Rais Magufuli anahoji; Je, ninyi hamuamini kuwa yupo Mungu?

Rais Magufuli anahoji; Je, ninyi hamuamini kuwa yupo Mungu?

Acha unafiki

Kama wewe unaelewa sio wote wataaoelewa

Hebu fikiria kama huduma ndogondogo za kijamii zinapatikana kwa shida vipi kuhusu vingine
Nimekuuliza wamekutuma uwasemee! Rais ameagiza yafanyike maombi ya siku tatu kuliombea taifa liondokane na corona, hiyo kwa mawazo yako unaona bd haitoshi! Unahisi watz bado hawajaewa!?
 
Sijui kama kwali hiyo roho ya kiungu kama imo ndani mwake au anajisemea tu. Kama anamwamini Mungu na hayo anayotuambia sisi juu ya Corona, ni rahisi kujiuliza majeshi yote yanayomzunguka ni ya nini? Watu hawasemi tena wala hawatoi maoni yao hadharani kwa mambo mepesi. Biblia inatuambia tuishike elimu na tusiiache iende zake, yet yeye hataki watu japo watumie sayansi kutafiti na kuelewa juu yajanga hili. Hataki hata itajwe kuwa Tanzania corona ipo. Sijui wanataka kumdanganya nani na huo uwongo sijui kama ndio tiketi ya kukaa karibu na Mungu. Mi nadhani kama ni ya kaisari basi apewe kaisari na hayo ya Mungu aachiwe Mungu. Tusije tukamjaribu Mungu tukavuna yatakayotuangamiza na vizazi vyetu. Mungu ni wa kweli na ni wa haki. Tujitafakari!
 
Nimekuuliza wamekutuma uwasemee! Rais ameagiza yafanyike maombi ya siku tatu kuliombea taifa liondokane na corona, hiyo kwa mawazo yako unaona bd haitoshi! Unahisi watz bado hawajaewa!?
Amesema waombe
Hajathibitisha kama covid ipo
Tumia akili
 
Mhe. Rais naona ameumaliza mzizi wa fitina leo katika mazishi ya Balozi Kijazi na kusema kuwa magonjwa yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, na sisi si pekee ndiyo tunaotaabika na matatizo haya ya magonjwa ya milipuko hata nchi zingine wamekufa wengi sana. Na tatizo linapokuwa kubwa kuzidi uwezo wa binadamu tulisogeze kwa Mungu.

Rais anasema mwaka jana tulimuona Mungu akitusaidia lakini sasa naona wengine hawana imani tena wanatengeneza taharuki na kutishana mimi sifanyi lokudauni tuchape kazi Mungu yupo. Kwanini au amwamini kuwa Mungu anaweza kuishinda Korona?

Mimi mtoto wa mchungaji nahoji hivi hawa baadhi ya viongozi wa dini ambao nao pia wanaogopa Corona kiasi cha kwamba wanatushauri tuwasikilize watu wa afya na wamitandaoni hivyi hawa watumishi wa Mungu si wangeacha hiyo kazi na kuja huku mchangani ijulikane moja.

Nawauliza na ninyi wana janvi Mungu yupo au, maana babuzetu waliomba mvua zilinyesha, waliomba nzige waondoke asubui waliwakuta chali kificha mende, magonjwa ya mlipuko hayakuwagusa, hivi na yule Mungu wa babu zetu yupo wapi siku hizi na huyu wa kanisani na msikitini yupo wapi.
Sijui kama kweli hiyo roho ya kiungu kama imo ndani mwake au anajisemea tu kulingana na tafsiri yake. Kama anamwamini Mungu na hayo anayotuambia sisi juu ya Corona, ni rahisi kujiuliza majeshi yote yanayomzunguka ni ya nini? Kwanini yeye ulinzi wa Mungu usimtoshe? Watu hawasemi tena wala hawatoi maoni yao hadharani kwa mambo mepesi, kama hata kuvaa barakoa. Biblia inatuambia tuishike elimu na tusiiache iende zake, yet yeye hataki watu japo watumie sayansi kutafiti na kuelewa juu yajanga hili. Hataki hata itajwe kuwa Tanzania corona ipo. Sijui wanataka kumdanganya nani na huo uwongo sijui kama ndio tiketi ya kukaa karibu na Mungu. Mi nadhani kama ni ya kaisari basi apewe kaisari na hayo ya Mungu aachiwe Mungu. Tusije tukamjaribu Mungu tukavuna yatakayotuangamiza na vizazi vyetu. Mungu ni wa kweli na ni wa haki. Tujitafakari!
 
Kwa waganga wa kienyeji kinatafutwa nini?

Mhe. Rais naona ameumaliza mzizi wa fitina leo katika mazishi ya Balozi Kijazi na kusema kuwa magonjwa yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, na sisi si pekee ndiyo tunaotaabika na matatizo haya ya magonjwa ya milipuko hata nchi zingine wamekufa wengi sana. Na tatizo linapokuwa kubwa kuzidi uwezo wa binadamu tulisogeze kwa Mungu.

