Rais Magufuli anahoji; Je, ninyi hamuamini kuwa yupo Mungu?

Rais Magufuli anahoji; Je, ninyi hamuamini kuwa yupo Mungu?

Kamwe huyu Mungu tunayemwabudu Wakristo Mungu wa Abraham, Izaka na Yakobo siye Mungu anayemwabudu Magufuli.

Kwa matendo aliyowatendea wenye vyeti feki, aliowatumbua kazini, aliowapeleka Segerea, aliowaua kwa kikundi cha WASIOJULIKANA, anaowanyima nyongeza za mishahara, anaowabomolea nyumba Kimara kamwe hawezi kuomba Mungu akamsikiliza. Kwa namna anavyoacha watu wasichukue tahadhari kwenye Corona, huyu hawezi kuwa anamuamini Mungu.

Labda mungu (m- ndogo) wa Gwajiboy, Mch Mashimo na Sheikh Alhad wa Dar ambao anaomba nao kila mara
Mungu anapenda vyeti feki si ndiyo?
 
Mbona anafanya ubabe wa kikatili alafu anasingizia Mungu au mwenzetu huwa anamaanisha mungu wake anaemjua.

Kwa aliyo yafanya na anayoyafanya huwa akitaja taja jina LA Mungu huwa namshangaa sana.
Magufuli ana mungu wake anaepelekewa sadaka za kafara kila mara: Ben Saanane ,Azory Gwanda, Kanguye, Akwilini n.k
 
Mhe. Rais naona ameumaliza mzizi wa fitina leo katika mazishi ya Balozi Kijazi na kusema kuwa magonjwa yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, na sisi si pekee ndiyo tunaotaabika na matatizo haya ya magonjwa ya milipuko hata nchi zingine wamekufa wengi sana. Na tatizo linapokuwa kubwa kuzidi uwezo wa binadamu tulisogeze kwa Mungu.

Rais anasema mwaka jana tulimuona Mungu akitusaidia lakini sasa naona wengine hawana imani tena wanatengeneza taharuki na kutishana mimi sifanyi lokudauni tuchape kazi Mungu yupo. Kwanini au amwamini kuwa Mungu anaweza kuishinda Korona?

Mimi mtoto wa mchungaji nahoji hivi hawa baadhi ya viongozi wa dini ambao nao pia wanaogopa Corona kiasi cha kwamba wanatushauri tuwasikilize watu wa afya na wamitandaoni hivyi hawa watumishi wa Mungu si wangeacha hiyo kazi na kuja huku mchangani ijulikane moja.

Nawauliza na ninyi wana janvi Mungu yupo au, maana babuzetu waliomba mvua zilinyesha, waliomba nzige waondoke asubui waliwakuta chali kificha mende, magonjwa ya mlipuko hayakuwagusa, hivi na yule Mungu wa babu zetu yupo wapi siku hizi na huyu wa kanisani na msikitini yupo wapi.
Imani bila matendo imekufa
 
Kumjua Mungu sio kumtaja ni kuishi matendo.Anaemjua Mungu katu hawezi umiza watu huko ni kumfanya Mungu mjomba.
 
Mungu ashikamani na watu dhalimu,watu dhaifu,watu wenye dhambi,washirikina.
 
Watu Hawa wanapotaja mungu sio Mungu Jehovah bali umtaja kinyume ktk ulimwengu wa roho.
 
Jamaa ni mwepesi sana kumtaja mungu,japo yeye mwenyewe haonekani kuwa na guidance ya mungu bali ya shaitwani
 
Usimjaribu bwana Mungu wako!
Alitupa akili na tuzitumie tusiuogope ukweli korona IPO na inaua tahadhari za kisayansi na zizingatiwe
 
Hu ukristo ulikoanzia kwa taifa teule ni wabobezi wa sayansi na wanaitumia vilivyo kupambana na maradhi. Sisi na Kinjikitile na risasi kugeuka maji!
 
Tatizo sio Mungu hayupo ila tunaomba atangaze hadharani kua C19 ipo ili tahadhari zianze kuchukuliwa.

😷 😷😷😷😷😷😷😷
Kama Watanzania wana Mtazamo kama wa kwako kwamba wanataka mpaka watangaziwe ndio wachukue tahadhari basi naanza kuwaza juu ya ulewa mdogo wa kufikiri wa watu.

