Rais Magufuli anahoji; Je, ninyi hamuamini kuwa yupo Mungu?

Bunge lingekuwa credible walistahili kuanza mchakato wa impeachment. JPM hafai, ameshindwa kuongoza nchi wakati wa janga.
 
una mapepo wewe sio bure mpaka unasema hakuna Mungu
Naona umekariri mapepo,mapepo ...mpaka unashangaza! Mwenye post yake amesema Hakuna Mungu anayewaambia watu wawe wapumbavu. Ndio,huwezi kumuomba Mungu akuponye na korona huku ukiacha kuchukua tahadhali kulingana na miongozo ya kitaalamu. Kama kuvaa barakoa na social distancing. Kumuomba Mungu bila kuchukua hatua ni kumkejeli. Ni upumbavu!
 
Bunge lingekuwa credible walistahili kuanza mchakato wa impeachment. JPM hafai, ameshindwa kuongoza nchi wakati wa janga.

..halafu kila anapokweda kuna mtambo nadhani wa hewa unawekwa karibu yake. pia hakai karibu na viongozi wenzake. wakati huohuo anawaambia wengine wasichukue tahadhari.
 
Tatizo leo omba Mungu kesho weka ndani yule bila kosa Mungu wa hivyo hayupo.
 
Ukiwa na tabia ya kutukana wengine bila sababu unapoteza hekima ya asili,kakukosea nini?Kila mmoja aachwe atoe hoja na mawazo yake kwa Uhuru.Don't Judge people according to your own mentality, every one have the right to express themselves.
For stupid questions, sometimes a backflip sends a message faster!
 
Na yeye kwanini anazungukwa na Walinzi lukuki usiku na mchana popote alipo huwa haamini Mungu yupo?? Haamini ulinzi wa Mungu juu yake??

Watz siyo Wajinga. Eti walale usiku bila kufunga milango kisa Mungu yupo atawalinda!!
 
Yapo matukio ya ajabu kama haya; wasabato wa uwanja ndege JKN wakitaka kwenda ughaibuni kwa miujiza bila nauli. Wapo wachungaji wanasema wanaponya ukimwi. Wengine wanakataza waumini kumeza dawa.
Lakini Mungu alitupa akili ambayo pia ni miujiza yake.
Mfano tuna akili ya kupanda mbegu kuongeza chakula kwa hivi hatuwezi kuomba Mungu miujiza kupata chakula.
Tuna akili kama mfano wake tulioumbiwa. Tusimjaribu kwa kutaka miujiza.
 
John Pombe Joseph Magufuli alipopitishwa kuwa mgombea wa CCM alisema "..nitamtanguliza Mungu mbele, na sitowaangusha...". Hotuba Yake baada ya kuapishwa ilikuwa na maneno haya.

Shambulio la covid-19 anapambana nalo kwa kauli hii hii. Mapokeo ya Watanzania wakati ule wa kuapishwa na sasa dhidi ya covid-19 yamekuwa tofauti. Watanzania walipenda alivyomtanguliza Mungu kuanza uongozi, lakini wamegawanyika sasa wakati wa vita dhidi ya covid-19.

Nasubiri Magufuli astaafu nimuulize kwa nini Watanzania wamepokea tofauti kauli yake ya "... nitamtanguliza Mungu mbele..?
 
Mwisho wa siku mmechezea tu mpapaso , mnaambiwa muandamane mnaishia tu kutoa mapovu mitandaoni, endeleeeni na ndoto zenu ma keyboard warriors
 

Kumwamini Mungu ni jambo moja ila haiondoi umuhimu wa kupractice common & sensible preventive measures.

Hata Kitabu kitakatifu kimesema wazi kwamba “watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa......
 
Mpambane sasa sio uanaharakati wa keyboard tu sasa mnakamatwa mnarudi nyuma??si mnapendaga kujipa moyo mkiona huko wenzenu wa nchi nyingine wanakinukisha kweli , hao wakishikwa wanaachaga kuandamana? Just a bunch of cowards mtatishia mapunguani tu
 
Kama ana itikadi Kali hivyo kama wasabato walokwenda airport Mungu awapeleke (sijui ulaya?) Haspitali zinajengwa za nini?
Wasabato Masalia wanaitwa, wapumbavu sana, sasa si wangeenda ulaya wakiwa kanisani kwao, walienda airport kufanya nn?
 
Katulizwa....mtatulizwa wakija wapumbavu wengine watatulizwa nyie leteni maneno wenye nguvu wanafanya vitendo tu.........yaani hata ukipiga chafya tu utatulizwa endeleeni na ukamanda wenu wa keyboard na majina yenu bandia ndo kitu pekee mnachoweza,,,, taarabu mingi....mlidhani nchi mnapewa kwa kuimba taarabu tu mitandaoni ...........mwanaume vitendo sio taarabu nyuma ya keyboard na ma kemera.....yani unalia unashindwa kujikomboa kisa unakamatwa sasa ulidhani ukombozi ni kama kuletewa keki ya besdei magetoni..........textbook warriors.....
 
sasa wewe unaona yupo sawa kuandika hivyo nawewe utakua na mapepo tu sio bure. Ilitakiwa aandike Mungu huwa hawaambii watu wawe wapumbavu. Hiyo kauli ya hakuna Mungu ambaye maana yake anaaminisha kuna Mungu zaidi ya mmoja. Mapepo yakiwa kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…