Rais anasema mwaka jana tulimuona Mungu akitusaidia lakini sasa naona wengine hawana imani tena wanatengeneza taharuki na kutishana mimi sifanyi lokudauni tuchape kazi Mungu yupo. Kwanini au amwamini kuwa Mungu anaweza kuishinda Korona?

Mimi mtoto wa mchungaji nahoji hivi hawa baadhi ya viongozi wa dini ambao nao pia wanaogopa Corona kiasi cha kwamba wanatushauri tuwasikilize watu wa afya na wamitandaoni hivyi hawa watumishi wa Mungu si wangeacha hiyo kazi na kuja huku mchangani ijulikane moja.

Nawauliza na ninyi wana janvi Mungu yupo au, maana babuzetu waliomba mvua zilinyesha, waliomba nzige waondoke asubui waliwakuta chali kificha mende, magonjwa ya mlipuko hayakuwagusa, hivi na yule Mungu wa babu zetu yupo wapi siku hizi na huyu wa kanisani na msikitini yupo wapi.
 
Labda huwa anamaanisha MUNGU = Muujiza Unaopatikana Nje Gizani Usiku

Kwa ufupi ni ushirikina.
 
Kwahiyo Mungu akamwambia Jiwe tusitumie akili alizotupa na maarifa aliyotupa ila kuepuka magonjwa .
 
Tatizo sio Mungu hayupo ila tunaomba atangaze hadharani kua C19 ipo ili tahadhari zianze kuchukuliwa.

😷 😷😷😷😷😷😷😷
Kwa hy mpaka sasa hachukui hatua unasubiri rais atangaze, Ignorance! Chukua hatua Covid imejaa tele mze baba.
 
Achana na mambo ya score twende kwenye point
Haya bana! Tuishie hapo😂🤣😂! Maombi mema!
Mungu tunaomba utusamehe kwa maovu yetu yote ambayo ni mengi sana tuliyoyatenda! Mungu tunaomba uturehemu sisi watanzania wote! Mungu tunaomba utuponye magonjwa yetu yote tuliyonayo ikiwa pamoja na hii tauni ya corona! Mungu tunaomba uiponye na nchi yetu yote na kila aina hatari, majanga, magonjwa, machafuko, dhoruba, na hofu zote! Tunaomba haya katika jina lipitalo majina yote, jina la Yesu Kristo, amen!
Mungu tunaomba uzidi kumlinda kumuongoza na kumbariki rais wetu mpendwa Mh Dr JPM na serikali zetu zote! Mungu azidi ibariki na kuilinda nchi yetu Tanzania, amen!
 
Nimeona leo kwenye mitindao muheshimiwa Sana ,mtukigu Rais anatuamasiha waumini wa dini za kikristo,kiislamu na kisabato tusali na kufunga na kwamba tumtegemee MUNGU tu

Je ,ana hofu na Nini?

Tuko uchumi wa Kati kwani shida iko wapi?

Mbona kila siku tunaenda kwenye nyumba zaidi iweje leo kwenye kuaga mwili wa kijazi asisitize Sana hivyo ana hofu gani?

Tuendelee kupiga nyonga[emoji1]
View attachment 1706217
Wewe unachanganya siasa na dini, uchumi wa kati unahusiana vipi na kuomba MUNGU kuhusiana na Corona. Marekani wana uchumi wa 1 lakini wanakufa wewe unaongelea uchumi wa kati, chini.... non-sense.
 
Pia kuna mambo mengine kama ya kuvaa barakoa kwenye public au kupunguza misongamano kwenye vyombo vya usafiri, kuweka sanitizers nk hivyo haviwezi kufanyika sawaswa bila maelekezo ya serikali
Wakati tulipoingiliwa na huu ugonjwa kwa mara ya kwanza mwaka jana maafisa afya walikuwa wanatembelea sehemu za biashara kuhakikisha kuna maji ya kunawa na sabuni. Hivyo hivyo ilikuwa kwenye vyombo vya udafiri na mahali pengine penye mikusanyiko ya watu. Sasa hivi hatuoni hayo. Imefika mahali hata kutamka tu covid 19 ni kosa. Haki ya kutoa tahadhari imehodhiwa na baadhi ya viongozi. Viongozi wengine wakifanya hivyo wanapata misukosuko. Hii si sawa
Kwa ujumla serikali inakwepa wajibu wake kwa kisingizio kuwa watu wanaona hali hivyo wachukue tahadhari. Mbona kwenye kujifukiza na dawa za asili wako wazi na wanazipigia kampeni waziwazi. Kwa nini was ifanye hivyo kwenye mengine ambayo ni ya kuzuia tu na si kuponya.
 
Ambayo ni yapi kwa mfano?.
 
Ni Africa ila it is changing

Siku ya siku inafika,wale mliozoea unapiga wananyamaza watakugeuza kitoweo

Hata Ulaya ilikua hivi back in the days,walipita hii phase...Africa inavuta sooner
Sio bongo walipojaa ma keyboard warriors labda miaka 1000 ijayo
 
Back
Top Bottom