Sasa Rais Akitangaza ndio Atabadilisha nini? Kama wewe unashidhwa kujiongoza mpaka uambiwe basi umeshikiwa Akili zako.

Pia niseme.
Mimi naungana mkono na Ndugu Rais Watanzania Tuondoe hofu. Tusi focus sana kwenye corona tuka sahau kwamba yako magonjwa mengine Ambayo ni hatari hata kuliko korona.

Unaweza ukajilinda kwa kujisiriba mibarakoa nakujifukiza na mikaratusi. Ukafa kwa malaria au Ajali.

Binadamu kifo kinatuwinda mchana na usiku lakini Tukiwa karibu na Mwenyezi Mungu Anatuepushia na Maradhi yote.

Tuache dhambi tumrudie Mwenyezi Mungu. Maovu yamekua mengi sana. Corona haiwadhuru Watoto il a inawaathiri watu wazima tujiulize kulikoni kwa watu wazima? Utagungua Dhambi imezidi.
 
Angekuwa anamjua huyo Mungu asingeumiza watu Wala kuwasomesha namba
 
Mhe. Rais naona ameumaliza mzizi wa fitina leo katika mazishi ya Balozi Kijazi na kusema kuwa magonjwa yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, na sisi si pekee ndiyo tunaotaabika na matatizo haya ya magonjwa ya milipuko hata nchi zingine wamekufa wengi sana. Na tatizo linapokuwa kubwa kuzidi uwezo wa binadamu tulisogeze kwa Mungu.

Rais anasema mwaka jana tulimuona Mungu akitusaidia lakini sasa naona wengine hawana imani tena wanatengeneza taharuki na kutishana mimi sifanyi lokudauni tuchape kazi Mungu yupo. Kwanini au amwamini kuwa Mungu anaweza kuishinda Korona?

Mimi mtoto wa mchungaji nahoji hivi hawa baadhi ya viongozi wa dini ambao nao pia wanaogopa Corona kiasi cha kwamba wanatushauri tuwasikilize watu wa afya na wamitandaoni hivyi hawa watumishi wa Mungu si wangeacha hiyo kazi na kuja huku mchangani ijulikane moja.

Nawauliza na ninyi wana janvi Mungu yupo au, maana babuzetu waliomba mvua zilinyesha, waliomba nzige waondoke asubui waliwakuta chali kificha mende, magonjwa ya mlipuko hayakuwagusa, hivi na yule Mungu wa babu zetu yupo wapi siku hizi na huyu wa kanisani na msikitini yupo wapi.
Kama Huna imani kumuelewa Mzee Magu ngumu kidogo imani ni kuona jambo lililopo halipo na lisilokuwepo lipo sasa kww macho haya ya nyama huwezi ona ila kwa macho ya imani vinaonekana...

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo sio Mungu hayupo ila tunaomba atangaze hadharani kua C19 ipo ili tahadhari zianze kuchukuliwa.

[emoji40] [emoji40][emoji40][emoji40][emoji40][emoji40][emoji40][emoji40]

Umegundua kitu kizuri sana!! Watawala wanaotaka namna zao ndio zitumike, humtaja Mungu. Tawala za kale ziliungana na dini ili kutuliza na kutiisha watu!!

Ajabu ni kuwa wanaotaka hatua madhubuti zichuliwe wanadhihakiwa kwa dhana kuwa vifo havikwepeki na kuna magonjwa mengi tu yanaua. Anasahau kuwa covid hata isipoua mtu wako, itakufanya ukose kazi na biashara ife - jambo ambalo ugonjwa wowote haujafanya!! Anasahau kuwa sisi ni sehemu ya dunia kiuchumi - kuisha haraka kwa ugonjwa huu ndio kurudi haraka uchumi wa dunia!!

Mitazano ya kiwango cha chini sana kujadiliwa na mtu mwenye cheo kama kile katika jamii! Anasahau pamoja na mamlaka na uwezo wa Mungu - hatujawahi kusema tusitumie chandarua, tusinywe maji safi, tuendesh vyombo vya moto kwa kasi nk eti kwa kuwa Mungu ndiye mwamuzi wa kila kitu!!
 
Back
Top Bottom