!

Chukulia mfano halisi wa tukio hilo, mkuu wa Mkoa, anaongea bila aibu kuwa amepata ujumbe kutoka kwa Mheshimiwa Rais kuwa amepiga "Stop" kuwa hiyo hoteli isivunjwe!

Hivi watendaji watakuwa wanafanya kazi kwa maagizo ya Rais na wala si kwa kufuata sheria za nchi?
 
Hahaha, Mdee kakakaa bungeni miaka 15 sijui kawekeza nini ndio wanasumbua sumbua tuu daily
CLEVER BOY, SIO WALE WENGINE WALIOWEKEZA KWENYE MASHINE ZA KUSAGA . UMETUMIA UBUNGE WAKO VIZURI HUTAKUFA NJA
 
Rais Mzalendo na anayejali wawekezaji leo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa tamko au salamu kuwa SUGU au Mbunge mstaafu wa Mbeya Joseph Mbilinyi ni muwekezaji hivyo atalindwa na hotel yake haitabomolewa na mtu yeyote.

Kulikuwa na uzushi mitandaoni kuwa hotel imejengwa kwenye uoto wa asili yaani pembezoni mwa mto hivyo kulikuwa na mpango wa kuibomoa.

Kwa ufupi Rais amesisitiza hilo eneo limepimwa na linafahamika,Watu wa mazingira yaani NEMC wanalifahamu vizuri.

Mkuu wa mkoa ameonyesha jinsi Sugu anavyolinda mazingira ya mto huo huku maji yakitiririka na kumiminika.

Aidha Bwana SUGU amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuhakikishia hilo na kujenga imani kwa wawekezaji wengine.

Maendeleo hayana chama

View attachment 1659613
Tatizo lilikuwa ni ubunge tu, wameshafanikiwa kumpora ubunge hawana shida naye tena.

Kinachojamba ushuzi ni tumbo, matako ni spika tu.

Aliyetowa amri ya kuvunja ndiye aliyetowa amri ya kusitisha uvinjaji.
 
Labda wakati mwingine mtu anajisikia aibu ,
Ujue unaweza kufanya ukatili mpaka mwenyewe unajistukia
 
Wakati wanajenga hao NEMC walikuwa sayari gani
Hizi institutions zimejaa matapeli. Wao ndio waliotoa permit. Halafu bila aibu wanaenda kubomoa.
Tumuogope Mwenyezi Mungu. Haya mambo ya aina hii tutayalipia
 
Tatizo lilikuwa ni ubunge tu, wameshafanikiwa kumpora ubunge hawana shida naye tena.

Kinachojamba ushuzi ni tumbo, matako ni spika tu.

Aliyetowa amri ya kuvunja ndiye aliyetowa amri ya kusitisha uvinjaji.
Swadakta
 
Ndugu Yangu Suguuu!
Jifunze kuwa na Diplomasia ya Kiafrika, Umeingia kwenye biashara sharti uachane na Uanaharakati hizo mbwembwe zako za kuanza Kujidai Oooooooh Makaratasi yote ninayo hazina mantiki wala tija yoyote just play low brother huwezi pungukiwa na kitu. Achana na jeuri, Ubabe na Uanaharakati chagua kimoja. Tunajua Wanyaki ni Jeuri lkn ukiendekeza hizo swagga zako za Kijuaji ippo siku utabaki na makaratasi yako na hoteli imevunjwaaaa.
Ni hayo tuuuu, we endelea kujimwambafai ooooh makaratasi yote ninayo🤣🤣🤣🤣
 
Shangazi yangu hajawahi kupata hiyo fursa ya kuwa mbunge kwa miaka 15 mfululizo au kuwa mtetezi wa kampuni ya acasia. Tunachoshangaa ni mtu aliyewahi kupata fursa kama hizo lakini hana cho chote alichowekeza hapa nchini na baada ya kukosa kuendelea na fursa hizo anaamua kuishi maisha ya ukimbzi nje ya nchi.
Unao uhakika au sababu wewe ni CCM ndiyo uhakika wako! Elimu yako na kipato chako kheri ungejinyamazia tu, mlo wako ni wakuungaunga
 
Lipo wazi hilo visasi vyake huwa haviishi.
Hao hao nemc ndio waliotoa vibali vya ujenzi na ndio hao hao watakao jengo livunjwe. Wanaweza wakawa wanamkoa Sugu sawa atakaa kimya serikali nyingine ikingia anashtaki na anashinda analipwa fidia ya jengo plus faida ya KILA siku kwa miaka yote hio. Tuoneeni huruma Kodi zetu kwani ndizo zitakazotumika kuwalipa fidia wengi awamu ijayo sababu ya mkurupuko wa mtu mmoja tu asiye na uchungu na kodi zetu. Maana serikali ipo awamu ndizo upita. Hata wa kimara watashinda kesi usione wamekaa kimya tu wanasubiria mwingine akiingia tu kesi zinafufuka Hawa watawala wanapita lakini haki za watu hazitopita asipolipa anaye atalipa mwingine.
Sio kila madaraka yana mwisho,,wengine madaraka yetu hayana mwisho mpaka kufa..mfano mimi ni mkulima,nitakua mkulima daima
 
Tuendelee kuwatia moyo wawekezaji, hasa wazawa ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi.
 
Ni maamuzi yenye Afya sana kwa mustakbari wa maendelwo ya Mbeya na TZ kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom